Rais Evo Morales wa Bolivia amesema
kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuondolewa New York
Marekani na kupelekwa katika nchi nyingine kutokana na siasa za
Washington za kutoa vitisho na kutumia mabavu dhidi ya nchi nyingine.
Rais wa Bolivia ambaye alikuwa
akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa
makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuwa katika nchi inayoheshimu
sheria na makubaliano yote ya kimataifa na isiyotoa hifadhi kwa magaidi
na kuwalinda mafisadi.
Morales amelaani hatua ya Marekani ya kumzuia
Rais wa Venezuela kuhudhuria mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa,
"haiwezekani kwa mtu asiyeamini
ubeberu na mfumo wa kibepari kuwa na usalama mjini New York" alisema Morales.
Morales
vilevile amemkosoa vikali Rais Barack Obama wa Marekani na kusema: Obama
hawezi kuzungumzia amani na uadilifu wakati nchi yake inaendelea
kuingilia masuala ya nchi nyingine na kufanya dhulma katika nchi hizo.
No comments:
Post a Comment