WAKATI Ushindani mkali ukiendelea kati ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya
ukizidi kuwa mkali zaidi kati ya Waziri Mkuu wa nchini hiyo Raila Odinga na Uhuru
Kenyatta watu zaidi ya 20 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa
kuuwawa baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa
na Kilifi saa chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.
Saa chache kabla ya uchaguzi huo,
askari polisi tisa waliuawa katika mashambulizi yaliyotokea kwenye miji ya
Mombasa, Kilifi na Kwale na kuacha wavamizi wapatao 10 na raia wa kawaida
watatu pia wakifariki.
Baada ya vifo hivyo, serikali ilipeleka
vikosi vya askari kutoka Mariakani Barracks kwenda kutuliza ghasia hizo wakati
kundi lingine la askari lilitoka Nyali Barracks ili kuweka doria katika miji ya
Mombasa na North Coast.
Taarifa zilizopatikana baadaye jana
zilisema kuwa kwenye mji wa Mombasa askari polisi wanne waliuawa na watu zaidi
ya 100 waliovamia kituo cha kura cha Miritini.
Polisi pia ilithibitisha kuuawa kwa
watu saba katika mapigano hayo huku na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.
Wavamizi wengine waliuawa katika miji
ya Kisauni na Kilifi huku polisi wanne wakiuawa Chumani na mmoja huko Chonyi
huku watu watatu wakiuawa kwa kupigwa risasi.
No comments:
Post a Comment