By: Butije Hamisi
Bara la Afrika limempoteza aliyekuwa raisi wa Afrika kusini na wa kwanza
kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Dr.
Nelson Rolihlahla Mandela baada ya
kufariki dunia alhamisi ya tarehe 5 Desemba 2013.
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini
Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Akiwa ni kiongozi shupavu na muumuini wa mabadiliko Mandela atakumbukwa kama kiongozi wa ampambano (vita) dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
KKatika kupinga ubaguzi wa rangi Mandela
alinukuliwa akisema “I hate race
discrimination most intensely and in all its manifestations. I have fought it
all during my life; I fight it now, and will do so until the end of my days.”
Akimaanisha kuwa anachukia ubaguzi wa rangi na amepambana kupinga ubaguzi wa
rangi katika maisha yake, anaendea na ataendelea kupinga ubaguzi huo mpaka
mwisha wa uhai wake.
Mandela alikuwa ni kiongozi wa mfano na
wa kuigwa na aliyekuwa na nia thabiti ya kuliunganisha taifa la Afrika kusini
kwani aliweza kuwasamehe makaburu
waliomtesa yeye na waafika kusini wengine na kumfunga jela kwa miaka 27.
Wakati akitoka jela, Mandela alihutubia
wananchi Jijini Cape Town 11 February 1990 na kusema “I stand here before
you not as a prophet but as a humble servant of you, the people. Your tireless
and heroic sacrifices have made it possible for me to be here today. I
therefore place the remaining years of my life in your hands” (Nipo hapa nanyi si kama Nabii bali kama
mtumishi wenu. Kutokata tama na juhudi zenu ndio zimefanikisha mimi kuwa nanyi
hapa, hivyo ninakabidhi maisha yangu yaliyosalia mikononi mwenu.”
Pia katika
kuonyesha kuwa alijitoa muhanga kuwasaidia watu wote bila kujali rangi zao Mandela
alisamehe kila kitu kilichotokea hapo nyuma “My
message to those of you involved in this battle of brother against brother is
this: take your guns, your knives, and your pangas, and throw them into the
sea! Close down the death factories.
End this war now!” ( Ujumbe wangu kwa wote waliohusika katika vita hii ya
ndugu dhidi ya ndugu yake ni kuwa chukueni bunduki zenu, visu na panga na
mzitupe baharini, sitisheni mauaji na kuacha vita kabisa).
Kitendo cha Mandela kuacha kulipiza
kisasi kwa Makaburu kilikoleza hadhi yake na kung’arisha nia yake ya kutaka
amani ya kweli hali iliyomfanya Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush
kuenesha mshangao na kumuona mtu wa aina yake Nelson Mandela kwa kuwa na uwezo
wa kusamehe watu waliomfunga miaka 27 jela bila makosa, akitoa fundisho kwa
sisi sote kuweza kusamehe hata maadui zetu.
Watu wengi wakiwemo viongozi wa mataifa
mbalimbali duniani wameguswa na msiba huu na kuonesha hisia zao kwa msiba wa
kiongozi shupavu na mwenye sifa za kipekee katika karne ya 20 na 21.
KAULI ZA VIONGOZI WA MATAIFA JUU YA MANDELA
Rais wa Tanzania Mh Dr. Jakaya Kikwete amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
“Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa karne ya 20 na 21. Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwanamapinduzi na mstahamilivu,” alisema Raisi Kikwete.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon mbali na kusikitishwa na msiba huu amempongeza Nelson Mandela kama mtu mnyenyekevu na mafano wa kuigwa na binadamu.
"Nelson
Mandela alikuwa mtu wa aina yake duniani, mtu mwenye utu na aliyefikia
mafanikio ya juu, mwamba wa haki na mnyenyekevu.”
Kwa upande
wake Rais Obama wa Marekani ameungana na wabunge na marais wa zamani kuomboleza
kifo cha Nelson Mandela, akimtaja kuwa mmoja wa watu wenye ushawishi zaidi,
jasiri na mtu mwema kuwahi kuishi.
"Amepata zaidi ya kile kilichotarajiwa kutoka kwa
mtu yeyote. Leo amekwenda nyumbani," alisema Obama "Si wetu tena. Ni wa vizazi vyote.".
Tanzania
imetangaza siku tatu za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingot kuanzia jana
tarehe 6 December 2013 huku mataifa mengine mengi duniani ikwemo Marekani,
Nigeria,
Dr.
Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa
mwaka 1918 na kufariki juzi 5 Desemba 2013 na aba yake alifariki Mandela akiwa
na miaka tisa. Alimtaja baba yake kama mtu mkali mwenye kutaka watu kufuata
maadili mema
Mandela
tazikwa mazishi ya kihistoria na ya aina yake, yatakayofanyika 15 Desemba 2013 katika
kijiji chake cha Qunu, mahala alipopachagua mwenyewe kabla ya kifo chake.
No comments:
Post a Comment