Na Magreth Magosso,Kigoma.
Polis Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia
Mabomu ya machozi ili kuwatawanya waendesha Bodaboda wa Manispaa ya
Kigoma Ujiji, baada ya kufanya maandamano ya kutaka askari wa
barabarani wasitumie nyadhifa zao kwa maslai yao binafsi.
Kauli hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa
waendesha Bodaboda Fikirini Shaban eneo la maweni, kudai kuwa,askari hao wana
tabia ya kuwasimamisha waendesha bodaboda si kwa tija ya kuwakosoa na
kuwaelimisha kwa makosa husika, bali hutaka kiasi cha fedha kuanzia 10,000 hadi
sh.5,000 ili uendelee kufanya kazi,la ukikataa kusimama watakuandama kwa
kufukuzana nao barabarani hali inayosababisha ajali zisizo tarajiwa.
“Baadhi ya abiria hukataa kuvaa kofia ,lakini
askari akikusimamisha na ukisimama wanatoza fedha isiyo na tija kwa serikali
huweka mifukoni mwao jana ajali ilitokea na kujeruhi watu watatu kisa
hakusimama baada ya askari kumsimamisha kwa kuhofu kutolewa sh.10,000
ukibana sana unatoa 5,000 eti ya mafuta tena hakuna risiti” alibainisha
Kaopa Denis mwendesha pikipik.
Mganga Mkuu wa Kigoma Leonard Subi alikiri
Hospitali yake jana ilipokea majeruhi wa ajali hiyo na kubainisha kuwa,
waliolazwa hadi sasa wapo watatu ambao hali zao si za kuridhisha.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,
Dismas Gapikisusi alidai kuwa,tukio hilo bado linafanyiwa mkakati wa kuweza
kulitolea jibu maalum na kumtaka mwandishi wa gazeti hili asubiri siku wandishi
wa habari watakapoitwa ili abainishe ukweli wa mambo.
Wakati huohuo baada ya waendesha bodaboda
kufanya mandamano hayo sanjari na kutupa jaketi za kuakisi mwanga
kituo cha polisi kati Kigoma, Waendesha pikipiki wanne
wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Kigoma kwa kosa la kufanya
fujo polisi leo.
No comments:
Post a Comment