Wednesday, January 30, 2013

LULU HUYOO!! ATINGA URAIANI



Lulu na mama yake wakimwaga machozi baada ya kukutana nje ya Mahakama Kuu
 Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) ameonana na Msajili wa Mahakama Kuu Amir Msumi na kusaini hati ya dhama kisha kuondoka na mama yake mzazi kurejea nyumbani.
Msanii huyo alishindwa kuzuia furaha yake na kumwaga machozi baada ya kukumbatiana na mama yake mzazi huku baadhi ya watu waliofika Mahakamani hapo pia wakifurahia kuachiliwa kwake kwa kumwaga machozi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mahakamani hapo Lulu alisema kwamba anamshukuru Mungu kmpatia nafasi ya kurudi nyumbani na kuungana na familia yake.
"Kwakeli sina chakusema kwa leo zaidi ya kumshukuru Mungu kwani bila yeye nisingepata hii dhamana ya kurudi nyumbani na kuonana na mama yangu"alisema Lulu.
Akisoma uamuzi wa maombi ya dhama ya msanii huyo Jaji Mruke alisema, "Mahakama imekubali maombi yako ya dhamana na uko huru kwa masharti yafuatayo, (moja) unatakiwa kuwasilisha gharama zote za safari ndani ya jiji la Dar es Salaam".


"(Pili) usisafiri nje ya Dar es Salaam bila idhini ya Msajili wa Mahakama Kuu, (tatu) unatakiwa kuripoti (kujiwakilisha) kwa Msajili wa Mahakama kila tarehe mosi ya kila mwenzi".
Akisoma uamuzi wa maombi hayo Jaji Mruke alifafanua kuwa, "Sharti la (nne) unatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini na wawe na tsh 20milioni kila mmoja".
"(Tano) ni kwamba unatakiwa kutimiza masharti ya dhamana na kusaini mbele ya msajili wa Mahakama na utaendelea kubaki rumande mpaka utakapotimiza masharti yote"


Monday, January 28, 2013

UCHAWI WACHANGIA KUENDELEZA UBADHILIFU WA MAPATO TRL KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma

Shirika la Reli Tanzania Kituo cha Kigoma,imeshindwa kudhibiti mtandao wa kuhujumu mapato yake kwa kuogopa mtandao wa uchawi.
Kauli hiyo imejitokeza Kigoma ambapo Naibu waziri wa uchukuzi Mh,Charles Tizeba alipolitembelea shirika hilo kukagua utaratibu wa uongozi huo kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo ambao ulikuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo viongozi kutumiwa na mtandao huo wa uchawi ambao huwaroga baadhi ya viongozi wao .
Fanuel Rugonzibwa ambaye ni Mkuu wa Kituo hicho alisema ,mtandao huo unachangiwa na viongozi walioko juu kuwapa jeuri ya kufanya jambo lolote bila kufuata sheria na taratibu za kazi kuwategemea waganga wao,kwa watakaokiuka matakwa yao.
Alidai,kutokana na hali tete ya kukithiri mtandao huo ambao hudiriki hata kuvujisha siri ya vikao vya utawala na kwa viongozi ambao wanamsimamo wa kutetea haki na stahiki za abiria ambao wanateseka na kudhulumiwa haki za msingi ikiwemo kuuziwa tiketi juu zaidi ya kiwango cha serikali cha sh.19.100.
Akichangia katika hilo Askari Polisi wa Reli mkoani hapa Koplo.Michael amedadavua kuwa,mtandao huo unaongozwa na vijana wawili Said Ngururka na Majaliwa Zuberi wamekuwa wakifanya hujuma hizo za kuuza tiketi zaidi ya bei husika na kuvujisha siri za kituo hicho na kutoa taarifa za uongo kwa uongozi wa juu ambapo huwachukulia sheria wafanyakazi wake bila kufanya uchunguzi wa kina.
Akijibu tuhuma hizo Mh,Dkt Tizeba amemtaka mkuu wa kitengo cha polisi cha reli kuwa,atakapopata taarifa ya wababe hao kuzengea maeneo ya kituo hicho siku za kusafirisha abiria watiwe nguvuni ili wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa mahakaman sanjari na sheria kuchukua mkondo wake, ili iwe fundisho kwa wale wote wanahujumu shirika hilo.
" mtandao wa kichawi utafanyiwa kazi,pia wafanyakazi wa reli muone uchungu na shirika hili,acheni udokozi wa fedha za abiria wasio na tiketi na kugawana fedha za mizigo ambayo haikubainishwa katika kitabu cha risiti "alisema Tizeba.
Naye mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani Maneno amewashauri watendaji wa shirika hilo wajitume kwa dhati ili kuwaunga mkono waziri wa uchukuzi Mh,Harrison Mwakyembe na Naibu wake Dkt.Tizeba ikiwa na tija ya kuwarudishia imani wananchi wake ,kwa kuwaondolea adha ya urasimu wa upataji wa tiketi na gharama za usumbufu wa ughahirishaji wa safari hasa waishio mbali na manispaa ya Kigoma Ujiji. 

Sunday, January 27, 2013

ZITO: SERIKALI IMECHANGIA MAUAJI MTWARA


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe  ameishutumu serikali kuwa ndio chanzo cha mauaji ya Mtwara kwani imeshindwa kusimamia amni mkoani humo
Akizungumza na waandishi wa habari zito amesema mauaji hayo yametokea kwa sababu serikali imeshidwa kusimamia na kutekeleza utawala bora.
"Hali inayoendelea huko Mtwara ni hali ya kusikitisha,vurugu,mauaji na kuharibu mali kamwe siyo utanzania"amesema Zitto.
Zitto amefafanuwa kuwa, Hatuwezi kuendelea kurushiana lawama ilhali nchi yetu inaungua,serikali na wanasiasa wote tuhakikishe kuwa tunatimiza wajibu wetu kwa kusikiliza wananchi na kufanyia kazi matakwa yao.
Kufuatia vurugu za jana watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku mali mali za serikali na za baadhi ya viongozi zikiharibiwa na wananchi. miongoni mwa waliojeruhiwa ni dereva mmoja wa bodaboda aliyepigwa na polisi hadi kuzirai kwa tuhuma za kuhusika katika uchomaji wa jengo la mahakama ya mwanzo na mwandishi wa habari wa Chanel Ten aliyepigwa jiwe kisogoni.
Mbali na uteketezaji wa malimza serikali nyumba ya Mh. Hawa Gasia ikivunjwa vioo na kuchomwa motto wakati ile ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa vioo
.vurugu hizo zinahusisha na sakata la GESI kwani Hawa Gasia na Sinani wamekuwa kwa Muda Mrefu wakishutumiwa kwa kuchochea na kuridhia usafirishaji wa gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam
 

Saturday, January 26, 2013

Clashes erupt after Egypt court sentences 21 to death in football riot


Egyptian protesters take part in a demonstration near the prison in city of Port Said on January 25.

