- Walishindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili
- Wananchi 13 na Askari 6 waliuawa katika opesheni hiyo
- Ubakaji, Unyanyasaji na uporaji vilitawala katika Operesheni hiyo
Na. Butije Hamisi
Rais Jakaya
kikwete hatimae amekubali ushauri wa wabunge na kuwavua nyadhifa za uwaziri
mawaziri watatu na kukubali kujiulu kwa waziri wa maliasili na utalii baadaya
kutuhumiwa kushindwa kusimamia Operesheni ya Tokomeza Ujangili iliyokuwa imejaa
unyana na ukatili dhidi ya raia wasio na
hatia.
Akitangaza uamuzi
huo wa rais ambe yuko nchini Marekani kwa matibabu wariri mkuu Mh. Mizengo Pinda
alisema rais Kikwete ametengua uteuzi wa mawaziri wanne ambao ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai
Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David
Mathayo.
Hatua hiyo
imefikiwa baada ya Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira
iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, kuonesha kuwa mawaziri hao
waalishindwa kusimamia ipasavyo OTU ambayo ilijawa na vitendo vya ukatili,
unyama, na dhulma dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Kabla ya Pinda
kutangaza hatua hiyo iliyochukuliwa na rais aliyekuwa waziri wa maliasili na
utalii Khamisi Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa
akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa
kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama (CCM).
“Mimi ni mtu
mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge. Rais Kikwete
aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea
hali ya wanyama huko si nzuri ... nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya
uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).”
alisema Kagasheki.
Operesheni hiyo
inadaiwa kukabiliwa na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na mauaji ya wananchi
na wanyama.
Akiwasilisha ripoti
ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira Mwenye kiti wa kamati hiyo James
Lembeli aliituhumu wizara ya maiasili na utalii kuwa imekithiri rushwa kiasi
kwamba inakuwa vigumu kupmbana na kutokomeza ujangili nchini hivyo kutaka
watendaji wakuu wa wizara hiyo kuchukuliwa hatua stahiki
“...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya
Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama
uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani
ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali
izichunguze simu zao kuanzia leo.” Alisema Lembeli.
Wakichangia
ripoti hiyo wabunge waliitaka serikali kuwawajibisha mawaziri ambao waira zao
zilihusika katika operesheni hiyo kuhu wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka
waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda ajiwajibishe kisiasa na wengine wakitaka kama
mawaziri hawakuwajibika basi bunge livunjwe ili ufanyike uchaguzi mwingine.
MICHANGO
YA WABUNGE
Mbunge
wa Longido, Lekule Laizer (CCM), alitaka Bunge livunjwe endapo Waziri Mkuu na
mawaziri hao watatu(Kagasheki, Nchimbi na Nahodha) watakataa kujiuzulu kwa
lengo la kung’ang’ania madaraka.
Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema hakuna jinsi ya kuonyesha namna
wabunge walivyokasirishwa na vitendo hivyo zaidi ya Serikali nzima kwa maana ya
Pinda kujiuzulu.
“Naomba Waziri Mkuu uchukue ‘political responsibility’
(uwajibikaji wa kisiasa) na siyo kwamba kwa kufanya hivyo anahusika la hasha…
Kama hachukui hatua Bunge libebe dhamana hiyo,” alisema Zitto.
Akichangia
bungeni Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alibainisha kutuhumiwa kwa wabunge kwenye ripoti hiyo kwa kujihusisha na ujangili
na kuhujumu operesheni hiyo.
“Bungeni kazi yetu, sisi Wabunge ni kuisimamia
Serikali kwa hiyo wale wabunge waliotajwa kwenye ripoti watajwe ili nao
wawajibike ili Bunge letu liwe na nia thabiti ya kuisimamia Serikali,” alisema
Mbatia.
Ripoti
hiyo ilibainisha Operesheni ya Tokomeza Ujangili ilisababisha mauaji ya watu 13
na askari sita, utesaji wa kutisha wa watuhumiwa, ubakaji, rushwa na uporaji wa
mali za wananchi.
..............................Maoni:- 0752231172
Email: b2jhms@gmail.com
No comments:
Post a Comment