
Mchezaji wa kiungo wa Arsenal na England amezusha
mjadala kuhusu matamshi yake kwamba Waingereza tu ndio waiwakilishe timu
ya soka ya England.
Jack Wilshere alikua akielezea msimamo wake
baada ya kijana wa Manchester United Adnan Januzaj kutajwa kwamba
anaweza kuichezea England ikiwa atatimiza masharti ya Fifa ya ukaazi wa
miaka 5 kwa kua bado hajaamua alichezee taifa gani.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 18, ana haki ya kuchezea Ubelgiji, Serbia, Albania na Uturuki.
Alipoulizwa kuhusu hilo , Wilshere alijibu: "Kuishi England kwa miaka mitano haikufanyi kua Muingereza."
Baadae akiandika katika mtandao wa jamii wa
Twitter alisema matamshi yake hayakumkusudia Januzaj.
"swali lilikua
wachezaji wageni waruhusiwe kuichezea England, na kwa maoni yangu
sidhani waruhusiwe. Yeye ni mchezaji hodari lakini si Muingereza."
No comments:
Post a Comment