Na Butije Hamisi- Mwanza
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu Ameitaka jamii
na kila mtu kutumia nafasi alonayo kuzuia ukatili wa kijinsia ili kuboresha
afya ya jamii.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa siku 16 za kupambana na
ukatili dhidi ya wanawake uliofanyika jana katika viwanja vya line polisi
Mabatini jijini Mwanza.
Kamanda Mangu amesema kanda ya ziwa inaongoza kwa matukio ya
kikatili nchini, hivyo watu wote hawana budi kuamka kupambana na ukatili huo.
“Uwepo wa matukio hayo unaleta haja ya walio katika nafasi
kusimama na kuzuia vitendo vya ukatili” alisema kamanda Mangu
Kamanda mangu amesema mkoani mwanza mpaka sasa matukio ya
mauaji ya kishirikina yamefikia 40 na watu 44 wakipoteza maisha katika matukio
hayo wanawake wakiwa ni 34 na wanaume 10 tu. Huku watuhumiwa 133 wakishikiliwa
na jeshi la polisi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa shirika la
KIVULINI Bw. Ramadhan Masele amesema
kampeni hiyo ya siku 16 inalenga kuamsha ari kwa watanzania kupambana na
ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na kauli mbiu ya kampeni hiyo ni “Funguka
! Tumia mamlaka yako, zuia ukatili wa kijinsia, kuboresha afya ya jamii.
Bw. Masele amebainisha kuwa kukosekana kwa sheria maalumu
inayohusika na ukatili wa kijinsia, mitazamo hasi ya jamii dhidi ya wanawake,
ukosefu wa huduma bora za afya na vitisho kwa wahanga wa ukatili ni baadhi ya
changamoto zinazo wakabili katika harakati za kupambana na ukatili wa kijinsia.
Pia Diwani wa kata ya Mbugani Bw. Hashim Hassan Kijuu
ameitaka jamii kushirikana katika ngazi zote toka familia, mtaa mpaka taifa kupambana
dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Shirika la KIVULINI limekuwa likendesha harakati za kupinga
ukatili dhidi ya wanawake na watoto na siku ya November 25 ya kila mwaka ni
siku ya kimataifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake duniani.
No comments:
Post a Comment