Saturday, December 21, 2013

KIKWETE AWAFUTA KAZI MAWAZIRI MZIGO, NI BAADA YA KUSHINDWA KUSIMAMIA WIZARA ZAO IPASAVYO

  •  Walishindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili
  • Wananchi 13 na Askari 6 waliuawa katika opesheni hiyo
  • Ubakaji, Unyanyasaji na uporaji vilitawala katika Operesheni hiyo

Na. Butije Hamisi

Rais Jakaya kikwete hatimae amekubali ushauri wa wabunge na kuwavua nyadhifa za uwaziri mawaziri watatu na kukubali kujiulu kwa waziri wa maliasili na utalii baadaya kutuhumiwa kushindwa kusimamia Operesheni ya Tokomeza Ujangili iliyokuwa imejaa unyana na  ukatili dhidi ya raia wasio na hatia.

Akitangaza uamuzi huo wa rais ambe yuko nchini Marekani kwa matibabu wariri mkuu Mh. Mizengo Pinda alisema rais Kikwete ametengua uteuzi wa mawaziri wanne ambao ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, kuonesha kuwa mawaziri hao waalishindwa kusimamia ipasavyo OTU ambayo ilijawa na vitendo vya ukatili, unyama, na dhulma dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia.

Kabla ya Pinda kutangaza hatua hiyo iliyochukuliwa na rais aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Khamisi Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama (CCM).
“Mimi ni mtu mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge.  Rais Kikwete aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea hali ya wanyama huko si nzuri ... nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).” alisema Kagasheki.
Operesheni hiyo inadaiwa kukabiliwa na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na mauaji ya wananchi na wanyama.
Akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira Mwenye kiti wa kamati hiyo James Lembeli aliituhumu wizara ya maiasili na utalii kuwa imekithiri rushwa kiasi kwamba inakuwa vigumu kupmbana na kutokomeza ujangili nchini hivyo kutaka watendaji wakuu wa wizara hiyo kuchukuliwa hatua stahiki

 “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.” Alisema Lembeli.
Wakichangia ripoti hiyo wabunge waliitaka serikali kuwawajibisha mawaziri ambao waira zao zilihusika katika operesheni hiyo kuhu wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda ajiwajibishe kisiasa na wengine wakitaka kama mawaziri hawakuwajibika basi bunge livunjwe ili ufanyike uchaguzi mwingine.
MICHANGO YA WABUNGE
Mbunge wa Longido, Lekule Laizer (CCM), alitaka Bunge livunjwe endapo Waziri Mkuu na mawaziri hao watatu(Kagasheki, Nchimbi na Nahodha) watakataa kujiuzulu kwa lengo la kung’ang’ania madaraka.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema hakuna jinsi ya kuonyesha namna wabunge walivyokasirishwa na vitendo hivyo zaidi ya Serikali nzima kwa maana ya Pinda kujiuzulu.
“Naomba Waziri Mkuu uchukue ‘political responsibility’ (uwajibikaji wa kisiasa) na siyo kwamba kwa kufanya hivyo anahusika la hasha… Kama hachukui hatua Bunge libebe dhamana hiyo,” alisema Zitto.
Akichangia bungeni Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alibainisha kutuhumiwa kwa wabunge  kwenye ripoti hiyo kwa kujihusisha na ujangili na kuhujumu operesheni hiyo.
“Bungeni kazi yetu, sisi Wabunge ni kuisimamia Serikali kwa hiyo wale wabunge waliotajwa kwenye ripoti watajwe ili nao wawajibike ili Bunge letu liwe na nia thabiti ya kuisimamia Serikali,” alisema Mbatia.
Ripoti hiyo ilibainisha Operesheni ya Tokomeza Ujangili ilisababisha mauaji ya watu 13 na askari sita, utesaji wa kutisha wa watuhumiwa, ubakaji, rushwa na uporaji wa mali za wananchi.
..............................
Maoni:- 0752231172
Email: b2jhms@gmail.com

SHERIA YA KUWAWAJIBISHA WABUNGE WANAOKWENDA MSOBEMSOBE INAHITAJIKA.

