Wednesday, April 24, 2013

UGONJWA WA KIMETA WAINGIA NCHINI, WAUA MTU MMOJA


Ugonjwa wa kimeta umelipuka katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mifugo kadhaa. Kutokana na hali hiyo, wakazi 386 katika kijiji cha Kibaoni kata ya Nanjara Reha wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wamepatiwa chanjo kufuatia ugonjwa huo. 

Akizungumza na NIPASHE, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judathadeus Mboya, alisema Aprili 5, mwaka huu katika Kata ya Nanjara Reha ng’ombe mmoja wa Afisa Mtendaji wa kata ya Ubetu Kahe, Peter Kavishe, aliugua na baada ya kuzidiwa mmiliki wake aliichinja na kuiuza nyama kwa bei nafuu katika kijiwe kwa Mafungu.
Mboye alisema Aprili 15 mwaka huu, Ofisa huyo ambaye aliugua na alizidiwa kutokana na ugonjwa wa kutokewa na  malengelenge makubwa meusi na kukimbizwa katika hospitali ya Huruma. Mboya alisema usiku wa kuamkia Aprili 17, mwaka huu Kavishe alifariki dunia.
Mkurugenzi huyo lifafanua kuwa uongozi wa hospitali hiyo alipokuwa amelazwa Kavishe, baada ya kuchukuwa vipimo walishindwa kuvibaini kwa haraka na kuvipeleka katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na kubaini kuwa ni ugonjwa wa kimeta.
 “Siku hiyo ya tarehe 17, mgonjwa mwingine ambaye alikula nyama hiyo alilazwa katika hospitali ya Huruma na bado anaendelea na matibabu,” alisema Mboya na kuongeza:
“Halmashauri imejitahidi kutoa chanjo kwa watu waliokula nyama na kufikia Aprili 20, mwaka huu watu waliopatiwa chanjo wamefikia 386.”
Hata hivyo, Mboya alisema hadi kufikia juzi idadi rasmi ya mifugo waliokufa kutokana na ugonjwa huo haikujulikana. 
Naye Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Rombo, Frank Mwanri, alimtaja bakteria ambaye huambukia ugonjwa huo kuwa ni Basilus anthrax na dalili za ugonjwa huo ni mifugo kutoa damu isiyoganda katika maeneo yote yenye uwazi.  Mwanri aliongeza kuwa pia kimeta huenea kwa njia ya damu kwa kushika damu au nyama ya mfugo ambao tayari umeathirika na ugonjwa huo. Alisema chanjo kwa ajili ya mifugo ilitarajiwa kuanza rasmi jana wilayani humo.
“Wananchi wote wilayani Rombo, chanjo itaanza rasmi kesho (jana), hivyo tujitokeze kwa wingi ili kupata chanjo ya ugonjwa huu na kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza na hata maafa kama tusipoangalia,” alisema Mwanri.
CHANZO: NIPASHE

Saturday, April 20, 2013

TCU KUDAHILI DARASA LA SABA KUJIUNGA VYUO VIKUU


Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

SIFA ZINAZOTAKIWA
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”

VIGEZO
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.

CHANZO: Mwananchi Communications Ltd

Friday, April 19, 2013

TANGAZO LA KAZI- IQRA FM RADIO


IQRA FM RADIO YA JIJINI MWANZA INATANGAZA NAFASI 4 ZA KAZI,

1. AFISA UTAWALA, NAFASI 1

MUOMBAJ AWE NA ELIMU YA KIDATO CHA SITA AU CHUO, AWE NA TAALUMA YA MAWASILIANO YA UMMA NA MWENYE UJUZI WA USIMAMIZI WA VYOMBO VYA HABARI. UZOEFU KATIKA UTAWALA WA VYOMBO VYA HABARI MIAKA 2

2. AFISA MASOKO, NAFASI 1

 MUOMBAJI AWE NA TALUUMA YA BIASHARA/MAHUSIANO NA MASOKO NGAZI YA DIPLOMA NA KUENDELEA, AWE NA MOYO NA ARI YA KUFANYA KAZI.

 3. WATANGAZAJI, NAFASI 2

MUOMBAJI AWE MWANAUME NA AWE NA TAALUMA YA MAWASILIANO YA UMMA NA UANDISHI WA HABARI, WAWE NA NGAZI YA ELIMU KUANZIA CHETI, DIPLOMA NA KUENDELEA. PIA MUOMBAJI AWE NA UWEZO WA KUZUNGUMZA KISWAHILI FASAHA.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI 23 APRIL 2013. USAILI UTAFANYIKA TAREHE 25 APRIL 2013 SAA NNE ASUBUHI JIJINI MWANZA.

