Monday, July 8, 2013
FIGO ZA MANDELA ZAACHA KUFANYA KAZI
IKIWA takribani mwezi mmoja sasa tangu Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, akimbizwe hospitalini akiwa mahututi kutokana na ugonjwa wa mapafu, taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa madaktari bingwa wanaomtibu, wamegundua ugonjwa mwingine mwilini mwake.
Nje ya Hospitali ya Medi Clinic iliyoko Pretoria, ambako waandishi wa habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani wamefurika wakifuatilia mwenendo wa afya ya Mandela, juzi na jana, zilivuja taarifa kuwa Mandela ambaye anaishi kwa msaada wa mashine maalumu inayomwezesha kupumua, madaktari wake wamebaini kuwa figo zake zimeshindwa kufanya kazi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, madaktari bingwa wanaomtibu wameanza kupambana na ugonjwa huo kwa kumuwekea mashine ya kusaidia figo zake kufanya kazi na kwamba wanaangalia uwezekano wa kuzibadilisha bila kusababisha madhara mengine katika mwili wake ambao sasa unalindwa dhidi ya magonjwa nyemelezi.
POLISI DAR WAPAMBANA NA WAMACHINGA
Mapambano kati ya Polisi na wafanyabiashara ndogondogo, maarufu Machinga, katika eneo la Manzese, yamesababisha uharibifu wa mali na kufungwa barabara, kusimamisha shughuli zote kwa zaidi ya saa tatu.
Hali hiyo ilitokea baada ya ‘Wamachinga’ ambao waliondolewa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa biashara wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini, kuamua kurejea kwa nguvu katika maeneo hayo.
Shughuli za kijamii na kibiashara katika eneo la Manzese, zilisimama kwa takriban saa tatu kutokana na eneo hilo kugeuka uwanja wa vita na usalama wa wananchi wasiokuwa na hatia kuwa shakani.
Awali polisi walitoa tangazo la kuwataka Machinga hao kuondoka katika eneo hilo agizo ambalo halikuwe za kukubaliwa, jambo lililosababisha kutumika kwa mabomu ya kutoa machozi.
Tukio hilo la Polisi kutumia mabomu hayo lilianza saa 7 mchana hadi saa 9.45, waliposimamisha kutumia mabomu ambayo yalikuwa yakifyatuliwa kuwatawanya Machinga hao.
Wakati Polisi wakizunguka kuwatawanya, machinga nao walikuwa wakiweka mawe na magurudumu ya magari barabarani kuhakikisha magari ya askari hao hayapati nafasi ya kupita.
Mitaa ya kuzunguka eneo hilo ambalo mara nyingi huwa na mkusanyiko wa watu, lilionekana kuwa wazi huku Polisi wakilitawala kwa kuzunguka huku na kule kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Mwananchi Jumapili lilishuhudia gari la polisi aina ya Land Rover likiwa limejaa wafanyabiashara hao waliokamatwa wakati wa kuwaondoa eneo hilo, ambalo ni kandokando ya barabara inayojengwa ya mabasi yaendayo kasi ya Strabag.
Baadhi ya wafanyabiashara wenye maduka, walijifungia ndani ya maduka yao kuepuka wizi ambao ungeweza kutokea.
Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya mali ambazo zimeharibiwa katima vurugu hizo pamoja na kuchomwa moto kwa jengo la tawi la Klabu ya Yanga eneo la Manzese.
Baada ya barabara kufungwa kwa mawe na wamachinga hao, hali hiyo ilisababisha foleni na usumbufu kwa wenye magari, waliokuwa wakitoka Ubungo kwenda Karikaoo na wale waliokuwa wakitoka Karikoo kwenda Ubungo iliwabidi kutumia njia za vichochoro kuepuka vurugu hizo.
Wakati polisi wakifyatua mabomu hayo, baadhi ya watu walikuwa wakikimbia ovyo huku watoto wakilia bila ya kupata msaada wa kuwaondoa katika eneo hilo.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
Monday, June 3, 2013
BODI YA MIKOPO YAWATAKA WANAFUNZI KUZINGATIA MUDA WA KUOMBA MIKOPO
Mkurugenzi wa mawasiliamo wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, alitoa kauli iyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kujaza fomu za maombi na kuwa siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni Juni 30 mwaka huu.
