Post by Butije Butije H.
Sunday, March 30, 2014
Friday, March 28, 2014
TRENI YA MIZIGO YAPATA AJALI WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA
Treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar Es Salam kuelekea mkoani Kigoma imepata ajali saa 9 usiku wa kuamkia leo 28 March 2014 na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wawili hawajulikani walipo na wengine sita kujeruhiwa
Ajali hiyo imetokea karibu na stesheni ya Gulwe iliyoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kusombwa kwa kipande cha njia ya reli na hatimae mabehea matano kuanguka.
Akithibitisha ajali hiyo katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dr. Shaaban Mwinjaka amesema mafuriko hayo yalikuwa na mawimbi makubwa ya zaidi ya mita 4 kwenda juu yaliweza kukitupa umbali wa mita mia moja kichwa cha treni chenye uzito wa tani 80.
Dr. Mwinjaka amesema kwa sasa wanafanya taratibu za kukiondoa kichwa hicho na kurekebisha miundombinu iliyoharibika ili mabehewa ambayo hayakuanguka yaweze kuendelea na safari
Thursday, March 27, 2014
VIONGOZI WA KAMATI 12 ZA BUNGE MAALUMU LA KATIBA
Kamati ya Uandishi
Mwenyekiti - Mhe. Andrew Chenge,
Makamu Mwenyekiti- Mgeni Hassan Juma.
Kamati ya Kanuni
Mwenyekiti- Pandu Ameri Kificho
Makamu Mwenyekiti- Dkt. Susan Kolimba.
Mwenyekiti- Ummy Ally Mwalimu
Makamu Mwenyekiti- Prof. Makame Mbalawa
Kamati Na. 2
Mwenyekiti- Shamsi Vuai Nahodha
Makamu Mwenyekitini Shamsa Mwangunga
Kamati Na. 3
Mwenyekiti- Dkt. Francis Michael
Kamati Na. 4
Mwenyekiti- Christopher Ole-Sendeka
Makamu wake Dkt. Sira Ubwa Mamboya
Kamati Na. 5
Mwenyekiti- Hamad Rashid Mohamed
Makamu Mwenyekiti- Assumpter Mshama.
Mwenyekiti- Stephen Wassira
Makamu Mwenyekiti- Dkt. Maua Daftari
Kamati Na. 7
Mwenyekiti Brig. Hassan Ngwilizi
Makamu Mwenyekiti- Waride BakariJabu
Kamati Na. 8
Mwenyekiti- Job Ndugai
Kamati Na. 9
Mwenyekiti- Hamidi Saleh
Makamu Mwenyekiti- Wiliam Ngeleja
Kamati Na. 10
Mwenyekiti- Anna Abdallah
Kamati Na. 11
Mwenyekiti- Anne Malecela
Makamu Mwenyekiti- Hamad Masauni
Kamati Na. 12
Mwenyekiti- Paul Kimiti
Makamu Mwenyekiti- Thuwaybah E. Kisasi.
Aidha, kwa uchaguzi huo, Mhe. Sitta alitangaza wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ambao ni wenyekiti wote wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua kwa mujibu wa Kanuni.
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati ya Uongozi ni
- Fakharia Khamisi Shomari
- Mary Chatanda
- Profesa Ibrahim Lipumba
- Amon Mpanju
- Hamoud Abuu Juma.
Baada ya Mh. Sitta kutangaza uteuzi wake Profesa Lipumba alisimama na kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kufanya nafasi za uteuzi kuwa nne badala ya Tano .
MAALIM SEIF: HATUKO TAYARI KUJADILI SERIKALI MBILI
- Zanzibar itaendelea kuwa nchi
- watatumia kura ya maoni kuwahoji wananchi
Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake cha CUF hakiko tayari kujadili mfumo wa Muungano wa serikali mbili kama inavyotetewa na wabunge wa CCM na Rais Jakaya Kikwete.
Amesema tayari amewaandikia barua Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwaeleza juu ya msimamo huo.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.
Alisema CUF imebaini kuwa kuna njama za kufuta kipengele katika Katiba ya Zanzibar kinachosema; “Zanzibar ni nchi” na kwamba hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa Wazanzibari kamwe hawatakubali kufanya hivyo.
