Friday, May 31, 2013

CHADEMA, CUF WAOMBA RADHI KUFUATIA VURUGU ZA JANA BUNGENI

145
Chama cha CUF na Chadema vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF  chenye mrengo wa Kiliberali  na Chadema kimefanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao  kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo  pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni  na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni ushoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo  John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo.

MATOKEO YA KIDATO CHA 6 YATANGAZWA HUKU UFAULU UKIONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA JANA

kawambwa
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita huku ufaulu ukiongezeka kulinganisha na mwaka jana. Shule ya Marian Girls imeendelea kuongoza kwa kushika namba moja ikifuatiwa na shule ya Mzumbe. 
Kwa matokeo kamli bofya hapa

MATOKEO YA KIDATO CHA 6 2013

Thursday, May 30, 2013

MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA 4 2012

Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Mh. Shukuru Kawambwa ametangaza matokeo mapya ya kidato cha nne 2012. Kwa taarifa kamili bofya hapa chini.
MATOKEO MAPYA KIDATO CHA 4 2013

Tuesday, May 21, 2013

CHANGUDOA: WABUNGE NDIO WATEJA WETU, WANAFUNZI WA VYUO NA RAIA WA NJE WAVAMIA BIASHARA YAO


WAKATI Serikali ikitafuta kila njia ya kukomesha biashara ya ngono, hali imezidi kuwa tete jijini Dodoma baada ya kundi la makahaba kutoka ndani na nje ya nchi kupiga kambi katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Dodoma wafanyabiashara hao walidai kwamba biashara yao imevamiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.

"Wanafunzi wamevamia wateja wetu, ambayo wengi wao ni wabunge, na tumekuwa na wakati mgumu kwa sababu wanafunzi hao wanamvuto zaidi kutoka na umri wao kuwa mdogo,maumbile mazuri zaidi yetu, ingawa gharama zao ni kubwa kuliko gharama zetu, lakini bado wanatuzidi ujanja"alisema mama wa makamo anayesomesha watoto wake kwa kutumia biashara hiyo.

Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mariam (35) alidai kwamba awali alikuwa akifanya biashara hiyo jijini Dar es Salaam na kituo chake kikuu ilikuwa ni Kinondoni Makaburini na alilazimika kuhamia mjini Dodoma miaka miwili iliyopita na kupata mafanikio makubwa kupitia biashara hiyo.

Uchunguzi wa kina uliofanywa umebaini maeneo ambayo yana wasichana wengi ambao ni makahaba ni Chako Nichako, Double H na Mtaa wa Uhindini ambako kuna nyumba maarufu kwa kufanya biashara hiyo haramu ya ngono.

Kahaba mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Anastazia (20) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) alisema kwamba viwango vyake ni kati ya   sh 200,000 kwa tendo moja bila kulala sh 300,000  kwa mchepuo mmoja wakati wa kulala na akitaka michepuo miwili na zaidi ni tsh 400,000 hadi 500,000 wakati wale wamama wakubwa wanajiuza kwa tsh 30,000 hadi 50,000 tendo moja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi alishatangaza kuwawinda na kuwatia kwenye mikono ya sheria wale wanaojihusisha na biashara hiyo haramu. Hata hivyo, kauli hiyo inaonekana kukosa mashiko kwani biashara hiyo inazidi kushamiri siku hadi siku.

CHANZO: http://habarimpya.com

MISAMAHA YA KODI NI JANGA KWA MUSTAKABALI WETU KAMA TAIFA


       By Said Msonga
Misamaha ya kodi imefikia Tsh 1.8 Trilioni kwa mwaka, hizi ni fedha nyingi sana endapo kama zingetumika vema katika miradi ya kimaendeleo. Jana Dr John Pombe Magufuli amesoma bajeti ya Wizara ya Ujenzi yenye jumla ya Tsh 1.2 Trilioni (hivyo misamaha ya kodi ni 150% ya bajeti ya Ujenzi kwa mwaka 2013/14, pia ni 300% ya Bajeti ya Wizara ya Maji 2013/14). Ni nani hasa anayesamehewa matrilioni haya na kwa manufaa gani kwa umma wetu?