MAOMBI YALIYOAMBATANISHWA NA VYETI NA CV YATUMWE KUPITIA 
email: iqrafm100@gmail.com au juqusuta@yahoo.com  KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIM 0752 231172/ 0717388503

Wednesday, April 17, 2013

SH 620 BILIONI DENI LA TAIFA LA TANZANIA HAZINA MAELEZO.

Kwa ufupi
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki.
http://www.mwananchi.co.tz

Waziri wa Fedha wa Tanzania kwa sasa, Dk. William MgimwaWaziri wa fedha

DAR ES SALAAM. 
WAKATI hali ya umaskini inaonekana kuendelea kuwasumbua Watanzania, hatua za dhati za kudhibiti mali za umma bado ni tatizo nchini, huku wananchi wakiongea wanavyojua juu ya sababu za Serikali kushindwa kuwachukulia hatua wanaotajwa kufanya ufisadi.

Wapo wananchi wanaofikiri kuwa huenda kuna vigogo wanahusika na ufisadi ndio sababu wanashindwa kuchukua hatua maana kuna msemo ‘mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenzake. 

Aidha wapo wanaowaza kuwa huenda wapo vigogo wanaona fedha za wananchi zikiibwa hazina athari kwao kwa vile wanaendelea na maisha kama kawaida.
aliyemaliza muda wake, Mustafa Mkulo.


Wakati watu wanasema hayo, Serikali mara kadhaa kupitia viongozi wake mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, imekuwa ikisisitiza kuwa inafanya liwezalo kuboresha maisha ya Watanzania na kupambana na wizi wa mali za umma.


CAG Ufisadi na viongozi
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 akionyesha kuwa kuna ufisadi wa kutisha katika akaunti ya Deni la Taifa.

Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 ukurasa wa 158 inaeleza “Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwapo kwa marekebisho ya deni ya Shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha”.

Katika Taarifa hiyo, CAG Deni la Taifa linazidi kukua, mwaka unaoishia Juni 2012 lilikua kwa asilimia 17 kutoka mwaka ulioishia Juni 2011.

Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki.


Mikopo zaidi yaja
Bajeti inaonyesha Serikali itakopa shilingi takribani trillioni tano katika mwaka huu wa fedha. 


Pia katika wakati huo, Serikali itapata shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanabainisha kuwa ni dhahiri sehemu ya mikopo ambayo Serikali inachukua sasa itakwenda katika matumizi ya kawaida.


Umaskini Tanzania, utajiri wa Malaysia
Wakati tunapata uhuru, tafiti zinaonyesha hapakuwa na tofauti kubwa hali ya uchumi wa Tanzania na nchi zingine kama Malaysia ambayo kwa sasa ni kati ya nchi za kuigwa Asia kwa uchumi imara.

Mafanikio baina ya nchi kiuchumi yanatofautiana kwa sababu za tofauti ya aina za taasisi walizoweka kwenye nchi husika, sheria, kanuni na taratibu zinazoathiri uchumi walizotunga na namna ya motisha walizoweka kwa ajili ya watu wao.

Kulingana na Takwimu za Benki ya Dunia mwaka jana, uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 6.5 hadi 7, kiasi ambacho kinaonekana kidogo mno.

Umaskini unaonekana kuwa mkubwa hasa maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini hasa kwa wasio na kazi na wale walio kwenye sekta isiyo rasmi, umaskini wao unaongezeka kwa kasi.

TUNDU LISSU AZUA BALAA BUNGENI, TBC WAKATA MATANGAZO KUFICHA UKWELI


HALI imekuwa tete katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuamuru askari wa bunge kumwondoa nje ya Ukumbi wa Bunge,  Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu.