 An Egyptian judge sentenced 21 people to death Saturday for their roles in a football game riot last year, a ruling that sparked deadly clashes between security forces and relatives of the convicted.
The Port Said football incident left 74 people dead and 1,000 others injured.
Soon after the sentencing in the nation's worst stadium disaster, protests erupted outside the prison in the northeastern port city. Clashes outside Port Said prison left at least 16 people dead and dozens injured, a hospital official told state TV.
The armed forces sent troops to secure public buildings and restore calm in Port Said, according to state media.
The fatal clashes started after some relatives attempted to storm the building to free their loved ones, Brig. Gen. Osama Ismail, a spokesman for the Interior Ministry, told state-run Nile TV.
Crowds outside the prison fired guns and hurled rocks at the security forces, who in turn used tear gas to disperse the crowd, Ismail said.
"There is a state of anger on the streets of Port Said, and the security forces are on high alert," Nile TV reported.
The sentences were handed down in a packed courtroom in Cairo as victims' relatives and those convicted wept.

In the hours after the riot in Port Said, protesters in Cairo chanted, "Down with military rule." At the time, the secretary-general of the Muslim Brotherhood party blamed Egypt's military for the deaths.
Egypt's interior ministry blamed fans for provoking police. Witnesses said police did little to try to quell the clashes.

SOURCE: CNN

Friday, January 25, 2013

MWENDELEZO WA TAARIFA:WANANCHI WA KIBITI WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI POLISI


VURUGU kubwa zilizowalazimisha Polisi kutumia helikopta kuzituliza, zilitokea jana baada ya baadhi ya wakazi wa Kata ya Kibiti kuvamia kituo kidogo cha jeshi hilo wakitaka kukichoma moto katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutaka kulipiza kisasi cha mwenzao kukamatwa na polisi na kisha kupigwa hadi kufariki dunia juzi.

Katika vurugu hizo, wakazi hao wengi wao wakiwa ni vijana, walifunga Barabara ya Kilwa kwa zaidi ya saa tatu hivyo kukwamisha usafiri wa kwenda na kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi.

Vurugu hizo hazikuishia hapo kwani vijana hao walivamia nyumba za askari wa kituo hicho na kisha kutoa vyombo na kuviharibu. Katika tukio hilo, nyumba moja ilichomwa moto.

Hali ilivyokuwa
Kamanda wa Operesheni Maalumu ya Jeshi la Polisi nchini, Saimon Sirro alisema katika tukio hilo, nyumba hiyo ya jeshi imeteketezwa kabisa kwa moto na vyumba vinne vya nyumba nyingine walizopanga askari wengine jirani vimevunjwa... “Vijana hao walikuwa wakiingia na kutoa vyombo na nguo za askari waliopanga humo na kuzichoma moto.”

Kamanda Sirro alisema vurugu hizo zilitokea baada ya kupatikana kwa taarifa za kifo cha Hamis Athumani (30), mkazi wa Kibiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amepelekwa kutibiwa majeraha ambayo kamanda huyo alisema marehemu alidai kuyapata baada ya kupigwa na askari waliomkamata alipojaribu kuwatoroka walipomkamata kwa tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya.

Alisema kukamatwa kwake kulitokana na operesheni ya msako wa bangi na dawa za kulevya.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema baada ya kipigo hicho, kijana huyo alilalamika maumivu na hivyo ndugu zake walifika kituoni hapo na kumpeleka Kituo cha Afya Mchukwi.

“Hali yake iliendelea kuwa mbaya na akapelekwa Muhimbili ambako alifariki dunia jana alfajiri,” alisema shuhuda huyo na kuengeza: “Taarifa hizo zilipofika kijijini, baadhi ya vijana walikusanyika na kuanza kuhamasishana na kuanza kuziba barabara kwa matairi na kuvamia nyumba za askari na kuchoma moto.”

Baada ya ghasia hizo kupamba moto, jeshi liliamua kutumia helikopta ambayo ilitua Kibiti saa 5.50 asubuhi ikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Mathei.
Kamanda Sirro alisema watu 18 wamekamatwa kwa kuhusika na vurugu hizo.

Chanzo cha vurugu
Inadaiwa kuwa Jumanne saa tatu usiku, askari wa Kituo cha Polisi Kibiti walivamia kambi ya vijana wanaodaiwa kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya inayojulikana kwa jina la Kosovo iliyopo Mbebetini karibu kabisa na Sekondari ya Kibiti.

Askari hao ambao baadhi ya wakazi wa Kibiti wamewaeleza kuwa ni mashujaa kwa hatua yao ya kuthubutu kuvamia kambi hiyo ambayo inadaiwa kushindikana kwa muda mrefu kushughulikiwa na askari wa Kituo cha Polisi Kibiti, walikumbana na upinzani mkali wa vijana wapatao 30 wakipinga kukamatwa kwa kiongozi wao.

Inadaiwa kuwa baada ya kumkamata, walimshambulia kwa virungu lakini kutokana na upinzani mkali waliopata kutoka katika kundi hilo, walishindwa kuondoka naye lakini walimwacha akiwa mahututi.

Habari hizo zilieleza kuwa vijana hao walimchukua kiongozi wao na kumpeleka Mchukwi kwa matibabu kabla ya kumsafirisha kwenda Muhimbili ambako alifariki dunia.

Baada ya kupatikana kwa taarifa za msiba huo, baadhi ya wananchi wa Kibiti waliandamana saa 1.22 asubuhi hadi kituo cha Polisi ambako waliharibu pikipiki tatu za polisi. Walitawanywa baadaye kwa baruti na silaha za moto.
Baadaye, polisi kutoka Ikwiriri walifika na kudhibiti kundi kubwa la watu hao wapatao 120 kwa mabomu ya machozi.

Askari afariki
Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU) H21 PC Domick, amefariki dunia na wenzake wanne kujeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kibaha Pwani kuelekea Rufiji kutuliza vurugu hizo kupinduka katika eneo la Mkuranga.

CHANZO: MWANANCHI

WASIRA: UCHIJAJI WA NYAMA YA BIASHARA UTAFUATA MFUMO AMBAO HAUTALETA MTAFARUKU KATIKA MADHEHEBU YOTE YA DINI

Hatiame mkutano wa usuluhishi na wa amani kati ya makundi mbalimbali aya kidini juu ya ikhtilafu za uchinjaji umemalizika kwa waumini wa madhehebu ya kikristo kuruhusiwa kuchinja katika hafla za kibinafsi na yule anataka kuchinja kwa ajili ya biashara achinje katika mfumo ambao hautaleta tafrani baina ya waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali.

Katiaka tamko la maafikiano lililotolewa na waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu Mh. Stevine Wasira amesema machinjio ya serikali yataendelea kusimamiwa katika utaratibu uliokuwepo toka awali na wakristo wanaruhusiwa kuchinja vichinjwa binafsi na si vya biashara.

Waziri Wasira amesema maafikiano hayo yamefikiwa kwa lengo la kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa watanzania.

Wakiongea na waandishi wa habari baada kikao hicho baadhi wa viongozi wa madhehebu ya kikristo hawakukubaliana na maafikiano hayo na kudai kuwa uamuzi uliofikiwa ulikuwa wa kisiasa zaidi na kukishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali kuwapendelea waislam.

Viongozi wa Madhehebu ya kikristo wamedai kuwa suala la kuchinja ni ibada kwa waislam na wanapolazimishwa kula nyama inayochinjwa na waislam ni sawa na kuwalazimisha wakristo kufanya ibada ya kiislam mkitu ambacho hawako tayari kukikubali.

Kwa upande wa viongozi wa madhehebu ya kiislam wamekubaliana na maafikiano walioafikiana katika kikao hicho.

Waziri wasira amewataka viongozi wa dini zote kuisaidia serikali katika kuwahimiza watanzania kufuata sheria bila kushurutishwa.

Thursday, January 24, 2013

WANANCHI WA KIBITI WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI POLISI


Wananchi wa Kibiti wilayani Rufiji wakichoma nyumba za askari polisiWanachi wenye hasira kali leo wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilaya ya Rufiji na kufanya vurugu zenye kubwa kiasi cha kutaka kukichoma moto baada ya kugundua kuwa mwenzao amekufa baada ya kupigwa na polisi.

Katiak vurugu hizo wananchi walikuwa na mapanga, marungu na wengine kushika matairi ya magari wakitaka kuchoma kituo hicho.

Inadaiwa kuwa polisi wa kituo hicho walimpiga Hamisi Mponda nakumsababishia majeraha na kuvuja damu nyingi kitendo ambacho kilimfanya alazwe katika hospitali ya Muhimbili na kufariki baadae.

Askari wengi walitanda  katika kituo hicho, wananchi hao wamebadili hicho na kuwafanya wanachi wabadili utaratibu na kuamua kuzichoma nyumba za askari hao zilizopo pembezoni mwa kituo hicho bila kuhofu kitu chochote kinachoweza kuwadhuru.

VYUO VYA UDSM, MKWAWA NA CUJ- DAR VYAONGOZA KWA UKAHABA

UDSM
MKWAWA




WANAFUNZI wa vyuo vikuu, hasa vya Dar es Salaam, Mkwawa Iringa na Chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam, vimeonekana kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofanya biashara ya ngono kuliko vyuo vingine nchini.
Hayo yalibainishwa na Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi wa Manispaa ya Iringa, Gaspar Nsanye, alipozungumza na wadau mbalimbali katika mdahalo wa siku mbili kuhusu mpango mkakati wa AMICAAL kuhusu makundi yaliyosahaulika katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na ukimwi na kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo, madiwani, wakurugenzi na wadau waliopo mkoani hapa.
Alisema matokeo ya zoezi la kupata maoni na hali halisi ya makundi maalumu yalionesha kuwa baadhi ya makundi yapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya mashoga, wanaotumia dawa za kulevya, watoto wa mitaani, wafungwa pamoja na wanaofanya biashara ya ngono.
“Hivi sasa kuna kasi kubwa ya kukua kwa makundi hayo na yanaelekea maeneo mengine hasa mijini na idadi ya watu wanaopata maambukizi mapya katika makundi haya inaongezeka,” alisema Nsanye.
Alisema sababu hasa zilizotajwa za watu kujiingiza katika makundi hatarishi ni pamoja na utamaduni katika baadhi ya maeneo kama Tanga na Zanzibar, umaskini na matatizo hasa kwa wafungwa, uchangiaji wa vifaa kwa wanaojidunga dawa za kulevya na ngono isiyo salama.
Alisema miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Manispaa ya Iringa ni kuongezwa kwa vituo vya huduma ya afya kwa walioathirika na dawa za kulevya na ukimwi na kutoa elimu jinsi ya kufanya ngono salama, kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya kondomu kwa watumishi, wanafunzi, vijana na kusambaza kondomu kwenye baa, kata vyuoni na katika jamii.

CHANZO: T/Daima.

WAZIRI MKUU ATAKA MADARAKA YA RAIS YAPUNGUZWE


Waziri mkuu wa jamuhui ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ametaka Katiba Mpya impunguzie Rais madaraka hasa katika nafasi ya uteuzi.
Pinda ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyoko katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya watanzania juu ya katiba mpya.

Kauli hiyo ya Pinda inapingana na ile iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuhusu Katiba Mpya ambaye aliiambia Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba madaraka ya Rais yasiguswe akisema kama atanyang’anywa, atashindwa kuongoza nchi.
Balozi Sefue alisema nafasi ya Rais inapaswa kuwa imara na yenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania wote.

Pinda amebainisha kuwa kuna haja ya kumpunguzia Rais madaraka kwani amekuwa na mzigo mkubwa wa kuongoza Serikali, "kitu kikubwa ambacho ningependa kiangaliwe kwenye Katiba Mpya kwa upande wa madaraka ya Rais ni katika uteuzi wa viongozi mbalimbali.”

"Nimetaka Katiba Mpya impunguzie mzigo Rais kwani amekuwa na kazi nyingi sasa ni vyema angepunguziwa mzigo huo hasa katika masuala ya uteuzi wa viongozi.”
Pinda alitoa mfano kwamba katika kazi ya uteuzi wa viongozi, Makamu wa Rais anaweza kumsaidia kazi hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine ambavyo Katiba itaviainisha.

