Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania zimetangaza kuwa zitaandamana Februari 15, mwaka huu endapo
Katibu wa Jumuiya hiyo, Shekh Ponda Isa Ponda, pamoja na wenzake walioko
gerezani hawatapewa dhamana Februari 14.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Amiri Mkuu wa Shura ya
Wahadhiri Tanzania, Kondo Bungo, wakati wa kongamano la mwendelezo wa
kuwainua Waislamu waweze kudai haki zao lililofanyika katiak viwanja vya
Shule ya Sekondari ya Nuruyakin, Temeke, jijini Dar es Salaam.
“Kupewa dhamana ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania, haiwezekani
hadi leo (jana) wenzetu wanasota jela kwa kosa la kutetea haki zao na
wakati wapo watu waliotuhumiwa kuua wamepewa dhamana, lakini Waislamu
wananyimwa, kwa sasa hatutakubali, lazima kieleweke,” alisema Bungo.
Alisema kama dhamana haitapatikana siku hiyo, wataandamana hadi
kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kuhakikisha kuwa haki
inatendeka kwani aliyewanyima dhamana viongozi wao ni yeye (DPP)na siyo
mahakama.
Sheikh Bungo alisema wapo viongozi wengi wa Kiislamu kutoka bara na
visiwani waliokamatwa kwa sababu ya kutetea haki za Waislamu na badala
yake kubadilishiwa makosa wanapofikishwa mahakamani ili ionekane kuwa
wana makosa.
No comments:
Post a Comment