.
Jaji Warioba alisema maoni yaliyomo katika Rasimu
ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi, hivyo lazima yalindwe ili
kudumisha amani... “Kilichomo katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya
wananchi, wasije wakafanya makosa ya kutoa maoni haya. Haya yametoka kwa
wananchi na wao ndiyo watakuwa na sauti ya mwisho kuhusu mchakato huu,”
alisema na kuongeza: “Wahakikishe kwamba mawazo yaliyotolewa na
wananchi yanaingia katika Katiba Mpya, wasithubutu kuyatoa maana
wananchi wanaweza kukataa hali hiyo.”
Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza
sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu
ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa
itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.
Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya
NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi
wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa
Katiba Mpya.
Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu,
muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge
Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa
ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete
anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya
kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa
itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?”
Jaji Warioba pamoja na kukiri upungufu huo, alisema kurekebisha au kutokurekebisha kasoro hizo si jukumu la tume hiyo.
“Tunawaomba watafakari, waone jinsi gani tume
ambayo imekwishavunjwa itakuja kutoa elimu wakati wa kura ya maoni,
sheria ina ‘contradiction’ (ina mkanganyiko),” alisema.
No comments:
Post a Comment