“Bodi inasisitiza kuanza mchakato wa kuomba mikopo kwa waliomaliza kidato cha sita na kuzingatia muda uliotolewa kujaza fomu za maombi na kuziwasilisha kwenye ofisi za bodi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo, Mwaisobwa alisema tayari waombaji 62,758 wamekamilisha taratibu za maombi ya mikopo na kujaza fomu stahiki, tangu utaratibu huo ulipozinduliwa rasmi Mei Mosi mwaka huu.
“Hadi sasa mchakato kwa waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na wanafunzi wanaoendelea na masomo unaendelea vizuri ambapo wengi wamejaza fomu kwa njia ya mtandao,” alifafanua.
Katika mwaka wa masomo wa 2012/13, bodi hiyo iliwapatia mikopo waombaji 94,703, ambao wako katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.
TUME YA KATIBA INATARAJIA KUZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA LEO
Watanzania wanasubiri kwa hamu kuona kama rasimu
hiyo itakuja na majibu ya maswali magumu, makubwa ya muundo wa Muungano,
madaraka ya Rais, uteuzi wa mawaziri kutokana na wabunge, muundo wa
wakuu wa mikoa/wilaya na muundo wa mihimili mingine miwili ya dola;
Mahakama na Bunge.
Uzinduzi wa rasimu hiyo unafanyika baada ya Tume
hiyo kufanyia kazi ya uchambuzi wa maoni ya wananchi. Maoni hayo
yalitolewa na wananchi wapatao 1,015,564 kwa njia mbalimbali ikiwa ni
pamoja na waliohudhuria mikutano ya moja kwa moja, waliotuma ujumbe
mfupi wa simu (sms), barua pepe na kutumia mitandao ya kijamii.
Idadi ya makundi yaliyotoa maoni ni 170 zikiwamo
asasi 22 za dini, kiraia 72, taasisi za Serikali 71, vyama vya siasa 19,
viongozi na watu mashuhuri 43 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Rasimu hiyo ndiyo itakayopelekwa kwenye Mabaraza
ya Katiba na itajadiliwa miezi mitatu ili kuona kama mapendekezo ya Tume
hiyo baada ya kuchambua maoni hayo ya wananchi yanafaa au yanahitaji
marekebisho.
Huo ni mwendelezo wa mchakato wa mabadiliko ya
Katiba ulioanza mwaka jana baada ya Rais Jakaya Kikwete kuteua wajumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuanza kukusanya maoni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam
jana na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid uzinduzi huo utaonyeshwa moja
kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) kuanzia saa nane mchana.
Taarifa hiyo iliwaomba wananchi kufuatilia
uzinduzi huo kwa umakini ili waweze kujua kinachoendelea. Kuzinduliwa
kwa rasimu hiyo kutaanzisha upya mjadala wa Katiba ambayo inatungwa kwa
mara ya sita.
Katiba iliwahi kutengenezwa mwaka 1961 wakati
Tanganyika ilipopata Uhuru, mwaka 1962 baada ya nchi kuwa Jamhuri, mwaka
1964 ilipoundwa Katiba ya Muda baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana
na mwaka 1965 ilitungwa Katika Mpya iliyodumu hadi mwaka 1977 baada ya
vyama vya Tanu na ASP kuungana na kuifanya nchi kuwa chini ya utawala wa
chama kimoja cha siasa.
Kwa upande wa Zanzibar kumekuwapo Katiba Tatu.
Kwanza ni ile ya Uhuru iliyotungwa mwaka 1963, Mwaka 1979 ikatungwa
Katiba nyingine na ya mwisho ni ile ya mwaka 1984.
Muundo wa Muungano
Kwa muda mrefu, suala la muundo wa Serikali mbili katika Muungano limekuwa mwiba katika siasa za Tanzania Bara na Zanzibar.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
Friday, May 31, 2013
CHADEMA, CUF WAOMBA RADHI KUFUATIA VURUGU ZA JANA BUNGENI
Chama cha CUF na Chadema vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF chenye mrengo wa Kiliberali na Chadema kimefanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni ushoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo.
MATOKEO YA KIDATO CHA 6 YATANGAZWA HUKU UFAULU UKIONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA JANA
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita huku ufaulu ukiongezeka kulinganisha na mwaka jana. Shule ya Marian Girls imeendelea kuongoza kwa kushika namba moja ikifuatiwa na shule ya Mzumbe.