Maalim Seif alisema haikuwa mwafaka kwa Rais Kikwete kukosoa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba yanayotaka mfumo wa Muungano kuwa wa serikali tatu.
Alisema Jaji Warioba aliweka kando itikadi yake ya CCM katika utendaji wake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuja na uamuzi huo kwa vile ndiyo tiba ya kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Mapendekezo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi, Tanganyika imevaa koti la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga mwafaka katika kuendeleza Muungano wenye mfumo wa serikali tatu,” alisema Maalim Seif.
Alisema Muungano wa serikali mbili hauvumiliki na kama kuna watu wanaendelea kuutetea mfumo huo, Zanzibar inaweza kutumia sheria yake ya kura ya maoni kuwauliza wananchi wanaotaka na wasiotaka jambo hilo.
Wednesday, March 26, 2014
Ya Zitto na CHADEMA Hayakuanza Leo wa Jana, Mgogoro Ulianza Hata Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010
“Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana,” imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.
Fuatilia makala hii iliyochapishwa na gazeti lililotupwa korokoroni la MWANAHALISI
Siri za Zitto nje
- Mawasiliano yake yanaswa
- Aponzwa na mwandishi wa habari
Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009
Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.
SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.
CCM wanasikilizwa, CHADEMA wanaheshimika
Katika pitapita yangu nikakutana na makala hii iliyochapishwa katika gazeti lililotupwa korokoroni la MWANAHALISI.
Nilipo isoma makala hii nikajiuliza kwenye Bunge hili Maalumu la Katiba lenye viroja, mazingaombwe na matukio ya aibu kwa baadhi ya waheshimiwa ni nani anaesikilizwa na nani anaeheshimiwa?
Viroja vinavyoendelea katika Bunge hilo imepelekea baadhi ya wananchi kujenga shaka juu ya hatma ya upatikanaji wa katiba itakayokuwa kwa maslahi na ustawi wa wananchi na kwa Tanzania yetu tuitakayo.
Embu jikumbushe makala hii hapa chini>>>>
- MWENENDO WABUNGE WETU
MKUTANO wa Bunge la bajeti unaendelea mjini Dodoma, pamoja na kwamba wananchi wengi wamekatishwa tamaa na mwenendo wa serikali, lakini bado wanaendelea kufuatilia mjadala wake.
Na kwa kadri siku zinavyosonga mbele, ndivyo watu wengi wanaelekea kujenga msimamo juu ya mwenendo wa bunge hili.
Tuesday, March 25, 2014
SIMBA NA MAMBA WAZICHAPA KUGOMBEA MZOGA WA KIBOKO
Ni jambo la nadra sana kuona wanyama wanaosifika kwa kuwala wenzao mbugani kuonekana wakipambana, katika picha hizi zilizopigwa na mtaalam wa masuala ya teknolojia kutoka San Francisco nchini Marekani, Richard Chew aliyekuwa kwenye mapumziko na mke wake kwenye mbuga ya Maasai Mara iliyopo Kenya aliweza kunasa tukio la mamba akipambana na Simba mwenye njaa wakigombea mzoga wa kiboko aliyekufa A
ANGALIA PICHA ZAIDI
RAIS KIKWETE AVUNJA RASMI TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Na Butije Hamis- Dar Es Salam
Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza rasmi kuivunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na jani Joseph Sinde Warioba.
Tume ya mabadiliko ya katiba iliundwa na Rais Kikwete kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.
Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum la katiba Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.
BOFYA HAPA CHINI KUPATA TANGAZO HILO
VPL Kesho Azam Na Yanga Kusaka Alama Muhimu.
Klabu za Azam na Yanga ambazo zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania alama tatu.
Azam yenye alama 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama 19.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina alama 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).
Azam yenye alama 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama 19.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina alama 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).
WATU 176 WAPOTEA BAADA YA MAPOROMOKO MAREKANI
Maafisa wa utawala katika jimbo la Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.
Waokozi wangali wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura kwa kutumia helikopta na miale ya Laser.
Lakini maafisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata manusura.
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maafisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.
