Mahakama nchini Misri imewapa hukumu
ya kunyongwa watu saba walioshukiwa kuitengeza filamu iliyosababisha
kero na ghadhabu katika ulimwengu wa kiisilamu mapema mwaka huu.
Hasira dhidi ya filamu hiyo iliyokuwa inamkejeli
Mtume Mohammed, ilisababisha maandamano dhidi ya Marekani kiasi cha
kuteketezwa ubalozi wake nchini Libya.Washukiwa hao saba walihukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.
Hukumu hizo ziliidhinishwa na Mufti mkuu nchini Misri ambaye pia ni msomi wa dini ya kiisilamu.
Filamu hiyo ilitengezwa mjini Carlifonia, Marekani na kutolewa kwenye internet mwezi Septemba.
Miongoni mwa wale walioshtakiwa ni mtengezaji wa filamu yenyewe Morris Sadek ambaye ni raia wa Misri.
Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti
No comments:
Post a Comment