Hata hivyo Lissu pamoja na baadhi ya wabunge wa Chadema walisikika wakisema kwamba, hatoki mtu hapa, huku Ndugai akiendelea kusisitiza kwamba ili bunge liendelee ni lazima Lissu atoke kwanza.
Sababu kubwa iliyomfanya Ndugai amfukuze Lissu bungeni inatokana na hatua ya Lisssu kutaka kuzungumza, huku Naibu Spika akidai kwamba Lissu amezungumza mara nyingi tofauti na taratibu za bunge hilo.
Hata hivyo hatua hiyo iliendelea kwa zaidi ya dakika 15 kiasi cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lililokuwa likirusha matangazo hayo moja kwa moja kukata matangazo yake kwa dakika tano.
Hata hivyo walijaribu kurudi hewani hali ikawa bado inaendelea ndipo TBC ilipoamua katisha matangazo hayo mpaka kesho ili kukwepa kuonya hali ya hatari iliyokuwa ikiendelea katika bunge hilo mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

SOURCE: Habarimpya.com

UGUMU WA MASOMO, NA UKOSEFU WA FEDHA NI BAADHI YA SABABU ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUJINYONGA


Ubakaji, Ushirikina na matatizo ya kifamilia navyo vyachangia kujinyonga

“ Nafikiri ni wakati muhimu kuanzisha madarasa  maalum ya saikolojia,  ili kuwaweka sawa wanavyuo.  Nasema hivyo kwa sababu uamuzi wa kujiua ni sehemu  ya maradhi ya akili,’’anaeleza
Waandishi  Peltzer Karl na Paswana Nancy katika  kitabu chao, Suicidal behaviour among South African university students: Contributing factors, resources and prevention,  (Sababu na namna ya kuzuia vifo vya kujiua kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Kusini), wanataja sababu zinazochangia matukio ya kujiua kwa wanafunzi hususan wa  vyuo vikuu vya Afrika Kusini, ikiwamo ugumu wa masomo na masuala ya kijamii.

Sababu nyingine ni ukosefu wa fedha, matatizo ya kifamilia, imani za kishirikina, kubakwa, kuwa waathirika wa virusi vya Ukimwi, kufiwa na ndugu na jamaa, na tabia binafsi.
Aidha, kwa mujibu wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Afya (WHO), zaidi ya asilimia 90 ya vifo vya kujiua duniani vinatokana na matatizo ya akili kama vile kuwa na msongo wa mawazo,  unywaji pombe uliopitiliza na skizofrenia (magonjwa ya akili)

Ufumbuzi wa tatizo

 Taarifa nyingi zinaonyesha wanafunzi wa vyuo vikuu katika maeneo mbalimbali ni moja ya makundi mwathirika wa matukio ya kujiua. Bila shaka elimu, hamasa na misaada mbalimbali inatakiwa kutolewa vyuoni ili kulinda kundi hili muhimu katika jamii. 
Huduma za ushauri  hasa masuala ya kisaikolojia vyuoni hazina budi kuanzishwa,  kuimairishwa na kuwa rafiki ili kuvutia idadi kubwa ya wanafunzi wanaokabiliwa na matatizo husika.

Saturday, April 13, 2013

ARSENAL YAIBUKA NA USHIDI MNONO, LIVERPOOL YABANWA MBAVU


By Butije Hamisi
Timu ya Arsenal imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Norwich katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza. Mpaka dakika ya 84 Arsenal ilikuwa nyuma kwa bao 1 lililofungwa  na Michael Turner katika dakika ya 57. 
Arsenal ikicheza kwa kushambulia zaidi ilifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa kiungo wake Mikel Arteta kwa njia ya penalt katika dakika ya 85 baada ya mshambuliaji wake Olivier Girloud kuangushwa katika eneo la hatari. Bao la pili la Arsenal lilipatikana kwa Norwich kujifunga kupitia  Sébastien Bassong katika dakika ya 88 na bao la tatu lilpatikana kupitia Lukas Podolski katika dakika ya 90.

Kufuatia matokeo hayo Arsenal imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na point 59 nyuma ya Man City iliyoko nafasi ya pili kwa kuwa na point 65 na Man U iliyoko nafasi ya kwanza ikiwa na point 77

Matikeo ya mechi zingine ni Aston Villa 1 - 1 Fulham, Everton 2 - 0 Queens Park Rangers, Reading 0 - 0 Liverpool, Southampton 1 - 1 West Ham.

Tuesday, April 9, 2013

WATU 32 WAPOTEZA MAISHA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI IRAN


Jengo lililoharibiwa na zilizala eneo la Kaki kusini mwa Iran Aprili 9 2013

Tetemeko la ardhi  lenye nguvu ya 6.1 kwenye kipimo cha Richter limetikisa eneo la Kaki karibu mji wa Bushehr kusini mwa Iran. Shirika la Habari la Fars limesema  watu 32 wamepoteza maisha na wengine  850 kujeruhiwa katika tetemeko hilo.