Ipo haja sasa tukawa na mfumo makini wa kuchunguza ni kina nani? kwa shughuli zipi? zenye tija gani na umma wanastahili kupewa misamaha hii ya kodi? Inawezekana tukaendelea kulialia kuwa nchi yetu ni masikini lakini tunasahau kuwa huwenda umasikini wetu ni "ukosefu wa viongozi makini" ambao wanaweza kusimamia vema mapato ya nchi na kupanga mipango ya kimaendeleo.

Nakumbuka mwaka 2009 (kama sijakosea) Serikali kwa ushauri wa TRA iliridhia kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija kwa mashirika, makampuni na taasisi za kidini ili kuongeza ukusanyaji mapato na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya fursa ya misamaha ya kodi. Kila mmoja anakumbuka taasisi za dini ndizo zilikuja juu na kumlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufuta uamuzi wa Serikali ambao ulikuwa umepokelewa kwa mikono miwili na wana taifa hili.

Kama mipango ya Ujenzi wa miundombinu aliyotusomea Dr Magufuli haitakamilika kwa kisingizio cha kuwa na nakisi ya bajeti, kama miradi ya maji mijini na vivijini haitakamilika kwa kisingizio cha nakisi ya bajeti ni wazi kuwa taifa hili tunaongozwa na watu wasio makini na maisha ya watanzania wenziwao, na kwa mnasaba huo viongozi hao watakuwa wamethibitisha kushindwa kwao kiuongozi na wajibu wa wanataifa hili ni kuwachukulia hatua stahiki muda ukiwadia.

Pamoja na hayo ni wakati sasa wa kujua ni kina nani wanaonufaika na misamaha hii ya kodi? Tunakumbuka ripoti ya TRA ilibaini kuwa watu/makampuni/mashiriki/taasisi za dini wanajinufaisha sana na kujineemesha kutokana na misamaha hii ya kodi. LAZIMA tuwe na mfumo maalumu wa kuzifuatilia fedha hizi ili kama zina manufaa yaonekane kuleta athari kwa jamii na pia shughuli za taasisi na mashirika hayo ziwe zinafanyiwa ukaguzi kubaini uhalisia wake badala ya kuyaacha mambo kujiendesha kihobelahobela.

Kama itaonekana inafaa ni vema Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) awe anapitia hesabu za mashirika na taasisi hizi zinazonufaika na misamaha hii (kama baadhi ya wadau wanavyopendekeza) na kama itabainika kuna ubadhirifu basi watakaobainika wafutiwe misamaha na kufikishwa kortini kwa uhujumu wa uchumi.

Ifike mahali Wizara nyeti kama Ujenzi, Afya, Elimu, Kilimo, Maji n.k bajeti zake ziwe zinajitosheleza na mipango yake kukamilika ili kupunguza umasikini kwa watu wetu na kufungua fursa zaidi za wananchi kujiimarisha kiuchumi na kijamii.

Binafsi naamini kama tutajipanga kikamilifu, na tukawa na viongozi makini wenye utu na uzalendo kwa taifa hili ni wazi kuwa tunaweza kutumia vema fursa tulizonazo kujiletea maendeleo na kupunguza utegemezi kwa misaada ya wahisani ambayokwayo imekuwa ikitugharimu kila mara na kutofikia malengo yetu

PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA: ACHUKUA KADI YA CHAMA HICHO MJINI DODOMA..


Msanii wa muziki wa kizazi kipya chini Tanzania maarufu kama "bongo flavor" Josef Haule (prf. Jay) amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kukabidhiwa kadi ya chama hicho na Msaii mwenzake wa muziki huo na mbunge wa mbea mjini kupitia chama hicho Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama MR. Sugu.

MATOKEO KIDATO CHA SITA: SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYAKIMYA

MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.

“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha. Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa. Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho.

“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21.

Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani.

Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.”

Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.”

Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.”

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali.

Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361.

Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012.

Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao.

Source Gazeti la Raia Mwema.