Treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar Es Salam kuelekea mkoani Kigoma imepata ajali saa 9 usiku wa kuamkia leo 28 March 2014 na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wawili hawajulikani walipo na wengine sita kujeruhiwa
Ajali hiyo imetokea karibu na stesheni ya Gulwe iliyoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kusombwa kwa kipande cha njia ya reli na hatimae mabehea matano kuanguka.
Akithibitisha ajali hiyo katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dr. Shaaban Mwinjaka amesema mafuriko hayo yalikuwa na mawimbi makubwa ya zaidi ya mita 4 kwenda juu yaliweza kukitupa umbali wa mita mia moja kichwa cha treni chenye uzito wa tani 80.
Dr. Mwinjaka amesema kwa sasa wanafanya taratibu za kukiondoa kichwa hicho na kurekebisha miundombinu iliyoharibika ili mabehewa ambayo hayakuanguka yaweze kuendelea na safari
No comments:
Post a Comment