Tuesday, March 25, 2014

WATU 176 WAPOTEA BAADA YA MAPOROMOKO MAREKANI


Athari ya maporomoko Marekani

Maafisa wa utawala katika jimbo la Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.

Watu 176 bado hawajapatikana baada ya ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso, Kaskazini mwa Seattle.Hii imefikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo hadi 14.

Waokozi wangali wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura kwa kutumia helikopta na miale ya Laser.
Lakini maafisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata manusura.
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maafisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.

No comments:

Post a Comment