Kwa matokeo kamli bofya hapa
MATOKEO YA KIDATO CHA 6 2013
Thursday, May 30, 2013
MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA 4 2012
Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Mh. Shukuru Kawambwa ametangaza matokeo mapya ya kidato cha nne 2012. Kwa taarifa kamili bofya hapa chini.
MATOKEO MAPYA KIDATO CHA 4 2013
MATOKEO MAPYA KIDATO CHA 4 2013
Tuesday, May 21, 2013
CHANGUDOA: WABUNGE NDIO WATEJA WETU, WANAFUNZI WA VYUO NA RAIA WA NJE WAVAMIA BIASHARA YAO
WAKATI Serikali ikitafuta kila njia ya kukomesha biashara ya ngono, hali imezidi kuwa tete jijini Dodoma baada ya kundi la makahaba kutoka ndani na nje ya nchi kupiga kambi katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Dodoma wafanyabiashara hao walidai kwamba biashara yao imevamiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.
"Wanafunzi wamevamia wateja wetu, ambayo wengi wao ni wabunge, na tumekuwa na wakati mgumu kwa sababu wanafunzi hao wanamvuto zaidi kutoka na umri wao kuwa mdogo,maumbile mazuri zaidi yetu, ingawa gharama zao ni kubwa kuliko gharama zetu, lakini bado wanatuzidi ujanja"alisema mama wa makamo anayesomesha watoto wake kwa kutumia biashara hiyo.
Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mariam (35) alidai kwamba awali alikuwa akifanya biashara hiyo jijini Dar es Salaam na kituo chake kikuu ilikuwa ni Kinondoni Makaburini na alilazimika kuhamia mjini Dodoma miaka miwili iliyopita na kupata mafanikio makubwa kupitia biashara hiyo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa umebaini maeneo ambayo yana wasichana wengi ambao ni makahaba ni Chako Nichako, Double H na Mtaa wa Uhindini ambako kuna nyumba maarufu kwa kufanya biashara hiyo haramu ya ngono.
Kahaba mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Anastazia (20) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) alisema kwamba viwango vyake ni kati ya sh 200,000 kwa tendo moja bila kulala sh 300,000 kwa mchepuo mmoja wakati wa kulala na akitaka michepuo miwili na zaidi ni tsh 400,000 hadi 500,000 wakati wale wamama wakubwa wanajiuza kwa tsh 30,000 hadi 50,000 tendo moja.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi alishatangaza kuwawinda na kuwatia kwenye mikono ya sheria wale wanaojihusisha na biashara hiyo haramu. Hata hivyo, kauli hiyo inaonekana kukosa mashiko kwani biashara hiyo inazidi kushamiri siku hadi siku.
CHANZO: http://habarimpya.com
MISAMAHA YA KODI NI JANGA KWA MUSTAKABALI WETU KAMA TAIFA
Misamaha ya kodi imefikia Tsh 1.8 Trilioni kwa mwaka, hizi ni fedha nyingi sana endapo kama zingetumika vema katika miradi ya kimaendeleo. Jana Dr John Pombe Magufuli amesoma bajeti ya Wizara ya Ujenzi yenye jumla ya Tsh 1.2 Trilioni (hivyo misamaha ya kodi ni 150% ya bajeti ya Ujenzi kwa mwaka 2013/14, pia ni 300% ya Bajeti ya Wizara ya Maji 2013/14). Ni nani hasa anayesamehewa matrilioni haya na kwa manufaa gani kwa umma wetu?
Ipo haja sasa tukawa na mfumo makini wa kuchunguza ni kina nani? kwa shughuli zipi? zenye tija gani na umma wanastahili kupewa misamaha hii ya kodi? Inawezekana tukaendelea kulialia kuwa nchi yetu ni masikini lakini tunasahau kuwa huwenda umasikini wetu ni "ukosefu wa viongozi makini" ambao wanaweza kusimamia vema mapato ya nchi na kupanga mipango ya kimaendeleo.
Nakumbuka mwaka 2009 (kama sijakosea) Serikali kwa ushauri wa TRA iliridhia kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija kwa mashirika, makampuni na taasisi za kidini ili kuongeza ukusanyaji mapato na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya fursa ya misamaha ya kodi. Kila mmoja anakumbuka taasisi za dini ndizo zilikuja juu na kumlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufuta uamuzi wa Serikali ambao ulikuwa umepokelewa kwa mikono miwili na wana taifa hili.
