Monday, June 3, 2013

BODI YA MIKOPO YAWATAKA WANAFUNZI KUZINGATIA MUDA WA KUOMBA MIKOPO

 
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa msisitizo kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu tayari kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kuanza mara moja na kuzingatia ratiba.

Mkurugenzi wa mawasiliamo wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, alitoa kauli iyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kujaza fomu za maombi na kuwa siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni Juni 30 mwaka huu.

“Bodi inasisitiza kuanza mchakato wa kuomba mikopo kwa waliomaliza kidato cha sita na kuzingatia muda uliotolewa kujaza fomu za maombi na kuziwasilisha kwenye ofisi za bodi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya mikopo na kujaza fomu stahiki, tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi Mei Mosi mwaka huu.

“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wamejaza fomu kwa njia ya mtandao,” alifafanua.
Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, bodi hiyo iliwapatia mikopo waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

No comments:

Post a Comment