Friday, October 26, 2012

WANAOTUHUMIWA KUMUUA BARLOW WATAJWA

DIRA YA LEO: WANAOTUHUMIWA KUMUUA BARLOW WATAJWA: Majina hayo yametajwa na Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said...

Wednesday, October 24, 2012

ARSENAL, MAN CITY & MADRID ZAAMBULIA PATUPU

 Timu za Arsenal, Man City, na Read Madrid zimeambulia vipigo katika ligi ya mabingwa Ulaya iliyofanyika usiku wa leo jumatano ya tareh 24 October 2012.katiak michuano hiyo Arseanal imeambulia kipigo cha mabao mawili bila kutoka kwa Schalke Huku Man City ikipigwa tatu moja kutoka kwa Ajax. kwa matokeo zaidi angalia jedwali la matokeo hapo chini













 Champions League - Group A (Table)
 22:41October 24 

 FTDinamo Zagreb0 - 2Paris S.G.

 FTFC Porto3 - 2Dynamo Kyiv



 Champions League - Group B (Table)
 22:41October 24 

 FTArsenal0 - 2Schalke

 FTMontpellier1 - 2Olympiakos Piraeus



 Champions League - Group C (Table)
 22:41October 24 

 FTZenit St. Petersburg1 - 0Anderlecht

 FTMalaga1 - 0AC Milan



 Champions League - Group D (Table)
 22:41October 24 

 FTAjax Amsterdam3 - 1Manchester C.

 FTBorussia Dortmund2 - 1Real Madrid

Tuesday, October 23, 2012

MAN U. YAIBUKA KIDEDEA CHELSEA CHALI

MAN YAIBUKA KIDEDEA CHELSEA CHALI
Matokeo machi za ligi ya mabingwa Ulaya.








Champions League - Group E
 22:44October 23 

 FTFC Nordsjaelland1 - 1Juventus

 FTShakhtar Donetsk2 - 1Chelsea



 Champions League - Group F
 22:44October 23 

 FTBATE Borisov0 - 3Valencia

 FTLille0 - 1Bayern Munich



 Champions League - Group G
 22:44October 23 

 FTSpartak Moscow2 - 1Benfica

 FTBarcelona2 - 1Celtic



 Champions League - Group H
 22:44October 23 

 FTGalatasaray1 - 1CFR Cluj

 FTManchester U.3 - 2Braga

POLISI WAWILI WATELEKEZA LINDO NA KUFANYA KAZI YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Askari Polisi  wawili wametelekeza lindo lao na kuingia barabarani kukamata dalala iliyokuwa imepeba abiria kutoka malimbe kuelekea katikati ya jiji la Mwanza.
Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa mbili usiku eneo la ATM katika chuo cha SAUT ambapo askari hao waliokuwa lindo katka bank iliyopo eneo hilo waliacha kazi yao na kwenda kukamata daladala yenye namba za usajili T 130 BUK inayofanya safari za Buhongwa Kishiri.

Askari hao walidai kuwa daladala hiyo imebadilisha ruti kitendo ambacho ni kinyume na sheria.  Tuakio hilo lilizusha mabishano kati ya askari hao na derevairia wa gari hilo huku askari hao wakiwaamuru abiria zaidi ya 15 waliokuwa ndani ya gari hilo washuke na kusubiri gari jingine.
"Abiria wote shukeni na doreva weka gari pembeni na uizime" alisikika mmoja wa askari hao akitoa amri hiyo ambayo dereva wa gari hilo hakuitekeleza akidai kuwa gari hiyo ikizimwa haitowaka tena.

Kushindwa kutekelezwa kwa amri hiyo ilipelekea askari mmoja kuchukua funguo za gari hiyo hali iliyopelekea kuzima kwa gari hiyo na kushindwa kuwaka tena.

Baadhi ya abiria waliokuwemo ktk daladala hiyo walilalamikia kitendo hicho huku wakishangazwa na kitendo cha polisi hao kuacha kazi yao ya kulinda bank na kwenda kukamata magari kazi ambayo inatakiwa ifanywe na askari wa usalama barabarani. Mpaka mwandishi wa habari hizi anatoka eneo hiko majira ya saa saa tatu kamili daladala hiyo ilikuwa bado imeshikiliwa na askari hao huku wakimuamuru dereva aliwashe gari hilo na kuliondoa barabarani na dereva akidai kuwa gari hiyo haiwezi kuwaka.

