Saturday, October 13, 2012

TAFAKARI YANGU
A. asalam Alykum.Qur'an ni kiyabu cha ALLAH kisicho na shaka ndani yake ingawa baadhi ya watu wenye nongwa na inda wamekuwa wakifanya vitimbi vingi kwa lengo la kuidhalilisha.Tukio la Mbagala la jana tareh 11/10/2012 ni moja ya matokeo ya udhalilishaji wa Qur'an.imekuwa ikichomwa moto,kuitwa kuwa ni ndoto na mashairi ya mtu aliyepegawa,  ni kitabu cha majini, nk. Baadhi ya matukio yalifikishwa kwenye vyombo vya sheria na hakuna hatua za dhati kudhibiti kujirudia kwa vitendo hivyo. Baadhi ya waislam wamekuwa wakichukua hatua za kuonyesha kukasirishwa na vitendo hivyo kwa kufanya maandamano ambapo mengine huambatana na uharibifu wa mali za watu mbalimbali. ninapotafakari haya na vitendo vingine vinavyoudhalilisha uislam napata maswali ya kujiuliza
      1. Ni kwanini vitendo hivi vinaendelea na wanaofanya wanaagizwa na nani?
      2. je uharibifu wa mali unaotokea hauwapi funzo watekelezaji kuacha vitendo hivi
      3. Watekelezaji wa vitendo hivi wamakuwa wakiishi maisha ya hofu na kujificha wakihofia kuuawa, je hii haiwapi funzo watu wengine kuacha kutekeleza vitendo hivi?
      4.Sisi waislam baada ya kutokea matukio haya tumekuwa tukifikisha kiliocheztu kwa serikali, kufanya maandamano, kuwatishia maisha watekelezaji wa vitendo hivi viovu lakini bado mafanikio hayajapatikana, matukio haya bado yamekuwa yakiendelea.
   Uchomaji wa Qur'ani umekuwa ukiendelea. kati ya mwaka 2011 na 2012 si chini ya matukio ya uchomaji wa Qur'an yametokea mkoani Mwanza, tukio la Mbagala la kukojolea kitabu ktukufu cha Qur'an na matukio mengine ya kiovu dhidi ya mtume wetu MUHAMMAD (s.a.w)
    Wakati haya yakiendelea kujitokeza na waislam waikichukua hatua tofauti tofauti ambazo bado hazijazaa matunda, nashawishika kujiuliza maswali mengine kadhaa.
1. Hatua tunazozichukua kukabiliana na vitendo hivi ni sahihi?
2. kama ni sahihi mapungufu yako wapi mpaka hatufanikiwi kufikia lengo?
3.Matukio haya yalijtokea wakati wa Manabii/mitume ni njia zipi walizitumia kukabiliana nayo?
4. Naamini Qur'an inajibu la utatuzi wa matatizo haya. Je? Qur'an inatuambia nini tufanye ili kukabiliana na uchafu huu?
5. Mtume MUHAMMAD (s.a.w) alipokabiliwa na matatizo kama haya alitumia njia zipi kukabiliana nayo?
6. Sisi waislam wa sasa njia alizozitumia Mtumwe na kama Qur'ani inavyose tunazifuata? na kama tunazifuata kwa nini hatufanikiwi kutokomeza vitendo vya udhalilishaji wa Qur'an, Mtume na Uislam kwa ujumla?

No comments:

Post a Comment