Tuesday, October 23, 2012

POLISI WAWILI WATELEKEZA LINDO NA KUFANYA KAZI YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Askari Polisi  wawili wametelekeza lindo lao na kuingia barabarani kukamata dalala iliyokuwa imepeba abiria kutoka malimbe kuelekea katikati ya jiji la Mwanza.
Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa mbili usiku eneo la ATM katika chuo cha SAUT ambapo askari hao waliokuwa lindo katka bank iliyopo eneo hilo waliacha kazi yao na kwenda kukamata daladala yenye namba za usajili T 130 BUK inayofanya safari za Buhongwa Kishiri.

Askari hao walidai kuwa daladala hiyo imebadilisha ruti kitendo ambacho ni kinyume na sheria.  Tuakio hilo lilizusha mabishano kati ya askari hao na derevairia wa gari hilo huku askari hao wakiwaamuru abiria zaidi ya 15 waliokuwa ndani ya gari hilo washuke na kusubiri gari jingine.
"Abiria wote shukeni na doreva weka gari pembeni na uizime" alisikika mmoja wa askari hao akitoa amri hiyo ambayo dereva wa gari hilo hakuitekeleza akidai kuwa gari hiyo ikizimwa haitowaka tena.

Kushindwa kutekelezwa kwa amri hiyo ilipelekea askari mmoja kuchukua funguo za gari hiyo hali iliyopelekea kuzima kwa gari hiyo na kushindwa kuwaka tena.

Baadhi ya abiria waliokuwemo ktk daladala hiyo walilalamikia kitendo hicho huku wakishangazwa na kitendo cha polisi hao kuacha kazi yao ya kulinda bank na kwenda kukamata magari kazi ambayo inatakiwa ifanywe na askari wa usalama barabarani. Mpaka mwandishi wa habari hizi anatoka eneo hiko majira ya saa saa tatu kamili daladala hiyo ilikuwa bado imeshikiliwa na askari hao huku wakimuamuru dereva aliwashe gari hilo na kuliondoa barabarani na dereva akidai kuwa gari hiyo haiwezi kuwaka.

No comments:

Post a Comment