SOURCE: Idhaa ya Kiswahili ya Tehran
Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel
katika duru mpya ya mashambulizi yake huko Ghaza ambayo yalianza
Jumatano iliyopita zimekuwa na maafa ya kutisha sawa na mashambulizi
mengine ya utawala huo, kwa kadiri kwamba hadi sasa mamia ya Wapalestina
wameuliwa shahidi na kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto wadogo,
wanawake na wazee.
Jinai kubwa za utawala wa Kizayuni
katika siku kadhaa zilizopita zimewatia wasiwasi mkubwa walimwengu.
Ripoti za mashirika mbalimbali ya kimataifa kuhusu takwimu za watu
waliouliwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika
siku kadhaa zilizopita huko Ghaza zinazungumzia maafa makubwa ambayo
hayajawahi kushuhudiwa katika duru hii mpya ya hujuma ya Israel huko
Ukanda wa Ghaza.
Taarifa ya Mfuko wa Watoto wa Kimataifa
(Unicef) imeeleza kuwa makumi ya watoto wa Kipalestina wameuliwa au
kujeruhiwa katika mashambulizi yanayofanywa sasa na utawala wa Kizayuni
huko Ghaza. Hii ni katika hali ambayo idadi ya Wapalestina wanaouliwa
shahidi katika mashambulizi hayo ya Israel hususan watoto wadogo
inaongezeka.
Weledi wengi wa masuala ya kisheria
wamesema baada ya kushuhudia na kutathmini hali ya mambo ya Ghaza kuwa
hatua ya Israel ya kuendelea kuwauwa kwa umati Wapalestina ni ushahidi
wa wazi wa jinai dhidi ya binadamu. Katika mazingira hayo fikra za walio
wengi zinataraji kuwa taasisi za kimataifa zitachukua hatua haraka
iwezekanavyo kusimamisha jinai hizo za utawala wa Kizayuni na mauaji
makubwa yanayofanywa dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Palestina. Hii ni
katika hali ambayo taasisi za kimataifa zimeendelea kukaa kimya mbele ya
jinai hizo na utawala wa Israel, suala ambalo limeupa utawala huo
kiburi cha kuendeleza jinai na mauaji yake huko Ghaza.
Habari zinasema kuwa utawala wa Kizayuni
unajiandaa kufanya oparesheni kubwa ya nchi kavu huko Ghaza na katika
fremu hiyo Israel tayari imetuma vikosi na zana nzito za kijeshi katika
mipaka ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Serikali za Magharibi ambazo
zinaendeleza kuuunga mkono utawala haramu wa Israel zimekosolewa vikali
na walimwengu na kutambuliwa kuwa ni washirika wakuu wa Israel katika
jinai hizo.
Utawala wa Kizayuni umeshadidisha jinai
zake huko Ghaza ili kutimiza malengo yake makuu ambayo moja kati ya hayo
ni kujionyesha kuwa na nguvu kubwa na kuzusha hofu na wasiwasi ili
kuwalazimisha Wapalestina wasalimu amri mbele ya siasa zake za kujitanua
katika ardhi za Palestina. Israel ambayo mwaka 2005 ilipata pigo kubwa
mbele ya muqawama wa wananchi wa Palestina na kulazimika kuondoka Ghaza
kwa madhila hivi sasa inatumia njia mbalimbali ili kulikalia tena eneo
hilo. Mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2008, Israel ilianzisha vita vya
siku 22 dhidi ya Ghaza kwa uungaji mkono wa Marekani lengo likiwa ni
kulikalia tena kwa mabavu eneo hilo. Hata hivyo katika vita hivyo vya
siku 22 ambayo vilimalizika mwanzoni mwaka mwaka 2009, utawala wa
Kizayuni ulishindwa kufikia malengo yake haramu licha ya kutenda jinai
kubwa dhidi ya wananchi wa Palestina na kuwauwa shahidi maelfu ya raia
hao kutokana mapambano makubwa ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza.
Kwa hali yoyote ile kushadidi
mashambulizi na ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu
wa Gaza kumedhihirisha tena sura halisi ya ugaidi, kupenda vita, ukatili
na mauaji ya utawala huo jambo ambalo limekabiliwa na radiamali kali ya
fikra za walio wengi duniani. Maandamano makubwa yanayofanyika katika
pembe mbalimbali duniani kwa ajili ya kuulaani utawala haramu wa Israel
yanadhihirisha hasira kubwa za waliwengu kwa utawala huo unaotenda jinai
za kutisha dhidi ya raia wasio na ulinzi wala hatia wa Ukanda wa
Ghaza.
No comments:
Post a Comment