Kama mipango ya Ujenzi wa miundombinu aliyotusomea Dr Magufuli haitakamilika kwa kisingizio cha kuwa na nakisi ya bajeti, kama miradi ya maji mijini na vivijini haitakamilika kwa kisingizio cha nakisi ya bajeti ni wazi kuwa taifa hili tunaongozwa na watu wasio makini na maisha ya watanzania wenziwao, na kwa mnasaba huo viongozi hao watakuwa wamethibitisha kushindwa kwao kiuongozi na wajibu wa wanataifa hili ni kuwachukulia hatua stahiki muda ukiwadia.
Pamoja na hayo ni wakati sasa wa kujua ni kina nani wanaonufaika na misamaha hii ya kodi? Tunakumbuka ripoti ya TRA ilibaini kuwa watu/makampuni/mashiriki/taasisi za dini wanajinufaisha sana na kujineemesha kutokana na misamaha hii ya kodi. LAZIMA tuwe na mfumo maalumu wa kuzifuatilia fedha hizi ili kama zina manufaa yaonekane kuleta athari kwa jamii na pia shughuli za taasisi na mashirika hayo ziwe zinafanyiwa ukaguzi kubaini uhalisia wake badala ya kuyaacha mambo kujiendesha kihobelahobela.
Kama itaonekana inafaa ni vema Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) awe anapitia hesabu za mashirika na taasisi hizi zinazonufaika na misamaha hii (kama baadhi ya wadau wanavyopendekeza) na kama itabainika kuna ubadhirifu basi watakaobainika wafutiwe misamaha na kufikishwa kortini kwa uhujumu wa uchumi.
Ifike mahali Wizara nyeti kama Ujenzi, Afya, Elimu, Kilimo, Maji n.k bajeti zake ziwe zinajitosheleza na mipango yake kukamilika ili kupunguza umasikini kwa watu wetu na kufungua fursa zaidi za wananchi kujiimarisha kiuchumi na kijamii.
Binafsi naamini kama tutajipanga kikamilifu, na tukawa na viongozi makini wenye utu na uzalendo kwa taifa hili ni wazi kuwa tunaweza kutumia vema fursa tulizonazo kujiletea maendeleo na kupunguza utegemezi kwa misaada ya wahisani ambayokwayo imekuwa ikitugharimu kila mara na kutofikia malengo yetu
PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA: ACHUKUA KADI YA CHAMA HICHO MJINI DODOMA..
Msanii wa muziki wa kizazi kipya chini Tanzania maarufu kama "bongo flavor" Josef Haule (prf. Jay) amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kukabidhiwa kadi ya chama hicho na Msaii mwenzake wa muziki huo na mbunge wa mbea mjini kupitia chama hicho Mh. Joseph Mbilinyi maarufu kama MR. Sugu.
MATOKEO KIDATO CHA SITA: SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYAKIMYA
MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita
waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza
kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si
uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani,
matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne,
2012.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.
“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha. Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa. Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho.
“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21.
Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani.
Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.”
Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.”
Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.”
Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali.
Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361.
Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012.
Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao.
Source Gazeti la Raia Mwema.

Wednesday, April 24, 2013
UGONJWA WA KIMETA WAINGIA NCHINI, WAUA MTU MMOJA
Ugonjwa wa kimeta umelipuka katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mifugo kadhaa. Kutokana
na hali hiyo, wakazi 386 katika kijiji cha Kibaoni kata ya Nanjara Reha
wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wamepatiwa chanjo kufuatia ugonjwa
huo.
Akizungumza
na NIPASHE, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo,
Judathadeus Mboya, alisema Aprili 5, mwaka huu katika Kata ya Nanjara
Reha ng’ombe mmoja wa Afisa Mtendaji wa kata ya Ubetu Kahe, Peter
Kavishe, aliugua na baada ya kuzidiwa mmiliki wake aliichinja na kuiuza
nyama kwa bei nafuu katika kijiwe kwa Mafungu.
Mboye alisema Aprili 15 mwaka huu, Ofisa huyo ambaye aliugua na
alizidiwa kutokana na ugonjwa wa kutokewa na malengelenge makubwa meusi
na kukimbizwa katika hospitali ya Huruma. Mboya alisema usiku wa
kuamkia Aprili 17, mwaka huu Kavishe alifariki dunia.
