|
KATIKATI: Makam M/Kiti wa kamati ya maadili ya utangazaji nchini Bw. Wolter Bgoya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam |
Kamati ya maadili ya utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadinli ya utangazaji.
Vituo vya radio vilivyofungiwa kutangaza ni IMANI FM cha mjini Morogoro na KWA-NEEMA FM cha jijini Mwanza ambavyo vyote vimefungiwa kwa muda wa miezi sita..
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam, Makam mwenyekiti wa kamati hiyo Walter Bgoya amesema kituo cha IMANI FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi ya 2012 na kituo cha KWA-NEEMA FM kinadaiwa kuchochea mgogoro wa uchinjaji kati ya waislam na wakristo mkoani Geita.
Akitangaza uamuzi huo Bwana Bgoya amesema kituo cha CLOUDS FM kimetakiwa kulipa faini ya Sh. 5 milioni na kufuta kipengele ( segment) cha jicho la ng'ombe kwani kimekuwa kikiendeshwa kwa kutofata maadili na walihusii wa uchaguka katika kushabikia masuala ya ushoga wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa marekani.
CHANZO: Michuzi Blog na Jamii Forum
No comments:
Post a Comment