Saturday, December 21, 2013

SHERIA YA KUWAWAJIBISHA WABUNGE WANAOKWENDA MSOBEMSOBE INAHITAJIKA.

Na. Butije Hamisi

Watu wa kigoma wamekuwa na msemo unaoseama "Kigoma ya sasa sio ile ya zamani, Buzebazeba ya sasa sio ile ya zamani" Hivyo nami nashawishika kusema Tanzania ya sasa sio ile ya zamani.
 
Ni wazi kuwa kwa sasa watu wengi wameamka, wameelimika, wanatambua kila kinanchoendela na wanafuatilia kila hatua inayopipgwa na serikali.
 
Nayasema haya kwa kushangazwa na kauli iliyotolewa bungeni na Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Anne makinda pale aliposema “Waheshimiwa wabunge nimesema kama mlichukua pesa bila safari, mnarudisha si basi…. Wote kabisa ninawajua na ninalifanyia kazi. Wote waliochukua pesa warudishe ndiyo utaratibu wa Serikali na ndivyo inavyotakiwa. Wote watarudisha.” Alisema Anne Makinda.
 
Siamini huenda ipo siku nitaamini. Hivi ukichukua fedha za umaa kwa kazi maalum ya kiserikali ukaenda kufanyia mabo yako binafsi adhabu yake ni kuzirusha tu?
Je huu ni wizi, utapeli ukwapuaji, unyanganyi au nini nini? Hivi hakuna sharia inayoainisha kupelekwa mahakamani mtu aliyechukua fedha kama walivyofanya baadhi ya wabunge?
Chakunishangaza zaidi mbunge anajitetea kwa kujiamini kuwa haikuwa vibaya yeye kuahirisha ziara ya kimafunzo huku akiwa ameshatia mshiko kibindoni.

“Ningekuwa kiongozi wa ajabu sana kama ningekwenda Dubai na Uingereza na kutokwenda ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutoka chama kinachotawala.” alisema Mh. Erasto Zambi ambae ni Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Erasto Zambi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya.
Tumezoea kuona baadhi ya watumishi wa ngazi za chini serikalini (Mfano Walimu Wakuu) wakifikishwa mahakani kwa kufuja fedha za serikali katika ujenzi wa madarasa na ununuzi wa vitu vingine. Je mwalimu aliyepelekwa mahakamani kwa kufuja shilling milioni moja anatofauti gani na mbunge aliyefuja shilingi milioni 5 na kuendelea mpaka mwalimu apelekwe mahakani mbunge yeye aambiwe kuzirejesha bila kufikishwa mahakamani?

Mama yangu Anne Makinda ni wazi kuwa Wabunge wengi (toka ktk vyama vyote humo bungeni) kwa sasa wamepoteza imani kwa wapiga kura wao. wamekuwa wakikabiliwa na kashfa nyingi zinazolidhalilisha bunge, wabunge, wananchi na nchi kwa ujumla.
Unaonaje wewe (Anne Makinda) pamoja na wabunge unaowaongoza mkatunga sharia ya wananchi kuwawajibisha pindi wanapoona mnaenda msobemsobe.

Kwa sasa baadhi ya wabunge tena wengi bila kujali ni wa CCM, CDM au vyama vingine wamekuwa hawawajibiki kwa wananchi waliowachagua bali wamakuwa wakiwajibika kwenye maslahi yao. wakiamini kuwa hakuna mwananchi aneweza kuwawajibisha.

Achilia mbali sakata hili la kuchukua posho za safari/ziara za mafunzo bila kusafiri ni wabunge haohao ndio waliopitisha kodi ya laini ya simu bila kuangalia hali ya maisha ya wananchi, TNinamshukuru Raisi Kikwete kwa kuikataa, Ni wabunge hawa hawa ndio wanaopitisha bajeti ya serikali ambayo kiasi kukubwa huelekezwa kwenye matumizi ya kawaida badala ya kwenye miradi ya maendeleo.

Ni wabunge hawahawa wanaojipitishia posho na mishahara yao mikubwa huku mwalimu aliyemfundisha kusoma na kuandika akiendelea kwenya shule kwa mguu kwa kwa kukosa nauuli ya daladala huku akihangaika kutafuta malaki kama si  mamilioni ya kumlipia mwanae aweze kwenda sekondari au chuo akasome.
Ni wazi kuwa wabunge wengi wamekuwa wakiangalia manufaa yao bila kujali wananchi wanaohangaika kwa kukosa maji, umeme, chakula, huduma bora za afya ba huduma zingine muhimu.

Kulikuwa kunahaja gani ya baadhi ya wabunge kuwapa hizo fedha za kutalii badala ya kuzipeleka kijiji cha BUKOMELA wilayani Ushetu Mkoani Shinga ambako wanafunzi wa shule ya msingi Bukomela wanaancha kuingia darasani kwa kwenda porini kuwachotea maji walimu zao? Hivi wangechimba kisima kimoja cha maji hapo shuleni si kingepunguza adha kwa wanafunzi wao na kushiriki ipasavyo masomo yao na kwa wakati sahihi?

Kumekuwa na uhapa wa wataalamu na wenye ujuzi wa kutosha katika sekta mbalimbali hapa nchini, Je kulikuwa kuna haja gani ya kuwapeleka wabunge kwenye mafunzo nje ya nchi badala ya kuwapeleka wataalam kuongeza ujuzi kwani wao ndio watendaji wa shughuli za serikali na si wabunge.
kwa maajabu haya yanayoendelea nchini kwetu inanipa hamasa kurudia tena kale ka msemo kwa watu wa kigoma wanakosema "Kigoma ya sasa sio ile ya zamani, Buzebazeba ya sasa sio ile ya zamani" Hivyo nadiriki tena kusema Tanzania ya sasa sio ile ya zamani. Kwa sasa watu wengi wameamka, wameelimika wanatambua kila kinanchoendela na wanafuatilia kila hatua inayopipgwa na serikali.

Kwa sasa watanzania tunatambua mazuri na usanii unaofanywa na baadhi ya viongozi walioko madarakani pamoja na wabunge ambao wengi wao wamesahau majukumu yao ya kuwawakilisha wananchi badala yake wanawakililisha maslahi yao.

Napenda kuwakumbusha wabunge na viongozi mlioko serikalini, nii nchi ni yetu sote, na kila hatua ya maendeleo tungependa tusonge sote, maendeleo mazuri ya nchi ni yale yanayowanufaisha wananchi wote na si tabaka Fulani la wananchi pekee.
.......................
Kwa maoni:- 0752231172

No comments:

Post a Comment