RC MARA BW. JOHN GABIEL TUPPA AMEFARIKI DUNIA
MKUU wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa, amefariki dunia ghafla leo majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa wilaya ya Tarime mkoani Mara
Katibu tawala wa mkoa wa Mara, Bw. Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya kifo chake leo asubuhi akiwa na afya njema alifika katika ofisi ya za mkoa na kumuaga kuwa anakwenda kufunga mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime.
Amesema kuwa muda mfupi baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, alipatwa na tatizo la ugonjwa huo na muda mfupi alikimbizwa hospitali ya Tarime lakini alifariki wakati akipatiwa matibabu.
Katibu tawala huyo amesema mwili wa marehemu unasafarishwa kutoka Tarime kuja hospitali ya Musoma kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali yakisubiriwa kutolewa.
Monday, March 24, 2014
Sunday, March 23, 2014
ZITTO KABWE: KAZI YA BUNGE NI KUBORESHA RASIMU ILIYOPO
Asisitiza tusijenge chi kwa kujibu malalamiko na hofu maana hofu na malalamiko
hayaishi katika dunia inayobadilika kwa kasi sana.
Aomba tuamue tunataka Muungano wa namna gani. Nini sababu ya Jamhuri yetu na aina gani ya Tanzania tunataka kujenga.
Moja, hotuba zote mbili zilichukua muda mrefu zaidi kuelezea sura moja tu ya Rasimu ya Katiba nayo ni sura ya Sita inayohusu muundo wa Jamhuri ya Muungano kana kwamba Katiba hii inahusu suala hilo tu.
Aomba tuamue tunataka Muungano wa namna gani. Nini sababu ya Jamhuri yetu na aina gani ya Tanzania tunataka kujenga.
Tuboreshe Rasimu iliyopo
Wiki ya Machi 18 - 22, 2014 ilianza kwa siku ya Jumanne Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwaslisha rasmi Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge Maalumu la Katiba.
Wiki ya Machi 18 - 22, 2014 ilianza kwa siku ya Jumanne Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwaslisha rasmi Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge Maalumu la Katiba.
Wiki hiyo imeishia kwa
siku ya Ijumaa Rais
wa Jamhuri ya Muungano ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kutoa hotuba kwa Bunge Maalumu.
Hotuba zote zimepokelewa kwa hisia tofauti kulingana na msimamo wa kila mtu kuhusu hoja inayoonekana
ni kubwa kuliko zote katika mchakato wa
kuandika Katiba Mpya - Muundo wa Muungano.
Wale wanashabikia muundo wa Serikali Tatu, walifurahishwa mno na hotuba ya
Jaji Warioba. Wale wanaoshabikia muundo wa Serikali mbili walifurahishwa mno na hotuba ya Rais Kikwete.
Sikufurahishwa na hotuba zote mbili. Nitaeleza.
Moja, hotuba zote mbili zilichukua muda mrefu zaidi kuelezea sura moja tu ya Rasimu ya Katiba nayo ni sura ya Sita inayohusu muundo wa Jamhuri ya Muungano kana kwamba Katiba hii inahusu suala hilo tu.
Ni dhahiri suala hili ni kubwa na muhimu kwani linahusu uhai
wa Dola yenyewe na siwezi kubeza. Hata hivyo
masuala kama Haki za Raia ni muhimu zaidi
kwani hata uwe na muundo wa namna gani wa muungano au hata muungano wenyewe kuvunjika, bila ya kuwa na haki za
msingi za raia kwenye katiba katiba hizo
zitakataliwa tu na wananchi.
Huu mtindo unaozuka wa
kudhani muundo wa muungano ndio mwarobaini wa matatizo ya
ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, umasikini, elimu ya hovyo, afya dhaifu, utatufikisha pabaya na hata kurudi tena kuandika katiba kudai haki hizo. Jaji Warioba na Rais Kikwete wameshindwa
kuruka kiunzi cha kwamba Katiba ni zaidi ya Muungano.
ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, umasikini, elimu ya hovyo, afya dhaifu, utatufikisha pabaya na hata kurudi tena kuandika katiba kudai haki hizo. Jaji Warioba na Rais Kikwete wameshindwa
kuruka kiunzi cha kwamba Katiba ni zaidi ya Muungano.