Taasisi ya Kupimatetemeko ya  Iran imesema  tetemeko hilo limejiri leo Jumanne alasiri huko Kaki kilomita tisini kusini mwa Bushehr na kina chake kilikuwa kilomita 12 ndani ya ardhi. Pia limehisika katika nchi za Ghuba ya Uajemi za Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kituo cha Kuzalisha Nishati ya Nyuklia cha Bushehr hakikuharibiwa hata kidogo na tetemeko hilo. Shirika la Urusi la Atomstroyexport ambalo limejenga kituo hicho cha nyuklia limetoa taarifa na kusema kinu cha  nyuklia cha Bushehr kiko katika hali ya kawaida. Iran  iko katika eneo ambalo hukumbwa na mitetemeko ya ardhi mara kwa mara.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI-TEHRAN

UHURU KENYATTA AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA NNE KENYA.


  • Rais Kikwete amtaka Uhusu Kenyatta aingie Ikulu kama Rais na si kama mtoto aliyekulia Ikulu ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa sababu kukulia Ikulu ni tofauti na kuishi kama Rais wa nchi.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiejWThb2LRRGsTpS-30c9zNierakfYGadQQfBbkqg2U3aGm20qtvT1eMJIgMtwdWMo1BevfHn5CwCmY9uPDqHp2QWNNi0KR9zVbz_mo7Px4CE37EERo7K7f63xKzqoF-oEfJkBrWZ8NENn/s1600/164287_10151195580187609_1571565168_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivra0vJZQOpl2EBoRqDpzTlIn8_hHeyVL39lcKAW36yN1gzdnrN7fNm2-CcagdYga15iC8VUUSHr66x-xKrgs7XhnSTOUhZ-RpvbtO7-JQCpGW4rKFYwbFCWClcd8ltMZb7PcAyqk9pd3d/s1600/64844_10151195579017609_1383596097_n.jpgRais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHdUTXmhjcprqo1M-Fn9kuzyIeWyFnKTx0jFprvACI_3pFgQ3z6keldMdeOC4N8rs7ZVkivawuErV4gMLRSIGMS60EEy1E-BibVGb7cWBfnWum0amtu6pwH4dZknhpIb4dEjfi4qluUl7d/s1600/547497_10151195583982609_1581134814_n.jpgRais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi mbalimbali na watu mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEidXlo_5Lr4Z3blVAsy5Rt8ahqfIET6FcOPYi56m91eEsYUnZRGywZ0USXDWpaxyLFn42zFTLHth6pTUBKY4c_JnU_OVYAEWN8yRiE_dLNB1nJeku3ZsH7khQZqkZFUCx49XrRLFCsFQngM/s1600/529085_10151195578917609_1205076097_n.jpg
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgo-iBCuJDeVAGyTUymEahZpaf_jTe-K1E_la4P1jk5Zb6EiihWUZJxIKBFuFM1j5pb932ggmgnrU-pFZZTrzwA_yVbem6Z_A_l7BQ4Yd6q-4kIF6bzBo3Ul9TxBzAc6SFZFD5rAerkNP4W/s1600/11691_10151195578622609_363234948_n.jpg
Rais wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma hotuba yake fupi wakati wa kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWqL11shWRzEsfKalP06zZfbX1javNuFWVURsiXhPtc-gtIekUPathyicpUNSgiFW-s1765DmB1R15rUu56fuT3EkXRqnKTNKm4gyYTwJ_rI7RWvEtL3GNM_CFhycY6Jwga0f8Y696uJlc/s1600/524443_10151195579592609_804760154_n.jpg

Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo alisema kwamba suala la amani ya nchi hiyo ndiyo itakuwa ajenda ya kwanza katika utawala wake.
"Ndugu zangu wakenya, suala la amani ni suala muhimu sana, kulinda amani ya nchi ni ngumu kuliko kuzua vurugu mdani ya nchi,napenda kuwahakikishia kwamba amani itaendelea kutawala Kenya na kamwe sitapenda kuona mtu yoyote akijaribu kuivuruga amani yatu"alisema Rais Kenyatta.
Kuhusu suala la ajira nchini humo alisema,"Kazi ya pili itakayofuata ni kazi ya kuhakikisha kwamba watu wasiokuwa na ajira wanapata ajira ndani ya nchi kwani kwa kipindi kirefu wakenya wamekuwa wakikosa kazi huku wataalam mbalimbali wakitoka nje ya Kenya" , Kwa upande wake Makamu wa Rais William Ruto alisema kwamba huu ni muda wa kuwatumikia wakenya na hiyo ndiyo kazi iliyopo mbele yao.
Naye Rais wa Tanzania  Jakaya Kikwete akitoa salamu kwa niaba ya viongozi mbalimbali walioalikwa katika sherehe hizo alimtaka Kenyatta aingie Ikulu kama Rais na si kama mtoto aliyekulia Ikulu ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa sababu kukulia Ikulu ni tofauti na kuishi kama Rais wa nchi, huku pia akimwakikishia ushirikiano mkubwa katika jumuia ya Afrika Mashariki.