Wednesday, January 23, 2013

WANAFUNZI WA AMITIER SEC. WANATUHUMIWA KWA MAUAJI


 
,Na Magreth Magosso,Kigoma,
 
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya `AMITIER’ iliyopo katika kambi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma,wanasadikiwa kufanya mauwaji ya Tona Kabwe(63) kwa kumtuhumu kuwa ni mchawi. na walimu wao wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani hapo.
 
Taarifa hiyo imetolewa na ACP Frasser Kashai alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwakwe Kigoma Ujiji jana, alisema 22,Januari,2013 saa 4.20 kwenye kambi ya wakimbizi ya nyarugusu wanafunzi hao wakiwa pamoja na walimu wao,walikwenda nyumbani kwa marehemu kwa tija ya kutoa pole baada ya kufiwa na mjukuu wake ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.
 
"inasemekana wanafunzi hao awali mjukuu wa marehemu ambaye naye alifariki baada ya kuugua kwa siku chache hivi karibuni ,inasadikiwa kabla ya kifo chache aliwahadithia baadhi ya wanafunzi wenzie juu ya ndoto yake aliyomuota babu yake akimrisha nyama hali iliyowajengea imani wanafunzi hao kwenda kulipiza kisasi kwa babu huyo kwa kumpiga na fimbo sanjari na kuni hadi umauti ulipomfika" alisema Kashai.
 
Alidai kutokana na tukio hilo Jeshi la polisi linawashikilia walimu wane wa shule hiyo kwa upelelezi ,huku akitoa rai kwa wananchi wapunguze imani za kishirikina.Wakatihuohuo 22,Januari,2013,saa 10 jioni kijiji cha kwaga wilayani kasulu watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni mke na mume Hakani (45) na Prisca William wamekufa baada ya kupigwa na radi wakiwa shambani.
 
Muguzi wa zahanati ya Kwaga Leonard Haiki alipohojiwa na wandishi uwepo wa taarifa hiyo,alikana kufa kwa Prisca huku akidai kufa riki kwa mumewe Hakai, na kubainisha majeruhi watano ambapo watatu wamepelekwa kituo cha afya cha Kasulu. Wakati huohuo kijiji cha Nyarugusu saa 4.00 mtoto Sharifu Rajabu (15) amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba ya chandarua chumbani kwakwe .
 
Kashai alidai chanzo cha kujinyonga kwake ni kitendawili na upelelezi bado unaendelea.

KICHANGA CHATUPWA UWANJA WA MPIRA MALIMBE


Mtu asiyejulikana ametupa kichanga ambacho ambacho kilizaliwa kabla ya muda wake. kichanga hicho ambacho kinakisiwa kimezaliwa kikiwa na kati ya miezi saba na minane kimekutwa kimetupwa katika uwanja wa mpira Malimbe ulioko katika chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) huko Malimbe jijini Mwanza.
Wachezaji wa mpira uwanjani hapo wakiwa katika mazoezi yao ya jioni wamekikuta kichanga hicho kimetelekezwa uwanjani hapo huku kikiwa kimefariki.
Mashuhuda wa tukio hilo wamepeleka lawama zao kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha SAUT kwa kuhusika na tukio hilo.
Mpaka ripota wa habari hizi anaondoka eneo la tukio jeshi la polisi alikuwa wamefika eneo hilo kuchukua mwili wa kichanga hicho na kuanza uchunguzi rasmi wa tukio hilo.

PINDA AZINDUA TAASISI YA WAARABU TANZANIA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikata utepe wakati alipozindua  Taasisi ya Waarabu Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Novemba 18,2012. Kushoto Ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mecky Sadic.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Sheikh Noordin Kishk  baada ya kuzindua Taasisi ya Waarabu Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es alaam Novemba 18,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akizungumza a Shekh  Noordin Kishk (katikati) na Mwenyekiti wa  Taasisi ya Waarabu tanzania , Said Said Mohamed  (kulia) baada ya kuzindua Taasisi hiyo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Novemba 18,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AKALIA KUTI KAVU

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Willson Kabwe
Chama cha Mapinduzi kiko katika mkakati wa kumng'oa madarakani Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe kwa madai kuwa amechangia maendeleo  mabaya ya Chama hicho jijini Mwanza.
Mkurugenzi huyo anatuhumiwa na CCM kuhusika katika utapeli wa Sh1.6 bilioni za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akibainisha suala hilo Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde amesema,  amelifikisha suala hilo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, akidai kuwa tuhuma hizo zilichangia CCM kupoteza ushindi katika uchaguzi mkuu.
Taarifa za ndani ya kutoka CCM zinadai kuwa Mbunge huyo na wenzake pamoja na Makamu Mwenyekiti huyo walikutana katika Hoteli ya New Mwanza na kujadili masuala mbalimbali na kufikia maamuzi kuwa CCM lazima ibadili hali ya siasa katika Jiji hilo huku wakiahapa kwamba ili wafanikwe kisiasa katika eno hilo ni lazima Mkurugenzi huyo afukuzwe kazi.
"Nikweli kwamba hali ya kisiasa jijini Mwanza siyo nzuri na anayesababisha hayo yote ni Mkurugenzi huyo, ingawa sisi nhatuna mamlaka ya kuamua suala lake ndiyo maana tumeamua kufikisha suala lake katika ngazi husika,ila hatukulifisha kama kesi isipokuwa kama taarifa ya kawaida ama mazungumzo"alisema Lusinde.

Tuesday, January 22, 2013

WALIMU WAFUNDWA KUTUMIA UFUNDISHAJI WA MUHAMO WA RUHAZA- KIGOM

Na Magreth Magosso,Kigoma

Walimu wa shule za msingi wanaofundisha katika Manispaa ya Kigoma Ujiji,wanapigwa msasa wa siku saba ili kubaini  stadi za matumizi ya muundo mpya wa ufundishaji wa muhamo wa ruhaza ambao utasaidia kudhibiti tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.

Hayo yamebainishwa juzi na Ofisa Elimu shule za msingi Manispaa ya Kigoma Ujiji ,Shomari Bane ambapo
 imeanza kuendesha semina ya mafunzo hayo, kwa walimu kutoka shule mbalimbali za manispaa hiyo ili   kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wasiojua  kusoma na kuandika.
 
Hata hivyo kwa upande wake  Naibu Mkaguzi wa elimu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, George Ngwila alisema kuwa zipo sababu mbalimbali ambazo zinachangia katika kuwafanya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kufaulu mitihani yao ya mwisho  kutokana na ushirikiano duni baina ya  walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe.
 