Pili, wote wawili Rais Kikwete na Jaji Warioba wamejenga hoja zao kuhusu miundo ya
Muungano wanayopendekeza au kuunga mkono kutokana na misingi ama ya 'malalamiko' au 'hofu'. Jaji Warioba
aliorodhesha malalamiko 11 ya upande wa
Zanzibar dhidi ya Muungano na malalamiko 10 ya
upande wa bara.
Kimsingi malalamiko yote ya upande wa bara yanazaliwa na
vitendo vya upande wa Zanzibar isipokuwa lalamiko namba vii linalohusu kupotea kwa utambulisho wa Tanganyika
katika muundo wa Muungano.
Jaji Warioba anajenga msingi wa pendekezo la Tume yake kutokana na kujibu
malalamiko au maarufu kero za Muungano na anasema "....muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa
hali ya sasa.
Muungano wa Serikali mbili waliotuchia waasisi siyo uliopo sasa...... waasisi
walituachia Muungano wa Nchi Moja yenye Serikali mbili, na siyo Nchi Mbili zenye Serikali Mbili". Nukuu hii
niliipenda kuliko
zote katika Hotuba ya Mzee wangu Warioba.
zote katika Hotuba ya Mzee wangu Warioba.
Rais Kikwete alijenga msingi wa maoni yake kwenye hofu za kuwa na Serikali tatu.
Hofu hizo ni pamoja na gharama za kuendesha Muungano, kuzuka kwa hisia za Utaifa wa Utanganyika na Uzanzibari, uwezekano
wa Muungano kuvunjika kwa kushindwa
kuhudumia majeshi na hata Jeshi
kuchukua Nchi ikipidi na kutupilia mbali katiba na Serikali ya Muungano kutokuwa na Rasilimali zake. Rais alisema 'Serikali ya Muungano ni egemezi na tegemezi' nukuu ambayo niliipenda kuliko zote
katika Hotuba ya Mzee wangu Jakaya Kikwete.
kuchukua Nchi ikipidi na kutupilia mbali katiba na Serikali ya Muungano kutokuwa na Rasilimali zake. Rais alisema 'Serikali ya Muungano ni egemezi na tegemezi' nukuu ambayo niliipenda kuliko zote
katika Hotuba ya Mzee wangu Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete hakuniridhisha kabisa namna ya kumaliza kero za Muungano kwa muundo uliopo
sasa kwani muundo huo umeshindwa kuzimaliza kwa takribani miaka 50 tangu Muungano uundwe. Haiwezekani
muundo uliozalisha kero lukuki ndio
utarajiwe kuzimaliza kero hizo. Kwa vyovyote
vile ni lazima kuwa na muundo mpya lakini kiukweli ni lazima muundo huo mpya ujibu hofu alizoeleza ndugu Rais maana ni
hofu zakweli.
Jaji Warioba hakuniridhisha na namna suala la Uraia litakavyotatuliwa kwani kutoa jibu
la kubakia na 'kukubali' Nchi mbili halafu uraia mmoja kunaleta mashaka makubwa. Kama tunataka kuwa na
Uraia mmoja ni lazima tuwe Nchi moja,
hatuwezi kuwa na Nchi mbili uraia mmoja.
Vilevile vyanzo vya mapato ya Muungano ni vidogo mno kuendesha dola. Hivyo basi rasimu
iliyopo mbele ya Bunge Maalumu ina mapungufu makubwa japo imetoa mapendekezo yatakayomaliza malalamiko ya
Muungano.
Sasa kazi ya Bunge ni moja tu nayo ni kuboresha rasimu iliyopo mbele yake ili kumaliza
kero za muungano zilizopo na kujibu hoja za hofu za muundo mpya.
Hakuna sababu ya kubishana kwenye takwimu za Tume, tume imefanya wajibu
wake na sasa Bunge Maalumu nalo litimize wajibu wake.
Iwapo kama kweli tunataka kusikia Watanzania wanataka nini kwenye muundo wa
Muungano, tusimamishe Bunge na twende tukawaulize kwa kura (referendum).