Sunday, October 21, 2012

HARUSI HARUSI HARUSI


Ndugu jamaa na marafiki mnataarifiwa kuwa Mpendwa wenu, ndugu Butije Hamisi Butije anatarajia kufunga ndoa mnamo tareh 29 December 2012 itakayofanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Mnaombwa kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo.
Pia unaombwa mchango wako ili kumuunga mkono ndugu yetu katika kufanikisha tukio hilo muhimu.
unaweza kutuma chango wako kupitia M-PESA kwa namba zifuatazo:
        0752 231172 or 0769454447

Kwa maelezo zaidi pia waweza piga namba tajwa hapo juu.
Ndugu, Butije Hamisi

1 YEA OLD GIRL BECAME PREGNANT



Astonishing how a twin can find the sister's foetus.  []
Mengru found parasitic twin inside 
Shocking event for Chinese medicine, which found that  a year old girl is pregnant,

Mengru Kang was taken to hospital after her stomach was found unexpectedly much swollen . After doing a CT scan, the doctors were amazed to find that the girl has a baby in her womb; the baby is the child's twin brother .Doctors say that the embryo was not fertilised in the mother's womb but instead has somehow  landed in his twin sister's womb where it began to grow. Little Mengru will undergo a Cesarean delivery  .This unusual phenomenon, whih is very rare, is known as a "foetus within a foetus" and can only happent once in every 500,000 pregnancies.  

  []
 
STUNNED doctors have discovered a one-year-old girl is carrying a BABY in her tummy. Little Kang Mengru, from China , left medics baffled after her belly became enlarged. Doctors carried out a CT scan to discover the cause of the growth and found a foetus inside her. They believe that it is her parasitic twin. She is now waiting operation to have the tiny baby removed.

[]

Thursday, October 18, 2012

GATING DALADALA IS LIKE GOLDEN CHANCE



Mwanza resident struggling to take Daladala ( public transport service). Currently Mwanza city has large number of people compared to public transport service available. Those are SAUT students taking transport to their home. 

Wednesday, October 17, 2012

MICHUZI: NEWS ALERT: Hali si Shwari maeneo ya Kituo cha Kati cha Polisi Jijini Dar muda huu

MICHUZI: NEWS ALERT: Hali si Shwari maeneo ya Kituo cha Kati cha Polisi Jijini Dar muda huu
Jeshi la polisi jijini Dar limelazimika kutumia mabom ya machozi kuwatawanya baadhi ya waislam waliokusanyika katika kituo cha kati jijini Dar wakishinikiza kuachiwa kwa katibu wa jumuia na taasisi za kiislam Tanzania Sh. Issa Ponda
Watu 38 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya srikali na uchochezi kati ya waislam na wakiristo ikiwemo vurugu za hivi karibuni za Mbagala

MICHUZI: Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda ashikiliwa na polisi

MICHUZI: Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda ashikiliwa na jeshi la polisi jijini Dar
Sh. Ponda anashikiliwa kwa tuhuma mbalimbali zinazmkabili. Kamanda wa polisi kanda maalum, Suleiman Kova amesema Sh. Ponda amekamatwa kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali iliyopo madarakani, uchochezi wa udini kati ya waislam na wakristo na ndani ya waislam wenyewe, kuwachochea watu kufanya maandamano, vitisho vya kumuua Muft wa Tz Sh Issa bin Simba, kuingilia uhuru wa mahakama pamoja na uchomaji wa makanisa,
Sh. Ponda alikamatwa juzi usiku majira ya saa nne usiku akiwa kwenye pikipiki akielekea temeke jijini Dar.

