Thursday, September 12, 2013

KIKWETE: MTAAMBUKA BAADA YA 2015

 
Rais Jakaya Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji wake, wataona aibu atakapomaliza muhula wake 2015 huku akiwananga baadhi ya wanaCCM kwa kushindwa kuyaelezea mafanikio ya Serikali chini ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme katika mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), Rais Kikwete alisema: “Wakati wa kampeni nilibezwa sana, lakini sasa ninawaomba walionibeza kufika vijijini na kuangalia ukamilishaji wa ahadi zangu.
“Nataka waje waone, kwa sasa ninakamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote ili kufikia lengo la Watanzania asilimi 30 kufikiwa na nishati hiyo. Hadi 2015 umeme utakuwa umesambaa nchi nzima.
“Serikali yangu itavunja rekodi ya kusambaza umeme katika vijiji vingi nchini…Tumejenga mtandao wa barabara kwa sasa, hali yetu ya barabara ni bora Afrika Mashariki, tuliahidi meli Bukoba naomba niwaeleze kuwa zinakuja, tena siyo moja ni meli mbili.
Septemba 2 mwaka huu, Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ilitangaza kuanza kwa awamu ya pili ya usambazaji wa umeme vijijini, mpango ambao utagharimu Sh881 bilioni na kukamilika Juni 2015.
Katika utekelezaji wa mradi huo, huduma za jamii zitakazopewa kipaumbele katika kuunganishiwa umeme ni shule, zahanati, misikiti, makanisa na visima vya maji.
Mpango huo unatarajiwa kuinufaisha mikoa 24 ya Tanzania Bara, huku wateja 250,000 wa awali wakiunganishwa pamoja na kuhusisha kazi ya usambazaji umeme kwenye makao makuu ya wilaya 13 zisizokuwa na umeme.
Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Balozi Ami Mpungwe alisema tayari mikoa 14 imepata makandarasi na ujenzi wa vituo sita vya usambazaji umeme, wakati mchakato wa kuwapata wajenzi katika mikoa 13 iliyokosa wakandarasi awali, unaendelea.

CHANZO: MWANANCHI

TUMSAIDIE MTANZANIA MENZETU KUPATA MATIBABU YA UGONJWA UNAOMSUMBUA


Joseph Ayubu (40) mkazi wa Kijiji cha  Nyenze wilayani Kishapu,  mkoani Shinyanga, kwa miaka mingi amekuwa akihangaika kupata tiba ya tatizo lake bila mafanikio.

Ayubu anateswa na ugonjwa wa kansa, hali yake kwa sasa ni mbaya, anatokwa na usaa mwingi; akiukinga usaha unaotoka shingoni, kikombe hujaa ndani ya dakika moja.

“Nimevumilia mno, kadri siku zinavyokwenda mbele naona kifo kinakuja. Sitaki kuamini kama ulimwengu wote au Watanzania wote wanaweza kuwa na roho ngumu ya kushindwa kuniokoa, naomba msaada niondokane na shida hii,”  anasema Ayubu.

 Anawaomba wasamaria wema wamchangie fedha  ili akatibiwe katika Hospitali ya KCMC iliyoko mkoani Kilimanjaro.
Ayubu anasumbuliwa na tatizo la saratani  ya shingo, hivyo kusababisha shingo yake kuvimba na kumfanya ashindwe kutoa sauti  ipasavyo kwani sehemu kubwa ya koo lake imeziba.

Anaeleza kuwa kutokana na ugonjwa huo, kichwa nacho kinazidi kuvimba na kupata maumivu makali.
Macho nayo yanavimba na kumsababishia ashindwe kuona  mbali. Mbaya zaidi ni kwamba kwa namna anavyoona, kila siku ugonjwa unaendelea kukua katika mwili wake.

Kwa yeyote mwenye moyo wa kumsaidia chochote, Ayubu awasiliane na Mhariri wa Jarida la Ndani ya Habari, 0754498972.

Sunday, September 8, 2013

SHOGA ASU AAMUA KUOKOKA, ATUBU DHAMBI,AJIANDAA KUOA ILI AWE NA FAMILIA.





TAMAA ya kua na mke na kuitwa baba, ndiyo imemfanya shoga maarufu jijini Dar es Salaam anaye julikana kwa jina la Othuman Hamis au Anti Asu kuamua kuvua gwanda la kua `mototo si riziki’ na kuvaa gwanda jingine la `kidume cha mbegu’.

Anti Asu ambaye pia ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga, inaelezwa kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumzalia watoto na ambaye atampa mapenzi ya dhati.

Imedaiwa kwamba, hivi karibuni Asu alijisalimisha katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako alitubu dhambi zake. 

Sani liliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo lilifanikiwa kumnasa Asu akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo Magomeni Mapipa jijini anakofanya kazi.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli ameacha tabia hizo na kwa sasa ameokoka na  anaitwa Amos. 
``Nimeokoka kiukweli kabisa. Sitaki tena  kuusikia ushoga. Nimemkaribisha mungu katika maisha yangu. Najutia dhambi zangu na namuomba yeye (Mungu) anisimamie na kunilinda ili nisiweze kuanguka tena,’’ alisema Anti Asu ambaye anaonekana ni mwanaume halisi. Amesema kwamba, ameamua kuanza maisha mapya na kwamba anaishi katika kanisa la TAG Magomeni ambako amekuwa akikesha kwa maombi.

