Friday, November 1, 2013

KIKULACHO CHAKO: NIMEUZA MITUMBA MPAKA MIGUU IMEOTA MATEGE, WALOPATA CHETI CHA F4 MAMBO YAO SI HABA


"....baada ya kudunda kidato cha miaka kadhaa iliyopita, nikaona nikaona niingie mtaani kufukuzana na shilingi...lakini miaka yote hiyo pesa nayo imeota miguu na imenizidi kasi...kazi zenyewe ngumu na pia hazina future...nimeuza mitumba mpaka miguu imepata matege sababu ya kutembea...nikifungua kibanda askari wa jiji wanakibomoa..nikaona nibahatishe kwenye zege....nako nimebeba mpaka kichwa kimepata kipara...na mgongo umepinda....lakini nikiwacheki wenzangu angalau waliopata cheti cha form 4 mambo yao si haba na mimi nimeona bora nirudi school...wadau wa elimu mnanishauri vp..?..nawasilisha.."

No comments:

Post a Comment