Ngwila amedai siku saba za kupewa elimu hiyo itasaidia walimu hao marejeo ya nini wanachopaswa kufanya katika utendaji wao darasani  hasa suala la kuangalia muundo wa kusoma, kuandika na kuhesabu ili  kuondoa tatizo hilo.
 Mwalim Domiciana Peter  ambaye amefundisha shule mbalimbali za msingi katika manispaa hiyo kwa miaka mingi alidai kuwa, kubadilishwa kwa mitaala kumechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wanafunzi wamalize elimu ya msingi wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
 
Amesema kuwa kwa mfumo wa sasa wa mitaala  haina stadi zile za KKK na ufanyaji wa mitihani wa kuchagua unawapa nafasi baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuweza kupenya na hatimaye kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.
 
Ikumbukwe kuwa,zaidi ya wanafunzi47 waliomaliza shule ya msingi katika shule za manispaa hiyo 2012 walikuwa hawajui kusoma,kuandika wala kuhesabu,ingawa jitihada zimeanza walimu kupewa njia yakinifu ili kukabiliana na changamoto hiyo,lidara ya elimu ipeleke walimu wao mafunzoni kila wabadilishapo mitaala.
 

WAZIRI KOMBANI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI JIJINI MWANZA.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Ompeshi Kombani akizungumza mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

POLISI MWANZA WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA MAANDAMANO YA WAENDESHA BODABODA

Jeshi Polisimkoani Mwanza limelazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwadhibiti waendesha pikipiki maarufu (Bodaboda) waliokuwa wakiandamana kama ishara ya kufikisha kilio chao dhidi ya manyanyaso wayapatayo toka kwa askari wa usalama barabarani na kushinikiza kuachiwa kwa wenzao waliokamatwa mapema hii leo.
Waendesha bodaboda hao waliandamana kupinga hatua ya Askari wa Jeshi hilo kuwasaka wenzao na kuwakamata kwa madai kwamba hawana Leseni ya kuendesha bodaboda na ya kufanya biashara ya kubeba abiria.
Akizungmza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Mwanza amesema jeshi la polisi liko katika msako mkali wa kuwakamata waendesha bodaboda ambao wanakiuka sheria za usalama barabarni kama kuendesha pikipiki bila leseni, kufanya biashara ya kubeba abiria bila leseni ya biashara, kubeba abiria zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja (mishikaki)
Kamanda amesema waendesha bodaboda wamekuwa wakikiuka sheria za barabarani pamoja na kuwagonga watembea kwa miguu na kukimbia bila kutoa msaada wowote kwa mwathirika.

Monday, January 21, 2013

MWANAFUNZI WA St. JOHN APETEZA MAISHA BAADA YA KUBAKWA NA WATU WASIOJULIKANA



Mwili wa mwanamke mwanafunzi wa chuo cha St John Dodoma ukiondolewa eneo la tukio mjini DodomaTANGANYIKA ONEimepokea taarifa kutoka Dododma zikieleza kuwa Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha St John Dodoma aliyekuwa anasoma fani ya Unesi amekutwa akiwa amekufa katika eneo la chuo hicho leo asubuhi.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo hilo walishuhudia mwili huo ukiwa kama ulivyozaliwa(hauna nguo) na nguo za mama huyo anayedaiwa kuwa na zaidi ya miaka 40 zikiwa pembeni mwa mwili wake.

Taarifa zimeendelea kusema kuwa baada ya kukagua mwili huo imebainika kuwa mama huyo alibakwa na watu wasiojulikana hadi kufa na kutokana na suala hilo inadaiwa kuwa mkuu wake mmoja umekatwa.
Kitendo cha mguu wa marehemu huyo kukatwa imezua utata zaidi kwani haikujulikana mara moja kama ulikatwa na wanyama wa mwituni watuhumiwa wa mauaji hao

Polisi imeeleza kuwa inafanya uchunguzi mkali ilikuweza kuwabaini watu waliohusika katika sakata hilo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ukuta wajeruhi na kuharibu magari stendi ya Ubungo Dar



Magari yaliyoharibiwa baada ya ukuta kuanguka stendi ya Ubungo jijini Dar es SalaamNa Mwandishi wetu: Dar es Salaam

Mpango wa Ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam leo umesababisha hasara kubwa kufuatia kuanguka kwa ukuta wa ndani kwenye maegesho  ya magari madogo.
Baada ya ukuta huo kuanguka magari pamoja na  baadhi ya watu wameweza kujeruhiwa, hata hivyo jitihada za makusudi za kupunguza uharibifu zinaendelea.
"nipo hapa tokea alfajiri nilikuwa namsindikiza mgeni wadngu, ghafla nikasikia kishindo kikubwa kutahamaki watu wakaanza kukimbilia eneo la tukio nilipofika hapa nikakuta kumbe ukuta huu eneo la maegesho ya magari madogo umebomoka" alisema mmoja wa mashuhuda ambae hakutaka jina lake libainishwe.
Aidha taarifa za awali zimeeleza kuwa huenda kukawa na watu waliokufa kwani baadhi ya watu hupenda kukaa katika eneo hilo wakisubiri kufanyika kwa biashara mbalmbali.Ingawa pia zimeeleza kuwa majeruhi wa tukio hilo wamekimbizwa katika kituo cha afya cha Palestina kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Aidha watu wamehoji kwa nini wahusika wa ujenzi huo waanze kuvunja kuta hizo alfajiri wakati wanajua kuwa kunakuwa na pilikapilika nyingi, pamoja na hayo jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa suala hilo.