Vingivenyo tuboreshe rasimu iliyopo na iliyotokana na maoni ya wananchi
wote kwa kujibu hizo hofu muhimu alizoainisha ndugu Rais na hayo malalamiko muhimu yaliyoainishwa na Tume.
Sio kazi ya Bunge Maalumu kutafuta ubora wa hotuba zilizotolewa mbele
yetu bali kuona mazuri ndani ya hotuba hizo
yasaidie kazi yetu.
Tuzingatie kuwa tusijenge Nchi kwa kujibu malalamiko na hofu tu maana hofu na malalamiko
hayaishi katika dunia inayobadilika kwa kasi sana. Tuamue tunataka kuwa Jamhuri ya Muungano ya namna gani.
Nini sababu ya Jamhuri yetu na aina gani ya
Tanzania tunataka kujenga.
Tuanze kwa kutafsiri sababu
ya Tanzania kuwepo na Tanzania gani tunataka kujenga kisha tutunge Katiba itakayowezesha kutufikisha huko
tutakapo kufika.
Monday, March 17, 2014
AJIRA MPYA YA WALIMU WA PYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14
A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI I NATANGAZA ORODHA YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA IFUATAVYO:-
i. Wa limuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vyaualimu Tanzania Bara
.
B:Kila Mwalimu ( Ajirampya) atatakiwakuzingatiayafuatayo:-
1.Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwaajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
2.Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vyachuonaSekondari
3.Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi.
4.Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika Halmashauri waliko pangwa walimu. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa.
5.Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa Atena na atakuwa amepoteza ajira yake.
MAJINA YA WAAJIRIWA WAPYA
i. Wa limuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vyaualimu Tanzania Bara
.
B:Kila Mwalimu ( Ajirampya) atatakiwakuzingatiayafuatayo:-
1.Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwaajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
2.Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vyachuonaSekondari
3.Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi.
4.Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika Halmashauri waliko pangwa walimu. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa.
5.Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa Atena na atakuwa amepoteza ajira yake.
MAJINA YA WAAJIRIWA WAPYA
Wednesday, March 12, 2014
TATHMINI YA HALI YA UHALIFU MKOANI MBEYA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHIJESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Mbeya, Namba ya simu 2502572 S. L. P. 260,Fax - +255252503734 MBEYA.E-mail:- rpc.mbeya@tpf .go.tz
MKUTANO WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NA VYOMBO VYA
HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE 11.03.20
14.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Ahmed Z. Msangi
anatumia fursa hii kukutana na Waandishi wa Habari wa Mkoawa Mbeya kutoka Vyombo mbalimbali wa Habari ikiwa ni nafasi ya kutoatathmini ya Hali ya Uhalifu kwa Mkoa wa Mbeya pia kusikia maoni, ushauri nachangamoto mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari kwa lengo la kujenga nakuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA FEB-2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- 2014.1.
TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI
.Katika kipindi hicho cha
Feb
–
2014
jumla ya makosa
2,003
yaliripotiwa, wakati kipindikama hicho mwezi
Jan
–
2014
makosa
2,438
yaliripotiwa, hivyo kuna
pungufu
ya makosa
435
sawa na asilimia
18.2.
TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.
Katika kipindi hicho cha
Feb
–
2014
jumla ya makosa
makubwa 196
yaliripotiwa,wakati kipindi cha mwezi
Jan-2014
makosa
212
yaliripotiwa, hivyo kuna
pungufu
ya makosa
16
sawa na asilimia
8.3.
TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA ZA JESHI LAPOLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.
Aidha katika kipindi cha
Feb
–
2014
makosa makubwa yatokanayo na jitihada zaJeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali katika kufanya doria,misakona operesheni katika kupambana na uhalifu na wahalifu yaliripotiwa matukio
40,
wakati kipindimwezi
Jan- 2014
yaliripotiwa makosa
56
, hivyo kuna
pungufu
ya matukio
16,
sawa na asilimia
29.
4.
TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yoteyaliyoripotiwa katika kipindi cha
Feb
–
2014
yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheriaza usalama barabarani na usafirishaji ni
3,817
wakati kipindi mwezi
Jan- 2014
yaliripotiwa makosa
4,416
hivyo kuna
pungufu
ya makosa
599
sawa na asilimia
14.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)