Mahakama ya Misri imeamuru kuachiliwa huru aliyekuwa raisi wa nchi hiyo aliyepinduliwa madarakani kwa maandamano ya wananchi Hosni Mubarak.
Mahakama hiyo imesema kuwa hakupatwa na hatia katika kesi iliyokuwa imebakia ya ubadhilifu. Kwa mujibu wa wakili wake na duru za mahakama za Misri, korti imeamuru Mubarak aachiliwe huru katika kesi ambayo yeye na watoto wake wawili Alaa na Gamal walikuwa wakituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.
Taarifa hiyo inasema kwamba, Mubarak anaweza kuachiliwa huru wiki hii, lakini watoto wake wawili wataendelea kushikiliwa. Huko nyuma pia iliamriwa kwamba Mubarak aachiliwe huru katika kesi nyingine mbili ambapo alishitakiwa kuhusika katika mauaji ya waandamaji wakati wa harakati za maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimuaondoa madarakani na pia kujilimbikizia mali kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment