Watu zaidi ya 285 wanaripotiwa kupoteza maisha kufuatia Kimbunga Bopha kusini mwa Ufilipino.
mamia ya watu wengine wameachwa bila makao kufuatia kimbunga hicho kikali katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.
Pwani ya Palawana katika eneo la Mindanao limeathiriwa vibaya na Kimbunga Bopha chenye upepo wenye kasi ya kilomita 120 hadi 150 kwa saa.
Waziri wa Mambo ya Ndani Ufilipino Manuel Roxas amesema zaidi ya watu 300 wametoweka kufuatia kimbunga hicho.
Uharibifu mkubwa unaokadiriwa kupindukia dola milioni 100 umeripotiwa katika sekta za kilimo na miundombinu katika jimbo la Compostela.
Ufilipino hukumbwa na vimbunga kila mwaka na aghalabu husababisha vifo na uharibifu mkubwa.
No comments:
Post a Comment