OMBI LA DHAMANA YA LULU KUSIKILIZWA IJUMAA HII



Lulu akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Askari Magereza            Dar es Salaam
MAHAKAMA Kuu Dar es Salaam imepanga kusikiliza maombi ya dhamana ya Mwigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu, Ijumaa ya wiki hii.
 Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa msanii mwenzake wa fani hiyo, Steven Kanumba, bila kukusudia.
Uchunguzi uliofanywa na tovuti ya Habarimpya.com na kudhibitishwa na vyanzo vya ndani kutoka Mahakamani hapo zimedai kwamba msanii huyo anaweza kupata dhamana hiyo na kurudi uraiani.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini baada ya upelelezi kukamilika alibadilishiwa mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia, kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakakama Kuu, ambako ndiko
itakakosikilizwa.
Lulu akiwa ndani ya lindi la mawazo juu ya kesi inayomkabiliKwa sasa Lulu yuko mahabusu katika Gereza la Segerea, lakini amewasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu ,kupitia kwa jopo la mawakili wake, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe, akiomba aachiwe huru kwa dhamana wakati akisubiri uamuzi wa kesi yake ya msingi.
Habari zilizopatikana kutoka mahakamani hapo zinasema kuwa tayari maombi hayo ya dhamana yamepangwa
kusikilizwa, Januari 25 , mwaka huu, mbele ya Jaji Zainabu Muruke, wa Mahakama Kuu.
Maombi hayo yamewasilishwa kwa hati ya dharura ili yaweze kusikilizwa mapema kwa sababu kuwa kosa linalomkabili mshtakiwa huyo linadhaminika na pia kwamba mshtakiwa amekaa rumande kwa muda wa miezi saba.
Akizungumza na Habarimpya.com wakili wake, Kibatala amedai katika kiapo chake alichokiwasilisha sambamba na madai hayo kuwa anaiomba mahakama impe dhamana kwa masharti yoyote kwa kuwa yeye kama wakili wake yuko tayari , kutimiza wajibu wake.
"Wajibu wangu ni kuhakikisha kuwa mshtakiwa anatimiza masharti yote ya dhamana na kufika makamani kadri na wakati atakapohitajik"alisema Kibatala. Lulu anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, April 7, 2012, nyumbani kwake (Kanumba), Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

CHANZO: Habarimpya.com

KAFULILA: MASHINE ZA UCHIMBAJI VISIMA ZITAPUNGUZA ADHA YA MAJ



              Na Magreth Magosso : Kigoma
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila amewataka wananchi wa jimbo lake,watarajie ujio wa mitambo na mashine ya kuchimba visima ifikapo April Mwaka huu ili kupunguza adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa miongo 13.
 
Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma ya Wanawake wa kijiji cha Kabuyange kata ya Ilagala Jimbo la Kigoma kusini kumshutumu Mbunge huyo kwa kuwatelekeza na adha ya maji ambayo inawakabili kununua maji hayo, ambapo dumu la lita 20 huuzwa kwa sh.150 zaidi ya miaka 13.
Kafulila aamekiri jimbo lake linakumbwa na kadhia hiyo,ingawa alidai adha ya maji ni katika wilaya sita za mkoa wa kigoma ,ambapo zinazopata huduma hiyo ni 27% tu,huku akibainisha mkakati wa kufanikisha kupunguza adha hiyo April 2013,pindi mitambo na mashine zitakapowasili kutoka kwa wadau wake Nchini China .
 
"kweli wananchi wanateseka hasa kinamama ambao huathirika na zoezi la utafutaji wa maji kwa umbali mrefu huku baadhi ya watoto wa kike wakipata mimba kwa kusubiri foleni ya maji, ya kisima kimoja tu kijijini hapo,nawananchi waliowengi hushindwa kumudu ununuzi wa maji,kutokana na hali ngumu ya kimaisha" alisema Kafulila.
 
Aidha alidai kuwa,ili kumaliza tatizo la maji katika mkoa wa kigoma ni pamoja na kutumia mto malagarasi kwa kutandaza mtandao wa maji,ambao utasaidia kwa asilimia miamoja kigoma kuondokana na kadhia hiyo.
 
Akizungumzia kadhia hiyo Madina Abeid (mwananchi) amesema,wamekuwa wakiitwa kwenye vikao vya kijiji ili kuelezea changamoto zinazowakabili katika kijiji hicho,ikiwemo kero ya maji   na walishachangishwa sh.3,000 lakini haipatiwi ufumbuzi wa aina yeyote na wakijaribu kumhoji mtendaji wa kijiji fedha zilipo adai amepeleka ila hajui hatma yake..
 
"mimi sielewi kabisa hii shida ya maji itaisha lini hapa kabuyange,kisima kipo kimoja kiangazi hii maji ya foleni ,hivyo tunanunua maji ya m to malagalasi serikali nayo kupitia halmashauri wako kimya shida yetu" alisema kwa huzuni Abeid.
 
Hamisa Nungu aliongeza kwa kubainisha kuwa,wananchi walifarijika kumpata kiongozi kijana ambaye atasaidia wazazi wake waondokane na kadhia hiyo ya miaka kenda,lakini huzuni ya kusaka maji kila kukicha katika kijiji cha ilagala imebaki kuwa sugu.
 
Kutokana na mkakati wa Mbunge huyo,wananchi wa kata hiyo wasubiri mkao wa kunufaika na ujio wa mitambo na mashine za uchimbaji wa visima kulingana na maeneo yenye uwepo wa maji ikiwa ni sehemu ya kupunguza kadhia hiyo.
   

Mikakati ya kuweka amani mashariki mwa Kongo

Mikakati ya kuweka amani mashariki mwa KongoWakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika na Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC wamekutana mjini Kampala Uganda na kuweka mikakati ya kijeshi yenye shabaha ya kuwatokomeza wanamgambo  waasi walioko katika eneo  lililogubikwa na machafuko la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Maafisa hao wa kijeshi wamesisitiza juu ya kufanya juhudi za kuleta amani na uthabiti katika eneo hilo baada ya kuonekana dalili za kushindwa juhudi za kimataifa za kuutatua mgogoro huo. Crispus Walter Kiyonga Waziri wa Ulinzi wa Uganda amesema kwenye kikao hicho kwamba kuna ulazima wa kukurubishwa mitazamo kwa lengo la kutatua migogoro iliyoko katika eneo hilo. Wakuu wa nchi za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika wanavituhumu vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Kongo kwa kushindwa kuchukua hatua za kimsingi za kuzuia wimbi kubwa la mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Kongo linaloelekea katika nchi za Uganda na Rwanda.  

Watu 17 wauawa na kujeruhiwa katika vurugu Cairo


Watu 17 wauawa na kujeruhiwa katika vurugu  Cairo

Watu watano wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea kati ya vijana na askari wa usalama mjini Cairo nchini Misri.
Hayo yamethibitishwa na Wizara ya Afya ya Misri ambayo imeongeza kuwa, watu hao waliuawa na kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea katika eneo la Shubra El-Kheima kaskazini mwa mji mkuu huo.
 Ripoti hiyo imesema kuwa, ufyatulianaji risasi ni moja ya sababu za mauaji hayo. Duru za habari zinaarifu kuwa, vurugu hizo zilitokea baada ya mauaji ya kijana mmoja aliyeuawa na askari kwa bahati mbaya wakati akimkimbizwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na ulanguzi wa madawa ya kulevya. Kufuatia hali hiyo kulizuka vurugu zilizodumu kwa masaa kadhaa kati ya familia za marehemu na askari na kuwalazimu askari hao kutumia mtutu wa bunduki kuwatawanya watu hao waliokuwa wanakusudia kuvamia kituo cha polisi katika eneo la tukio. Tukio hilo la mauaji linajiri siku chache tu tangu kufanyika kwa sherehe za mapinduzi yaliyopelekea kung'olewa madarakani utawala wa dikteta Hosni Mubarak anayehudumia kifungo cha maisha katika jela za nchi hiyo.

