Monday, July 8, 2013

FIGO ZA MANDELA ZAACHA KUFANYA KAZI


IKIWA takribani mwezi mmoja sasa tangu Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, akimbizwe hospitalini akiwa mahututi kutokana na ugonjwa wa mapafu, taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa madaktari bingwa wanaomtibu, wamegundua ugonjwa mwingine mwilini mwake.
Nje ya Hospitali ya Medi Clinic iliyoko Pretoria, ambako waandishi wa habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani wamefurika wakifuatilia mwenendo wa afya ya Mandela, juzi na jana, zilivuja taarifa kuwa Mandela ambaye anaishi kwa msaada wa mashine maalumu inayomwezesha kupumua, madaktari wake wamebaini kuwa figo zake zimeshindwa kufanya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, madaktari bingwa wanaomtibu wameanza kupambana na ugonjwa huo kwa kumuwekea mashine ya kusaidia figo zake kufanya kazi na kwamba wanaangalia uwezekano wa kuzibadilisha bila kusababisha madhara mengine katika mwili wake ambao sasa unalindwa dhidi ya magonjwa nyemelezi.

No comments:

Post a Comment