Na. Butije Hamisi

Watu wa kigoma wamekuwa na msemo unaoseama "Kigoma ya sasa sio ile ya zamani, Buzebazeba ya sasa sio ile ya zamani" Hivyo nami nashawishika kusema Tanzania ya sasa sio ile ya zamani.
 
Ni wazi kuwa kwa sasa watu wengi wameamka, wameelimika, wanatambua kila kinanchoendela na wanafuatilia kila hatua inayopipgwa na serikali.
 
Nayasema haya kwa kushangazwa na kauli iliyotolewa bungeni na Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Anne makinda pale aliposema “Waheshimiwa wabunge nimesema kama mlichukua pesa bila safari, mnarudisha si basi…. Wote kabisa ninawajua na ninalifanyia kazi. Wote waliochukua pesa warudishe ndiyo utaratibu wa Serikali na ndivyo inavyotakiwa. Wote watarudisha.” Alisema Anne Makinda.
 
Siamini huenda ipo siku nitaamini. Hivi ukichukua fedha za umaa kwa kazi maalum ya kiserikali ukaenda kufanyia mabo yako binafsi adhabu yake ni kuzirusha tu?
Je huu ni wizi, utapeli ukwapuaji, unyanganyi au nini nini? Hivi hakuna sharia inayoainisha kupelekwa mahakamani mtu aliyechukua fedha kama walivyofanya baadhi ya wabunge?
Chakunishangaza zaidi mbunge anajitetea kwa kujiamini kuwa haikuwa vibaya yeye kuahirisha ziara ya kimafunzo huku akiwa ameshatia mshiko kibindoni.

Friday, December 20, 2013

RAIS KIKWETE AKUBALI KUFUTWA KODI YA LAINI ZA SIMU, ASAINI HATI YA DHARURA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUSWADA WA FEDHA WA 2013

http://tanganyikaone.blogspot.com
By Butije Hamisi- Dar es Salam

Rais wa  jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amesaini hati ya dharura (Certificate of Urgency)  kufuta kodi ya Tsh. 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu iliyopitishwa na Bunge na kuwekwa kwenye bajeti ya 2013/2014.

Kufuatia hatua hiyo Bunge limepelekewa taarifa hiyo na kulichukua kama dharura ili Muswada wa Fedha wa Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu..

Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu, hatua ambayo ilipingwa na wabunge wengi.
Akithibitisha utiaji saini huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete alitia saini hati hiyo juma hili.
“Muheshimiwa Rais ametia saini hati ya dharura kufanyika marekebisho kwa muswada wa fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu” alisema Makamba

Makamba alisema suala la muswada huo kurudishwa bungeni linategemea na ratiba huku akisisitiza kuwa licha ya Bunge kupitisha muswada huo tangu Julai, mwaka huu, bado kodi hizo zilikuwa hazijaanza kutozwa.
Kufuatia kodi hiyo kutoungwa mkono wa wananchi wengi pamoja na wabunge, Julai 23, mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza kukutana na mamlaka zinazohusika na kodi na mawasiliano pamoja na kampuni za simu za mikononi ili kutafuta suluhisho la mgogoro huo wa kodi.
Rais Kikwete Alisema lengo kuu la kukutana huko lilikuwa ni kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh178 bilioni ambazo zitapotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa
Alitoa kauli hiyo alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel, Ikulu, Dar es Salaam.

WAVAA NGUO FUPI NA ZINAZOACHA MAUNGO YA SIRI HADHARI WAKO HATIHATI NCHINI UGANDA, BUNGE LA UGANDA LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA KUPIGA MARUFUKU UVAAJI WA NGUO HIZO


Monday, December 16, 2013

LIPUMBA AMTAKA RAISI KIKWETE KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

By Butije Hamisi
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Pr. Ibrahim Lipumba amemtaka rais Jakaya Mrisho Kikwete kuunda serikali ya kitaifa ili iweze kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya,
 
 Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Lipumba ametaka kuundwa kwa  Tume Huru ya Uchaguzi, kuandikisha wananchi wote wanaostahili kupiga kura wapewe vitambulisho vinavyotumia alama ya mwili ili kuhakikisha uchaguzi wa 2015 unakuwa huru na wa haki.

