Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEBAINIKA kuwa, Mfumo wa kuwekeza fedha Benki kwa Riba ni anguko la viwanda vya kimataifa na kudumaa kwa uchumi wa Nchi za Afrika.
Kauli hiyo imebainishwa na Mkurugenzi wa huduma ya benki isiyo na riba NBC Yassir Masoud Kigoma Ujiji jana kwenye warsha ya wadau wa uwekezaji wa fedha katika mabenki mbalimbali wakibainishiwa mfumo wa riba na athari zake na chukizo kwa mungu ikiwa
na tija ya kufuata mfumo usiokuwa na riba ( Islamic Banking) ambao unaridhiwa na mungu kwa wananchi wa imani zote za dini hali itakayochochea kupanda kwa uchumi wa mmoja mmoja sanjari na kukua kwa huduma za wananchi .
“Mfumo
wa kuwekeza bila riba unaepusha ugomvi baina ya benki husika na mteja
,wateja wengi wanauziwa thamani zao kutokana na kushindwa kulipa riba ya
fedha alikyokopeshwa,sasa itumieni huduma hii ambayo hata mataifa ya
magharibi ikiwemo marekani ,malasia,Singapore wamebaini hili wanatumia mfumo kama Islamic banking msitishike na jina ni kwa wote wahitaji” alibainisha Masoud.
Meneja wa NBC-Tawi la Kigoma Mathias Mhangilwa
alisema kuwa,mfumo wa Islamic Banking ni uwekezaji wa fedha unaolenga
uhalisia wa maumbile ya mwanadamu ambao unauadilifu kwa mafundisho ya
vitabu vyote vinakataza riba haimanishi ni kwa ajili ya imani ya kislamu
tu ni kwa kila mdau huku akiwataka wafanyabiashara wa kigoma wachangamkie fursa hiyo ili waboreshe tija zao.
“ World Bank inafanya mchakato wa kuhakikisha kuna sera ya
mfumo huu usiokuwa na riba ,pia mfumo huu hauna anguko la kiuchumi
kwani anguko ni chachu ya fedha haramu ya riba watanzania tumechelewa kujiunga
na mfumo huu,lakini sasa utumieni ili nchi yetu isiyumbe kiuchumi ikiwa
mataifa ya magharibi yataanguka cha ajabu 30% waliwekeza mfumo huu ni
wakristo na 2% waislamu msihofu ” alisisitiza Mhangilwa.
Khadija Katumba na Asha Issa walidai kuwa,kutokana na elimu waliyoipata toka kwa NBC-Isalamic Banking ,juu ya adha ya mikopo
ya riba watakuwa mabalozi wa elimu hiyo kwa wanawake wathubutu wa
kufanya biashara waachane na mfumo wa udhalilishaji ambao wengi
wameuziwa majumba yao kutokana na riba ambaye ni sawa na mdudu wa kansa
kwa kumaliza uchumi wa wajasiliamali wasio na elimu juu ya mikopo ya
riba.
Ikumbukwe
kuwa,wadau wa uwekezaji ni wahanga wa kufilisiwa thamani zao na Benki
mbalimbali za hapa nchini pindi wanaposhindwa kulipa deni la mikopo,
hali iliyopelekea Benki ya Taifa NBC kuanzisha huduma hiyo ambayo kwa
sasa unatumiwa ulimwenguni na mataifa ya magharibi na Asia wakijaribu
kufutu (Financial Tsunami) anguko la kiuchumi siku za usoni kwa mujibu
wa mwanazuoni wa zamadamu bara la Asia anayejulikana kama Ibn Qayyim Jawziyya.
No comments:
Post a Comment