``Mimi nilikua shoga namba moja Tanzania baada ya marehemu Anti Kessy. Hakuna alieyekua ananifikia.Nimevunja ndoa zaidi ya 30 na nimetembea na wanaume hata zaidi ya 200. Nimeishi kinyumba na wanaume zaidi ya 10. 
Nimebwakwa na kufanya kila aina ya ufilauni. Nani ambaye alikua ananifikia mimi?  Shoga gani ajitokeze hapa. Lakini sasa nimeachana na yote haya baada ya kubaini nilikua naitwa na Mungu. Nimeludi kwake na ninahisi amani moyoni mwangu,’’ amesema. 

Ameongeza kwamba kwa sasa anajiandaa kuoa kwani alipima kama ana maambukizi ya maradhi ya Ukimwi na majibu yameonyesha kwamba yupo salama.`` Nashukuru kwamba hata jogoo anawika.’’ Aliongeza kwamba sababu nyingine nyingine iliyosababisha   aokoke ni kutokana na kuugua sana tangu alipokumbwa na tukio la kubakwa na wanaume zaidi ya 10. 
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Dunstan Kanemba amethibitisha kuokoka kwa Anti Asu na kusema kwamba yeye ndiye aliyemuombea na kumkaribisha rasmi kanisani hapo. 
``NI kweli Amosi (Anti Asu) tunaye hapa.Ibada ya Jumapili iliyopita tulimuombea hadharani na alidondoka chini. Hii ni ishara kwamba alikua na mapepo yanayomsumbua. Kanisa limempa hifadhi ya kuishi hapawakati tunamjenga kiroho. 
 
Pia tunamhudumia kwa mavazi na mahitaji mengine,’’ alisema Kanemba. Aliongeza kwamba uamuzi aliofanya kijana huyo ni wa msingi na kuwataka watu wengine ndani ya jamii wenye matatizo kama hayo kufika kanisani hapo kupata msaada wa maombi. 
``kwa yoyote anayehitaji kumsaidia zaidi kimwili basi asisite kufika hapa kanisani. Tunaamini kuwa kuokoka kwake kutasaidia sana kuwafanya vijana wengine wenye tabia hiyo kuokoka pia au kuacha’’ alisema Kanemba.

CHANZO: http://jumamtanda.blogspot.com/

WATAHINIWA 3000 KUTOFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA 4 2013

Dar es Salaam. 
Watahiniwa 3,000 wa kujitegemea wako hatarini kutofanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kutokuwa na taarifa zao za kulipia karo za mtihani huo pamoja na zile za usajili.
Tayari Necta imetuma barua kwa watahin
iwa hao kuwaeleza kuwa hawatafanya mtihani mwaka huu.
Licha ya maelezo hayo ya Necta, taarifa zinaonyesha kuwa watahiniwa hao walishalipa ada za mtihani huo kupitia njia mbalimbali za kielektroniki zilizoainishwa na baraza hilo, ikiwamo benki na kampuni za simu za mkononi.
Watahiniwa walipaswa kulipa Sh35,000 ikiwa ni ada za mtihani huo kupitia wakala mbalimbali walioteuliwa na Necta.
Gazeti hili lilifanikiwa kuona barua ya Necta kwenda kwa mmoja wa wanafunzi waliojisajili kufanya mtihani huo kwa mwaka 2013 ikimweleza kuwa, hataweza tena kufanya mtihani huo kwa kuwa hakulipa karo ya mtihani huo.
Barua hiyo ilieleza kuwa, kumbukumbu za Necta zinaonyesha kuwa wanafunzi hao wamejiandikisha kufanya mtihani, lakini hawajawasilisha fomu za usajili wala kulipa karo za mtihani huo.
“Hivyo kwa barua hii, unafahamishwa kuwa umeondolewa kuwa mtahiniwa mwaka 2013,” ilisema sehemu ya barua hiyo zilizosambazwa kwa watahiniwa hao.
Kutokana na kuwepo hali hiyo, baadhi ya watahiniwa kutoka maeneo mbalimbali nchini, wameanza kufuatilia Necta kujua hatima yao wakiwa na vielelezo vya malipo yao.
Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alithibitisha kuwa baraza hilo liliandika barua kwenda kwa watahiniwa takriban 3,000 waliokuwa wamejiandikisha kama watahiniwa binafsi na kuwaeleza kuwa hawatafanya mtihani huo kwa mwaka huu.
Alifafanua kuwa, baadhi yao walifika Necta wakiwa na stakabadhi zilizothibitisha kuwa wamelipa karo hiyo na hivyo kurudishwa kwenye kundi la watakaofanya mtihani huo mwaka huu.
“Necta hatupokei fedha moja kwa moja, tuna mawakala, kilichotokea ni kuwa baadhi ya watu walilipa karo za mitihani, lakini kwenye mfumo wetu tulikuwa hatuoni kama walilipa,” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo watu wote walioandikiwa hizo barua ni wale ambao kwenye mfumo wetu hawaonekani kama wamelipa, lakini wengi wa hawa walikuja na risiti zikionyesha kuwa walikuwa wamelipa na wakarudishwa kwenye mfumo,” alisema. MWANANCHI