Tuesday, August 20, 2013

MAHAKAMA YA MISRI YAAMURU MUBARAK AACHIWE HURU


 

Mahakama ya Misri imeamuru kuachiliwa huru aliyekuwa raisi wa nchi hiyo aliyepinduliwa madarakani kwa maandamano ya wananchi Hosni Mubarak.
Mahakama hiyo imesema kuwa hakupatwa na hatia katika kesi iliyokuwa imebakia ya ubadhilifu. Kwa mujibu wa wakili wake na duru za mahakama za Misri, korti imeamuru Mubarak aachiliwe huru katika kesi ambayo yeye na watoto wake wawili Alaa na Gamal walikuwa wakituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

Taarifa hiyo inasema kwamba, Mubarak anaweza kuachiliwa huru wiki hii, lakini watoto wake wawili wataendelea kushikiliwa. Huko nyuma pia iliamriwa kwamba  Mubarak aachiliwe huru katika kesi nyingine mbili ambapo alishitakiwa kuhusika katika mauaji ya waandamaji wakati wa harakati za maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimuaondoa madarakani na pia kujilimbikizia mali kinyume cha sheria.

NEWS OF RWANDA: RAISI KIIKWETE SI MTANZANIA, ASILI YAKE NI BURUNDI



Kufuatia sinto fahamu iliyopo kati ya Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete na Rais wa Rwanda  Paul Kagame mtandao wa kinyarwanda uitwao News of Rwanda umetoa taarifa inayomtuhumu Raisi kikwete kuwa si mtanzania bali ni raia wa burundi.
Katika tuhuma hizo mtandao huo umeshindwa kuonyesha ushahidi wa kiukoo na familia kuthibitisha tuhuma hizo baili ulijikita zaidi kwa kuangali historia kuwa Bagamoyo (Nyumbani kwao na Raisi Kikwete) ilikuwa ni kitovu cha biashara ya utumwa A. Mashariki hivyo baadhi ya watumwa kutoka Rwanda na Burundi walibakia Bagamoyo na kuanzisha makazi na hatimae familia.
Pia mtandao huo umeandika kuwa mke wa Raisi Kikwete Mama Salma Kikwete ni ndugu wa aliyekuwa raisi wa Rwanda Juvenal Habyarimana aliyeuawa kwa ajali ya ndege iliyotunguliwa mwaka 1994 nchini Rwanda. Kwa taarifa zaidi bofya hapa chini. 
bofya hapa

Monday, August 19, 2013

IKOWAPI DEMOKRASIA YA USA?


Photo From Mwananchi Newspaper


UTAPELI HUU UNAOFANYWA KWA WATU WANAOTAFUTA KAZI

TUNAOTAFUTA KAZI WAANGALIENI SANA WATU HAWA (Soma sms zinazotumwa)
 Hello, am Abdul from Climate Watch dsm, nimeona cv yako for Project officer post, nataka kukusaidia upate hii kazi, but ukipata salary ya kwanza utanipa kitu kidogo, salary is 1.2 Million. nimeongea na HR manager kakubali ila anataka tsh. laki 1 leo ili upite directly me nina elfu 65 tu, kama upo ready tuma elfu 35 nimkabidhi. tuma by M-pesa 0756 970602 or tigo pesa 0659777076, jitahidi utume mapema cv yako nimempa me naingia kikaoni  atakupigia badae.
 &
Hello, am Abdul from Raven Ltd dsm, nimeona cv yako for Marketing officer nataka kukusaidia upate hii kazi, but ukipata salary ya kwanza utanipa kitu kidogo, salary is 1.2 Million. nimeongea na HR manager kakubali ila anataka tsh. laki 1 leo ili upite directly me nina elfu 60 tu, kama upo ready tuma elfu 40 nimkabidhi. tuma by m-pesa yangu 0756 970602 or tigo pesa 0659777076, jitahidi utume mapema cv yako nimempa me naingia kikaoni  atakupigia badae.

KONGAMANO LA WAISLAM LATAKA KUTOCHAGULIWA CCM, MAANDAMANO YA NCHI NZIMA YAANDALIWA, LATAKA TUME HURU UCHUNGUZI WA CHEIKH PONDA

Sakata la kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, limepamba moto, baada ya mkutano wa Waislamu jana kuibua mapya.

Kati ya mapya yaliyoibuliwa katika mkutano huo ni pamoja na kupitisha maazimio matatu likiwamo la kuhamasishana kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi utakaoitishwa wakati wowote kuanzia sasa.

Maazimio mengine yanawataka Waislamu kujiandaa kwa maandamano yatakayofanyika nchini kote kupinga dhuluma na kudai haki zao.

Pia kuitaka serikali iunde Tume huru ya uchunguzi wa tukio la kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.

Maazimio hayo yalisomwa na Sheikh Kondo Juma Bungo, katika kongamano la waumini hao, lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za KiislamuTanzania, katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Akisoma maazimio hayo, Sheikh Kondo alisema tatizo la msingi dhidi ya Waislamu ni CCM.

Sheikh Kondo alisema juzi walishindwa kufanya maandamano kwa sababu hawakuwa wamejiandaa, hivyo anajiandaa kufanya maandamano nchini kote.

Hata hivyo, alisema Rais Jakaya Kikwete, bado ana nafasi ya kuundaTume huru kuchunguza tukio la
kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda na kwamba wakati hatua hiyo ikisubiriwa hatua nyingine zichukuliwe.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kushtakiwa mahakamani kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, Mkuu wa Kikosi cha Polisi kilichoongoza operesheni katika tukio lililosababisha kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda na askari polisi anayetuhumiwa kumpiga risasi Sheikh huyo.

Hatua nyingine ni kujiuzulu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Awali, akiwasilisha mada kuhusu yaliyosababisha Sheikh Ponda kujeruhiwa, Sheikh Suleiman Daudi, alisema kwenye kongamano hilo kuwa ni kuzungumzia madai ya Waislamu ya muda mrefu.

Alisema baadhi ya madai hayo ni Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) na kurejeshwa kwa Mahakamaya Kadhi.

Kwa mujibu wa Sheikh Suleiman, madai hayo yaliwahi kuwasilishwa na Waislamu kupitia halmashauri yao serikalini lakini hayakufanyiwa kazi.

Alisema wanashangazwa kuona baadhi ya makundi ya watu katika jamii, wakiwamo wanasiasa wakitoa kauli za uchochezi, kama vile nchi haitatawalika,lakini hawajawahi kufanyiwa kama alivyofanyiwa Sheikh Ponda.

Naye Sheikh Hussein Ismail, alisema Waislamu wanaviamini vyombo vya sheria nchini, hivyo akawataka Waislamu wachangie gharama za kuwezesha kusimamia kesi inayomkabili Sheikh Ponda mahakamani.

Kutokana na wito huo, Waislamu waliohudhuria kongamano hilo waliitikia na kuchangia fedha taslim katika viwanja hivyo.