Mkurugenzi huyo lifafanua kuwa uongozi wa hospitali hiyo alipokuwa
amelazwa Kavishe, baada ya kuchukuwa vipimo walishindwa kuvibaini kwa
haraka na kuvipeleka katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na kubaini kuwa
ni ugonjwa wa kimeta.
“Siku hiyo ya tarehe 17, mgonjwa mwingine ambaye alikula nyama hiyo
alilazwa katika hospitali ya Huruma na bado anaendelea na matibabu,”
alisema Mboya na kuongeza:
“Halmashauri imejitahidi kutoa chanjo kwa watu waliokula nyama na
kufikia Aprili 20, mwaka huu watu waliopatiwa chanjo wamefikia 386.”
Hata hivyo, Mboya alisema hadi kufikia juzi idadi rasmi ya mifugo waliokufa kutokana na ugonjwa huo haikujulikana.
Naye Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Rombo, Frank Mwanri, alimtaja bakteria
ambaye huambukia ugonjwa huo kuwa ni Basilus anthrax na dalili za
ugonjwa huo ni mifugo kutoa damu isiyoganda katika maeneo yote yenye
uwazi. Mwanri aliongeza kuwa pia kimeta huenea kwa njia ya damu kwa
kushika damu au nyama ya mfugo ambao tayari umeathirika na ugonjwa huo.
Alisema chanjo kwa ajili ya mifugo ilitarajiwa kuanza rasmi jana
wilayani humo.
“Wananchi wote wilayani Rombo, chanjo itaanza rasmi kesho (jana), hivyo
tujitokeze kwa wingi ili kupata chanjo ya ugonjwa huu na kuepusha
madhara ambayo yanaweza kujitokeza na hata maafa kama tusipoangalia,”
alisema Mwanri.
CHANZO: NIPASHE
Saturday, April 20, 2013
TCU KUDAHILI DARASA LA SABA KUJIUNGA VYUO VIKUU
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo
2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la
saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi
ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na
Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani
mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu,
lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha
mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa
vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
SIFA ZINAZOTAKIWA
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya
Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk
Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa
habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo
bila tatizo.”
VIGEZO
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni
75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja
E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa
kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa
kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha
kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
CHANZO: Mwananchi Communications Ltd
CHANZO: Mwananchi Communications Ltd
Friday, April 19, 2013
TANGAZO LA KAZI- IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO YA JIJINI MWANZA INATANGAZA NAFASI 4 ZA KAZI,
1. AFISA UTAWALA, NAFASI 1
MUOMBAJ AWE NA ELIMU YA KIDATO CHA SITA AU CHUO, AWE NA
TAALUMA YA MAWASILIANO YA UMMA NA MWENYE UJUZI WA USIMAMIZI WA VYOMBO VYA
HABARI. UZOEFU KATIKA UTAWALA WA VYOMBO VYA HABARI MIAKA 2
2. AFISA MASOKO, NAFASI 1
MUOMBAJI AWE NA
TALUUMA YA BIASHARA/MAHUSIANO NA MASOKO NGAZI YA DIPLOMA NA KUENDELEA, AWE NA MOYO
NA ARI YA KUFANYA KAZI.
3. WATANGAZAJI, NAFASI 2
MUOMBAJI AWE MWANAUME NA AWE NA TAALUMA YA MAWASILIANO YA UMMA NA
UANDISHI WA HABARI, WAWE NA NGAZI YA ELIMU KUANZIA CHETI, DIPLOMA NA KUENDELEA. PIA MUOMBAJI AWE NA UWEZO WA KUZUNGUMZA KISWAHILI FASAHA.
MWISHO WA KUTUMA
MAOMBI NI 23 APRIL 2013. USAILI UTAFANYIKA TAREHE 25 APRIL 2013 SAA NNE ASUBUHI
JIJINI MWANZA.
MAOMBI YALIYOAMBATANISHWA NA VYETI NA CV YATUMWE KUPITIA
email: iqrafm100@gmail.com au juqusuta@yahoo.com KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIM 0752 231172/ 0717388503
Wednesday, April 17, 2013
SH 620 BILIONI DENI LA TAIFA LA TANZANIA HAZINA MAELEZO.
Kwa ufupi
DAR ES SALAAM.
WAKATI hali ya umaskini inaonekana kuendelea kuwasumbua Watanzania, hatua za dhati za kudhibiti mali za umma bado ni tatizo nchini, huku wananchi wakiongea wanavyojua juu ya sababu za Serikali kushindwa kuwachukulia hatua wanaotajwa kufanya ufisadi.