ATCL imeuawa kwa ufisadi-Mwakyembe

ATCL imeuawa kwa ufisadi-Mwakyembe
 Waziri Mwakembe amebainisha kuwa shirika hilo limefilisiwa na ufisadi na itachukua muda mrefu sana kurejea katika hali yake.

ZITO, SIMBACHAWENE WATOFAUTIAN SAKATA LA GESI MTWARA



Kufuatia sakata la Gesi Mtwara kuwa mgogoro kuhusu gesi unachochewa na wanasiasa kwa lengo la kukwamisha juhudi za Serikali za kumaliza tatizo la mgawo wa umeme,  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema huo ni uzushi. Katika taarifa yake , Zito amesema Serikali haitashinda vita hii kwa kuzusha kwamba wanasiasa wanaopinga wanatumika na kampuni nyingine au kwa mataifa ya magharibi kutaka kuvuruga nchi.
“Serikali ijitazame yenyewe. Bila kufanya hayo tunayo pendekeza, wananchi wataendelea kupigania haki yao...Hii ni vita ya uwajibikaji. Wananchi wanataka kufaidika na rasilimali za nchi yao.
Kwa mujibu wa Zitto, Serikali imekuwa ikitoa majibu ya porojo na kuwatusi watu wa Mtwara, na kama ilivyozoeleka Rais Kikwete na mawaziri wake wamekuwa wakisema suala la Mtwara linatumika na wanasiasa kujitafutia umaarufu.
“Inasikitisha sana kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaambia mabalozi wa nchi za kigeni waliopo hapa nchini kuwa yanayoendelea mkoani Mtwara yanachochewa na wanasiasa tuliosimama na wananchi wanaodai kufaidi utajiri wa nchi yetu. Rais Kikwete na mawaziri wake wameshindwa kabisa kuonyesha uongozi katika suala hili na hatimaye kuhatarisha umoja wa kitaifa.”
Aliongeza kuwa anafahamu kwamba Ubalozi wa China umeandika barua serikalini kuwaondoa raia wa China waliopo Mtwara kwa hofu ya maisha yao. Serikali inaficha ukweli huu kama ilivyoficha ukweli kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alifukuzwa na wananchi alipokwenda huko hivi majuzi. Serikali itaficha ukweli mpaka lini?” alihoji.

SIMBACHAWENE
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesisitiza kuwa mgogoro na vurugu zinazoendelea mkoani Mtwara kuhusu gesi unachangiwa na wanasiasa.
Alisema kuwa watu hao aliodai wanakosa uzalendo na utaifa, wanalenga kuhakikisha tatizo la umeme linaendelea kuwepo nchini hadi uchaguzi mkuu ujao ili wapate ajenda ya kisiasa jukwaani.

Mlemavu anayeteseka baada ya kubakwa

“Bibi mimi huingiliwa na mwanamume  aitwaye Mashoto, ila kaniambia nisimtaje, ikitokea nimemtaja basi atanichinja ndiyo maana nilinyamaza, nikiogopa kuchinjwa,” anaeleza Mwajabu akimnukuu Aisha alipotaka kujua aliyempa ujauzito.


SIKU hizi kuna watu wanasema; “Ni heri ukutane na mnyama mkali kama, simba au chui unaweza kusalimika, kuliko kukutana na binadamu, kwani anaweza kukudhuru.”
Maneno haya yanatokana na unyama wanaofanyiana  wenyewe kwa wenyewe. Kila siku tunasikia unyama unaofanywa na binadamu, leo utasikia baba wa miaka 45 amemnajisi mtoto wa miezi minne, mke amemkata na shoka hawara wa mume wake, majambazi wameua familia nzima na mambo kama hayo.
Hayo yanadhihirishwa na mkasa  wa Aisha (siyo jina lake halisi), aliye na  ulemavu,  ambaye hajiwezi kwa lolote bila msaada wa mtu.
Hata hivyo, pamoja na hali aliyonayo, bila chembe ya huruma, Aisha amekuwa mwathirika wa unyama wa binadamu, baada ya kubakwa.
Binti huyo anaishi katika Kijiji cha Ntisi, Kata ya Bicha, umbali wa kilometa tano kutoka Kondoa Mjini, eneo ambalo hakuna usafiri mwingine unaoweza kukufikisha zaidi ya bodaboda.
Katika kijiji hicho hakuna asiyemfahamu binti huyo kutokana na hali yake na historia ya maisha yake, ambayo inasikitisha kila aliye karibu naye.
Kwa takriban miaka 21, binti huyo ameishi na bibi yake aitwaye Mwajabu Haji, lakini sasa familia hiyo imeongezeka, baada ya Aisha kujifungua mtoto, ambaye ni zao la kubakwa. Mtoto huyo sasa ana umri wa miaka sita.
Ukifika nyumbani kwao utamkuta Aisha amekaa katika kiti chake maalumu cha mbao, alichotengenezewa na bibi yake.
Hana kiungo chochote mwilini mwake kinachoweza kufanya kazi zaidi ya mdomo wake.
Hata hivyo, inzi humwingia mdomoni na kutoka, wakirukaruka katika mwili wake wapendavyo, kwani binti huyo hawezi kuwafukuza kwa kuwa mikono yake haifanyi kazi.
Umbile lake lilivyo
Zaidi ya kuzungumza, Aisha hawezi kufanya shughuli yoyote kutokana na kuwa, mikono na miguu vimejipindapinda. Tumbo lake limesogea upande wa kushoto na kichwa  kulia.
Mara nyingi anapoongea mikono hupata nguvu ya ajabu ambapo huanza kurukaruka huku na kule kwa kuwa hawezi kuizuia, hujigonga na kujiumiza katika sehemu mbalimbali.
Mikono hiyo haina nguvu ya kuweza kubeba kitu chochote  au kufukuza wadudu wanaotambaa katika mwili wake hasa inzi kutokana na vidonda vilivyojaa.
Historia ya maisha yake
Aisha  alizaliwa mwaka 1990 Musoma, mkoani Mara akiwa na ulemavu. Alipofikisha umri wa mwaka mmoja, alipelekwa kwa bibi yake mzaa mama, baada ya baba yake kukataa kuendelea kumlea. “Kwa kweli ninamshukuru Mungu na bibi yangu kwa kiasi kikubwa,  kwa kuwa katika historia yangu, nimekutana na changamoto nyingi, lakini hakunitupa au kuninyanyapaa,” anasema na kuongeza:
“Ninamhurumia bibi kwa kuwa pamoja uzee, lakini hana budi kubeba, jukumu la kututafutia riziki ya kila siku kwa ajili yangu na mtoto wangu.
Natamani ningekuwa na uwezo hata wa kumsaidia kuosha vyombo,” anasema Aisha.
Anasimulia kuwa, kwa mujibu wa bibi yake, mama yake alilazimika kumrudisha kijijini hapo, baada ya baba yake kutaka wamchinje au wamtupe.
Aisha anaeleza kwamba, kwa kuwa mama yake alikuwa akiipenda ndoa yake, hakuwa tayari kumtupa au kumuua badala yake alimpeleka kwa bibi yake, ili kuokoa uhai wake.
“Mama yangu mzazi aliwahi kupigwa na baba,  huku akitishiwa kuachwa endapo atanilea, ndugu zake baba walimshauri anitupe,” anasema Aisha.
Anaongeza kuwa, hajawahi kukutana na baba yake mzazi, lakini anadai kuwa anamfahamu kwa jina la David Chacha akieleza kuwa anafanya kazi ya upishi jeshini huko Monduli.
Mama yake mzazi ambaye pamoja na kumrudisha kwa bibi yake, alikuwa akifika kijijini hapo mara kwa mara kumjulia hali, hata hivyo alifariki mwaka 2011.
Alivyobakwa mpaka kupata ujauzito
Kutokana na umbile lake lilivyo na pilikapilika za bibi wa Aisha katika kutafuta riziki, ilimchukua miezi saba bibi huyo kugundua kuwa mjukuu wake ana ujauzito.
Bibi huyo anasema kuwa aligundua kuwa mjukuu wake ana ujauzito, wakati tayari imeshafikisha miezi saba.