Monday, October 15, 2012

TANGANYIKA ONE: HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF)

TANGANYIKA ONE: HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF)

HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF)

  HABARI NJEMA: 
Taasis mpya ya binafsi inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imeanzishwa. kwa  wale ambao ndugu zao wamekosa mikopo kupitia taasisi ya serikali ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu HESLB wanaweza kuwashauri waombe huko. taasisi hiyo inaitwa HLSSF ( Higher Learning Students Supporting Fund) kwa maelezo zaodi tembelea tovuti hii hapa http://www.hlssf.org/

Sunday, October 14, 2012

HAYA NDO MAISHA YETU


Nci yetu imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi lakini maisha wa waTZ wengi bado ni duni mno. Haya ni baadhi ya makazai watu wa mtaa wa Luchelele jijini Mwanza

TUVITUNZE VIVUTIO VYA UTALII TULIVYONAVYO

Kaburi ambalo baadhi ya mabaki ya mpelezi na mmisheni wa mwanzo DR. LIVINGSTONE yamehifadhiwa. Kburi hili linapatikana katika makumbusho ya DR. LIVINGSTONE MEMORIAL yapatikanayo Ujiji Kigoma

Saturday, October 13, 2012

Mass Communication Society Members
TAFAKARI YANGU
A. asalam Alykum.Qur'an ni kiyabu cha ALLAH kisicho na shaka ndani yake ingawa baadhi ya watu wenye nongwa na inda wamekuwa wakifanya vitimbi vingi kwa lengo la kuidhalilisha.Tukio la Mbagala la jana tareh 11/10/2012 ni moja ya matokeo ya udhalilishaji wa Qur'an.imekuwa ikichomwa moto,kuitwa kuwa ni ndoto na mashairi ya mtu aliyepegawa,  ni kitabu cha majini, nk. Baadhi ya matukio yalifikishwa kwenye vyombo vya sheria na hakuna hatua za dhati kudhibiti kujirudia kwa vitendo hivyo. Baadhi ya waislam wamekuwa wakichukua hatua za kuonyesha kukasirishwa na vitendo hivyo kwa kufanya maandamano ambapo mengine huambatana na uharibifu wa mali za watu mbalimbali. ninapotafakari haya na vitendo vingine vinavyoudhalilisha uislam napata maswali ya kujiuliza
      1. Ni kwanini vitendo hivi vinaendelea na wanaofanya wanaagizwa na nani?
      2. je uharibifu wa mali unaotokea hauwapi funzo watekelezaji kuacha vitendo hivi
      3. Watekelezaji wa vitendo hivi wamakuwa wakiishi maisha ya hofu na kujificha wakihofia kuuawa, je hii haiwapi funzo watu wengine kuacha kutekeleza vitendo hivi?
      4.Sisi waislam baada ya kutokea matukio haya tumekuwa tukifikisha kiliocheztu kwa serikali, kufanya maandamano, kuwatishia maisha watekelezaji wa vitendo hivi viovu lakini bado mafanikio hayajapatikana, matukio haya bado yamekuwa yakiendelea.
   Uchomaji wa Qur'ani umekuwa ukiendelea. kati ya mwaka 2011 na 2012 si chini ya matukio ya uchomaji wa Qur'an yametokea mkoani Mwanza, tukio la Mbagala la kukojolea kitabu ktukufu cha Qur'an na matukio mengine ya kiovu dhidi ya mtume wetu MUHAMMAD (s.a.w)
    Wakati haya yakiendelea kujitokeza na waislam waikichukua hatua tofauti tofauti ambazo bado hazijazaa matunda, nashawishika kujiuliza maswali mengine kadhaa.
1. Hatua tunazozichukua kukabiliana na vitendo hivi ni sahihi?
2. kama ni sahihi mapungufu yako wapi mpaka hatufanikiwi kufikia lengo?
3.Matukio haya yalijtokea wakati wa Manabii/mitume ni njia zipi walizitumia kukabiliana nayo?
4. Naamini Qur'an inajibu la utatuzi wa matatizo haya. Je? Qur'an inatuambia nini tufanye ili kukabiliana na uchafu huu?
5. Mtume MUHAMMAD (s.a.w) alipokabiliwa na matatizo kama haya alitumia njia zipi kukabiliana nayo?
6. Sisi waislam wa sasa njia alizozitumia Mtumwe na kama Qur'ani inavyose tunazifuata? na kama tunazifuata kwa nini hatufanikiwi kutokomeza vitendo vya udhalilishaji wa Qur'an, Mtume na Uislam kwa ujumla?