Thursday, September 12, 2013

TUMSAIDIE MTANZANIA MENZETU KUPATA MATIBABU YA UGONJWA UNAOMSUMBUA


Joseph Ayubu (40) mkazi wa Kijiji cha  Nyenze wilayani Kishapu,  mkoani Shinyanga, kwa miaka mingi amekuwa akihangaika kupata tiba ya tatizo lake bila mafanikio.

Ayubu anateswa na ugonjwa wa kansa, hali yake kwa sasa ni mbaya, anatokwa na usaa mwingi; akiukinga usaha unaotoka shingoni, kikombe hujaa ndani ya dakika moja.

“Nimevumilia mno, kadri siku zinavyokwenda mbele naona kifo kinakuja. Sitaki kuamini kama ulimwengu wote au Watanzania wote wanaweza kuwa na roho ngumu ya kushindwa kuniokoa, naomba msaada niondokane na shida hii,”  anasema Ayubu.

 Anawaomba wasamaria wema wamchangie fedha  ili akatibiwe katika Hospitali ya KCMC iliyoko mkoani Kilimanjaro.
Ayubu anasumbuliwa na tatizo la saratani  ya shingo, hivyo kusababisha shingo yake kuvimba na kumfanya ashindwe kutoa sauti  ipasavyo kwani sehemu kubwa ya koo lake imeziba.

Anaeleza kuwa kutokana na ugonjwa huo, kichwa nacho kinazidi kuvimba na kupata maumivu makali.
Macho nayo yanavimba na kumsababishia ashindwe kuona  mbali. Mbaya zaidi ni kwamba kwa namna anavyoona, kila siku ugonjwa unaendelea kukua katika mwili wake.

Kwa yeyote mwenye moyo wa kumsaidia chochote, Ayubu awasiliane na Mhariri wa Jarida la Ndani ya Habari, 0754498972.

No comments:

Post a Comment