CHANZO: MWANANCHI

Thursday, January 17, 2013

JK amaliza mgogoro Madagascar


RAIS wa Serikali ya Mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina ametangaza kutowania tena katika uchaguzi wa urais wa nchi hiyo unaotarajia kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Uamuzi wa kutogombea tena nafasi hiyo ulitangazwa jana na Rais Jakaya Kikwete mbele ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Benin, Beni Yayi Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mazunguzo baina yao.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ulinzi na Usalama ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)- Troika, awali alikutana na mpinzani mkuu wa Rais Rajoelina ambaye ni Rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana na kumshawishi kukukubali kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2009
Pia Rais huyo alitangaza kukubali kutokugombea tena ili kuleta amani na utulivu. “Nimezungumza na Rais Rajoelina na amekubali kutogombea uchaguzi ujao kama uamuzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni,” alisema.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, Rais Rajoelina ametangaza rasmi uamuzi huo juzi nchini kwake na kwamba sasa uchaguzi huo utakuwa wa kidemokrasia na utasimamiwa na Umoja wa Afrika (AU) ambapo marais wote wanatakiwa kuheshimu makubaliano ya umoja huo. Awali, Rais Kikwete alisema kuwa migogoro mingi ya Afrika inasababishwa na wanasiasa ambao wanatumiwa na nchi zilizoendelea kwa masilahi yao.
CHANZO: MWANANCHI

Monday, January 7, 2013

WATOTO MKOANI KIGOMA WAPATIWA CHANJO YA PCV-13


ZAIDI ya Watoto 97,000  Mkoani Kigoma wamepatiwa chanjo  aina ya (PCV-13) dhidi  ya magonjwa Hatarishi  ya kuhara kukali,enomonia na uti wa mgongo ambao husababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kauli hiyo ilitolewa leo Kwenye kituo cha Afya cha Gungu Kigoma Ujiji ,ikiwa na tija ya kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kutoka  99% kwa  mujibu wa takwimu ya 2004  ya (Tanzania DemographicHealth Survey) ili  ifikapo 2015 iwe 90% ya vifo hivyo visiwepo, hali ambayo iliwashawishi wananchi kuitumia fursa hiyo kikamilifu ambapo watoto 97 ,000, walifanikisha zoezi hilo la chanjo dhidi ya magonjwa korofi ikiwemo kichomi, uti wa mgongo sanjari na kuhara kukali ambapo kunachochea kufariki kwa watoto  hao.
Akizindua chanjo hiyo Mkuu wa Mkoa Kigoma Lt.Issa Machibya alisema lengo la kuzindua utoaji wa chanjo hizo ni pamoja na kupiga hatua za kutokomeza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, kutokana na magonjwa ya kuhara na enomonia hali inayohatarisha kizazi cha leo na cha kesho katika mkoa wa Kigoma na kitaifa.
Machibya amesema anaipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuthibitisha kuwa chanjo aina ya`PNEUMOCOCCAL(PCV13)  kuwa ni salama hukinga nimonia kwa 38% na uti wa mgongo zaidi ya 87% ,alafu jamii hailipii  ni bure , pelekeni watoto waepukane na adha ya magonjwa hatarishi msisikilize wazushi eti msiwapeke hawawatakii mema vijana wetu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Leonard Subi amesema kuwa,2009 chanjo zilikuwa zikitolewa dhidi ya magonjwa nane lakini  leo chanjo hutolewa dhidi ya magonjwa 11  baada ya kuongezeka chanjo mpya 2(PCV-13) ambazo zinakidhi kudhibiti maradhi hatarishi ya kuhala kukali,kichomi na uti wa mgongo
CHANZO: Magreth Magosso,Kigoma

UHABA WA MAJI SAFI WAHATARISHA AFYA ZA WATANZANIA

Uhaba wa maji safi na salama umekuwa ni chanzo cha magonjwa ya kuhara, kichocho na homa ya matumbo kwa watanzania. Ingawa Tanzania imejaaliwa rasilimali nyingi lakini wakazi wake wengi hasa wa vijijini wamekosa huduma ya maji safi na salama kwa kipindi kirefu sasa. Baadhi ya watanzania wamekuwa wakichangia maji na wanyama yanayopatika katika vidimbwi vinavyopatikana maene mbalimbali hapa nchini
Posted by Picasa

Mandhari tulivu ya ziwa Tanganyika

 
Posted by Picasa