Na Shaffiru Makosa & Muharami Matenga- kigoma
Wakati jitihada mbalimabli zikiendelea
kufanywa na serikali kwa lengo la kudumisha amani na upendo miongoni mwa wanajamii ya watanzania
Kaimu sheikh mkuu wa mkoa wa Kigoma wa
baraza kuu la waislamu Tanzania bakwata Alhaji Hassan Kibulwa ameunga mkono hatua hiyo ya kudumisha amani na upendo nchini kwakuwataka
viongozi wa dini kutekeleza maazimio mbalimbali ya vikao vya mabaraza ya mahusiano mema vinanavyo
shirikisha viongozi wa dini zote kwa lengo la
kudumisha amani na upendo ha pa
nchini.
Alhaji kibulwa ameyasema hayo katika
kikao maalum cha baraza kuu la waislamu Tanzania bakwata mkoa wa kigoma kilichoshirikisha
viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kwa shabaha ya kujadili mustakbali wa
amani ya mkoa huu ikiwa ni pamoja na
kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya
kidini inayoendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hapa mkoani Kigoma .insert
….
Alhaji Kibulwa amekemea tabia ya
baadhi viongozi wa dini wa kiislamu
wanaotumia maandamano kama silaha ya kuishinikiza
serikali kutekeleza madai yao jambo ambalo ni kwenda kinyume kabisa na mafundisho ya mtume muhamadi (s.a.w)
Licha ya shekhe kibulwa kuwataka
viongozi hao wa dini ya kiislamu na wakiristu kutataua changamoto zinazohatarisha mahusiano ya waumini wao kwa njia ya kidiplomasia pia akatoa wito kwa viongozi hao kujishughulisha
katika kutafuta ufumbuzi wa chanagamoto za kimaendeleo kwa waamini wao ikiwemo
za kielimu na kiuchumi badala ya kujikita katika masuala
ya kiimani pekee.
No comments:
Post a Comment