"Serikali ya umoja wa kitaifa pia iimarishe utendaji wa serikali, ipambane na ubadhirifu ulioainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali na Kamati za Bunge, ianzae kujenga utamaduni wa uwajibikaji na kutumia vizuri fedha za umma kwa maendeleo ya wananchi." imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa taarifa zaidi soma nakala ya taarifa hiyo hapa chini

MSIBA WA BARABARA KIKWAZO CHA USTAWI WA TAIFA, WACHANGIA KUZOROTA KWA SEKTA ZINGINE ZA MAENDELEO


By Butije Hamisi
Nilipita Maeneo mengi! Badhi yalikuwa na mvua, mengine jua kali na mengine yalikuwa na hali ya mawingu na mvua za rasharasha. Nilipita ktk mlima Sekenke sikujua hali ilikuwaje kwani nilikuwa nimesinzia na sasa nipo Dar es Salaam, Tanzania.

Nikiwa safarini nilipigwa na bumbuwazi na kujiuliza HIVI BARABARA ZETU HUWA ZINA EXPIRE (zinakwisha muda wa matumizi yake) baada ya muda gani? Hivi huwa zina expire ndani ya mwaka mmoja? maana kila ukisafiri toka Mwanza/Kigoma kwenda Dar. lazima utakuta sehemu wanatengeneza barabara. Smehemu iliyotengenezwa miezi michache iliyopita utakuta tena inatengenezwa upya au kufanyiwa marekebisho.

Sasa nabaki najiuliza huwa zinatengenezwa zitumike ndani ya mwaka mmoja kasha zitengenezwe tena? Ukiangalia barabara ya kutoka Morogoro to Dodoma upande unaopita gari kutoka Moro to Dom umetitia. Ninajiuliza barabara haina kiwango? au inapitisha vitu vizito zaidi ya uwezo wake? Jijini Dar babara ya Mandela imekuwa ilikarabatiwa kila mara na baada ya muda mfupi inaharibika.
Swali kwa serikali na wadau, Kama tatizo ni mizigo mizito je suluhisho hamlijui? Miaka kadhaa kabla ya shirika la reli T. kubinafsishwa kwa waliojiita wawekezaji ambao walishidwa kuliendesha shirika mizigo mingi ilikuwa ikisafirishwa kwa njia ya reli iweje ishindikane leo? Hivi taifa/Serikali imeshindwa kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo kuboresha reli ili kuokoa maisha ya barabara zetu zinazoendelea kuteketea kila kukicha katika tanuri la malori?

Monday, December 9, 2013

LOWASA AMPONGEZA RAIS KIKWETE, ASEAMA AMELITANGAZA VEMA TAIFA KATIKA MEDANI YA KIMATAIFA.


ZITTO: UWEZO WETU WA KUZALISHA MALI NA KUONDOA UMASIKINI UMEPUNGUA



Saturday, December 7, 2013

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA 2014 NCHINI BRAZI

MAN U YACHAKAZWA, CHELSEA YAPUNGUZWA KASI, LIVERPOOL WACHEKELEA


AFRIKA IMEPOTEZA SHUJAA WA KARNE YA 20/21



By: Butije Hamisi
 
Bara la Afrika limempoteza  aliyekuwa raisi wa Afrika kusini na wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia  Dr. Nelson Rolihlahla Mandela baada ya kufariki dunia alhamisi ya tarehe 5 Desemba 2013.
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.

Akiwa ni kiongozi shupavu na muumuini wa mabadiliko Mandela atakumbukwa kama kiongozi wa ampambano (vita) dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
KKatika kupinga ubaguzi wa rangi Mandela alinukuliwa akisema “I hate race discrimination most intensely and in all its manifestations. I have fought it all during my life; I fight it now, and will do so until the end of my days.” Akimaanisha kuwa anachukia ubaguzi wa rangi na amepambana kupinga ubaguzi wa rangi katika maisha yake, anaendea na ataendelea kupinga ubaguzi huo mpaka mwisha wa uhai wake.

