Friday, November 1, 2013
MGOMO WA MADAKTARI WALIOKO MAFUNZONI WANUKIA: BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA AFYA, Mh.Dr. Hussein Mwinyi
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA AFYA,
Mh.Dr. Hussein Mwinyi
Mh.Dr. Hussein Mwinyi
Wakati wenzetu wa Muhimbili wanalipwa 100%,yaani 1,225,000/= kwa madaktari na 994,000/= kwa wafamasia,sisi wa mikoani na nje ya Muhimbili tunalipwa 80% yaani 980,000/= kwa madaktari na 795,200/= kwa wafamasia.Tumejaribu kufuatilia tofauti hiyo kuanzia mwezi julai lakini hatujapata jibu linaloeleweka kwani ilidaiwa kwamba kulikuwa na makosa ya kiutendaji yalifanyika lakini kwa bahati mbaya mpaka leo tunakuandikia barua hii bado tatizo hilo linaendelea.
Kwa barua hii,tunaomba majibu yaliyokamilika na sahihi kutoka kwako Waziri wa Afya na kwamba tunajiandaa kugoma endapo ufumbuzi wa tatizo hilo hautafanyika kwa wakati kwa sababu hatua ya kutofautisha malipo siyo tu ya unyanyasaji lakini pia ni ya kibaguzi na inavunja katiba yetu ya nchi.Ni matumaini yetu kwamba madai haya yatafanyiwa kazi ipasavyo na hatimaye kupewa stahiki zetu kama ilivyo kwa wenzetu wa Muhimbili.
NAKALA· Chama cha madakatari Tanzania· Baraza la Famasi· Gazeti la Mwananchi· IPP media· Freemedia Group · Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Dar es salaam-Kinshasa Railway lazima ijengwe
Siasa ni mfumo wa kiuchumi ambso utawainua wananchi husika.
Siasa ya Tanzania kwa nchi za nje kwa miska mingi imekuwa ya ukombozi, ukombozi wa mwafrika toka tawala za kikandamizi za kikoloni.
Hivi karibuni Tanzania imejikuta katika sakata la kuitetea Kongo na wananchi wake walioko mashariki mwa Kongo.
Wananchi hawa kwa miaka mingi wamekuwa katika mlolongo wa matatizo ya kukosa amani na ustawi wa jamii.
Umoja wa mataifa umejaribu kwa miongo mingi tu kuleta amani bila mafanikio.
Lakini ni katika jaribio la mwisho hili la kutumia nguvu kwa kuwashirikisha majirani wa Kongo wenye nia ya dhati kuisaidia, sasa tunaona amani yaweza kurejea mashariki ya Kongo.
Ni wazi kuwaTanzania haina chake ndani ya Afrika Mashariki kutokana na hatua za wazi za kutengwa na majirani zetu wa kaskazini.
Lakini akufungiaye njia anakuonyesha mlango mzuri zaidi , hata ni kama wa kuufanyia kazi zaidi.
Ni vema sasa watanzania tukaweka mguu ndani ya Kongo, mguu wa kibiashara, mguu ambao hautaondolewa na tsifa lolote..
Ni muhimu sasa wananchi wa Kongo na Tanzania tukawa wamoja na kuendeleza spirit ya Goma, spirit ya ushirikiano kibiashara sasa.
Kilichobaki ni kuendeleza reli ya kati hadi Kigoma. Na kuanzisha rail ferries hadi mashariki mwa Kongo na kushinikiza wenzetu wa Kongo ku ifungua nchi yao kwa kujenga reli hadi Kinshasa.
Utajiri mkubwa wa Kongo na Tanzania utakuwa kichocheo kikubwa sana katika kujenga reli hii.
I have a dream!!!
CHANZO: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/
Subscribe to:
Comments (Atom)