Mikopo zaidi yaja
Bajeti inaonyesha Serikali itakopa shilingi takribani trillioni tano katika mwaka huu wa fedha.
Pia katika wakati huo, Serikali itapata shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida.
Umaskini Tanzania, utajiri wa Malaysia
Wakati tunapata uhuru, tafiti zinaonyesha hapakuwa na tofauti kubwa hali ya uchumi wa Tanzania na nchi zingine kama Malaysia ambayo kwa sasa ni kati ya nchi za kuigwa Asia kwa uchumi imara.
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema
kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni
la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na
kupata majawabu stahiki.
http://www.mwananchi.co.tz| Waziri wa Fedha wa Tanzania kwa sasa, Dk. William MgimwaWaziri wa fedha |
WAKATI hali ya umaskini inaonekana kuendelea kuwasumbua Watanzania, hatua za dhati za kudhibiti mali za umma bado ni tatizo nchini, huku wananchi wakiongea wanavyojua juu ya sababu za Serikali kushindwa kuwachukulia hatua wanaotajwa kufanya ufisadi.
Wapo wananchi wanaofikiri kuwa huenda kuna vigogo
wanahusika na ufisadi ndio sababu wanashindwa kuchukua hatua maana kuna
msemo ‘mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenzake.
Aidha wapo wanaowaza kuwa huenda wapo vigogo wanaona fedha za wananchi zikiibwa hazina athari kwao kwa vile wanaendelea na maisha kama kawaida.
Aidha wapo wanaowaza kuwa huenda wapo vigogo wanaona fedha za wananchi zikiibwa hazina athari kwao kwa vile wanaendelea na maisha kama kawaida.
| aliyemaliza muda wake, Mustafa Mkulo. |
Wakati watu wanasema hayo, Serikali mara
kadhaa
kupitia viongozi wake mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, imekuwa ikisisitiza kuwa inafanya liwezalo kuboresha
maisha ya Watanzania na kupambana na wizi wa mali za umma.
CAG Ufisadi na viongozi
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 akionyesha kuwa kuna ufisadi wa kutisha katika akaunti ya Deni la Taifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 akionyesha kuwa kuna ufisadi wa kutisha katika akaunti ya Deni la Taifa.
Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 ukurasa wa 158
inaeleza “Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa
tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwapo kwa marekebisho ya deni ya Shilingi
619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya
kuridhisha”.
Katika Taarifa hiyo, CAG Deni la Taifa linazidi kukua, mwaka unaoishia Juni 2012 lilikua kwa asilimia 17 kutoka mwaka ulioishia Juni 2011.
Katika Taarifa hiyo, CAG Deni la Taifa linazidi kukua, mwaka unaoishia Juni 2012 lilikua kwa asilimia 17 kutoka mwaka ulioishia Juni 2011.
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema
kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni
la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na
kupata majawabu stahiki.
Mikopo zaidi yaja
Bajeti inaonyesha Serikali itakopa shilingi takribani trillioni tano katika mwaka huu wa fedha.
Pia katika wakati huo, Serikali itapata shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanabainisha kuwa
ni dhahiri sehemu ya mikopo ambayo Serikali inachukua sasa itakwenda
katika matumizi ya kawaida.
Umaskini Tanzania, utajiri wa Malaysia
Wakati tunapata uhuru, tafiti zinaonyesha hapakuwa na tofauti kubwa hali ya uchumi wa Tanzania na nchi zingine kama Malaysia ambayo kwa sasa ni kati ya nchi za kuigwa Asia kwa uchumi imara.
Mafanikio baina ya nchi kiuchumi yanatofautiana
kwa sababu za tofauti ya aina za taasisi walizoweka kwenye nchi husika,
sheria, kanuni na taratibu zinazoathiri uchumi walizotunga na namna ya
motisha walizoweka kwa ajili ya watu wao.
Kulingana na Takwimu za Benki ya Dunia mwaka jana,
uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 6.5 hadi 7, kiasi ambacho
kinaonekana kidogo mno.
Umaskini unaonekana kuwa mkubwa hasa maeneo ya
vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini hasa kwa wasio na kazi na wale
walio kwenye sekta isiyo rasmi, umaskini wao unaongezeka kwa kasi.
Subscribe to:
Comments (Atom)