Mandela alikuwa ni kiongozi wa mfano na wa kuigwa na aliyekuwa na nia thabiti ya kuliunganisha taifa la Afrika kusini kwani aliweza  kuwasamehe makaburu waliomtesa yeye na waafika kusini wengine na kumfunga jela kwa miaka 27. 

Wakati akitoka jela, Mandela alihutubia wananchi Jijini Cape Town 11 February 1990 na kusema “I stand here before you not as a prophet but as a humble servant of you, the people. Your tireless and heroic sacrifices have made it possible for me to be here today. I therefore place the remaining years of my life in your hands” (Nipo hapa nanyi si kama Nabii bali kama mtumishi wenu. Kutokata tama na juhudi zenu ndio zimefanikisha mimi kuwa nanyi hapa, hivyo ninakabidhi maisha yangu yaliyosalia mikononi mwenu.” 

Pia katika kuonyesha kuwa alijitoa muhanga kuwasaidia watu wote bila kujali rangi zao Mandela alisamehe kila kitu kilichotokea hapo nyuma “My message to those of you involved in this battle of brother against brother is this: take your guns, your knives, and your pangas, and throw them into the sea! Close down the death factories. End this war now!” ( Ujumbe wangu kwa wote waliohusika katika vita hii ya ndugu dhidi ya ndugu yake ni kuwa chukueni bunduki zenu, visu na panga na mzitupe baharini, sitisheni mauaji na kuacha vita kabisa).

Kitendo cha Mandela kuacha kulipiza kisasi kwa Makaburu kilikoleza hadhi yake na kung’arisha nia yake ya kutaka amani ya kweli hali iliyomfanya Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush kuenesha mshangao na kumuona mtu wa aina yake Nelson Mandela kwa kuwa na uwezo wa kusamehe watu waliomfunga miaka 27 jela bila makosa, akitoa fundisho kwa sisi sote kuweza kusamehe hata maadui zetu.
Watu wengi wakiwemo viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wameguswa na msiba huu na kuonesha hisia zao kwa msiba wa kiongozi shupavu na mwenye sifa za kipekee katika karne ya 20 na 21.

KAULI ZA VIONGOZI WA MATAIFA JUU YA MANDELA
Rais wa Tanzania Mh Dr. Jakaya Kikwete amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

“Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa karne ya 20 na 21. Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwanamapinduzi na mstahamilivu,” alisema Raisi Kikwete.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon mbali na kusikitishwa na msiba huu amempongeza Nelson Mandela kama mtu mnyenyekevu na mafano wa kuigwa na binadamu.
"Nelson Mandela alikuwa mtu wa aina yake duniani, mtu mwenye utu na aliyefikia mafanikio ya juu, mwamba wa haki na mnyenyekevu.”

Kwa upande wake Rais Obama wa Marekani ameungana na wabunge na marais wa zamani kuomboleza kifo cha Nelson Mandela, akimtaja kuwa mmoja wa watu wenye ushawishi zaidi, jasiri na mtu mwema kuwahi kuishi.
"Amepata zaidi ya kile kilichotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote. Leo amekwenda nyumbani," alisema Obama "Si wetu tena. Ni wa vizazi vyote.".
Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingot kuanzia jana tarehe 6 December 2013 huku mataifa mengine mengi duniani ikwemo Marekani, Nigeria,

Dr. Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa mwaka 1918 na kufariki juzi 5 Desemba 2013 na aba yake alifariki Mandela akiwa na miaka tisa. Alimtaja baba yake kama mtu mkali mwenye kutaka watu kufuata maadili mema
Mandela tazikwa mazishi ya kihistoria na ya aina yake, yatakayofanyika 15 Desemba 2013 katika kijiji chake cha Qunu, mahala alipopachagua mwenyewe kabla ya kifo chake.

Thursday, December 5, 2013

PINDA ATANGAZA MSHAHARA WAKE, ASEMA NI Ml. 6 KWA MWEZI NA SI Ml. 30 KAMA ALIVYODAI ZITTO


Tuesday, December 3, 2013

MWENYEKITI WA CHADEMA SINGIDA (M) AJIUZULU, NI KUPINGA KWA ZITTO NA WENZAKE KUVULIWA NYADHIFA NDANI YA CHAMA