HAYA NDO NIMEYAONA YA MSINGI SANA KATIKA SPEECH YA KENYATA UHURU BAADA YA KUAPISHWA


By Denis Mpagaze
...'Today , work begins. The time has come, not to ask what community we come from but rather what dreams we share. 
The time has come not to ask what political party we belong to but rather what partnerships we can build. The time has come to ask , not who we voted for,but what future we are devoted to. 
Fellow Kenyans we must move forward together. Let us remember that although we may not be bound together by ethnicity, or cultural practices or religious conviction – our kinship rests solidly upon the fact that we 28 have all been adopted by Kenya’s borders;we are all children of this nation, we are all bound to one constitution which calls us to rise above our individual ideologies and march to our national anthem'......

Wednesday, April 3, 2013

VURUGU ZA KIDINI ZAIBUKA TUNDUMA, MSIKITI WACHOMWA MOTO


Mapigano makubwa yameibuka hii leo baina waislam na wakristo katika mji wa Tunduma Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya na kusababisha msikiti mmoja kuchomwa moto katika maeneo ya Mwaka na Kisiman

Vurugu hiyo iloyodumu takriban masa manne imeilazimu Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) kuingia mitaani na kupiga mabomu ya machozi kila mahali huku akitoa amri yakuwataka wananchi kuingia ndani na kulala mchana huu.
Chanzo cha virugu hizo inadaiwa kuwa imetokana na mzozo wa uchinjaji nyama ambao Rais Kikwete aliutole ufafanu na kusema kwamba burasa itumike katika kutatua mzozo huo.

Akizungumza  mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kwamba mbali na mabomu ya machozi kupigwa ovyo, barabara zimefung, maduka yamefungwa huku matairi yakicchomwa moto barabarani.

VIJANA HAWA WAFICHUA YALIYOFICHIKA CHADEMA,DR.SLAA APOROMOSHA MATUSI..SIRI YA KUMUUA ZITTO


Baadhi ya picha mbalimbali za matukio ya vurugu za kisiasa.
 
WANASIASA wawili vijana ambao wamekuwa katika vita ya maneno na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, kuhusu madai waliyoyatoa kuwa anawindwa kuuawa, mwishoni mwa wiki iliyopita, walijitokeza katika ofisi za Mtanzania Jumatano na kufunua siri na matukio ya utesaji raia na mauaji ya kinyama ambayo yamekuwa yakitokea kwa nyakati tofauti kwenye shughuli za kisiasa hapa nchini.

Wanasiasa hao, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, ambao wamefanya mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili, walisema madai waliyoyatoa awali kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alitajwa na kada wa chama hicho, Ben Saanane, kuwa alimtuma amuwekee sumu Zitto kwa lengo la kumuua ni ya kweli kwa sababu walimkamata akiwa nayo na alikiri jambo hilo na kumuomba msamaha Zitto kwa kitendo hicho.


Walidai, mbali na tukio hilo ambalo baada ya kuliibua limegusa hisia za wengi na kuzua mijadala mikali, yapo matukio mengine ya mauaji na majaribio ya kuua, ambayo yamekuwa yakiratibiwa na Chadema kwa lengo la kuwagombanisha wananchi na Serikali.

Shonza na Mwampamba walisema kuwa wapo tayari kutoa ushuhuda wa matukio hayo mahali popote watakapohitajika na walipoulizwa ni kwa nini baada ya kubaini kuwepo kwa vitendo hivyo, hawakutoa taarifa kwa vyombo vya sheria au taasisi za ulinzi na usalama, walisema mlengwa mkuu katika matukio hayo ambayo yalikuwa yakisababisha madhara kwa watu wengine hakuwa tayari siri hiyo kuanikwa.

Akizungumza mbele ya jopo la waandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Jumatano, Shonza alidai kuwa, yeye na baadhi ya vijana wenzake waliokuwa wakiunda kundi Patriotic Movement, walimnasa Saanane akiwa na sumu hiyo katika Hotel ya Lunch Time iliyoko Ubungo, Dar es Salaam, ambao awali alidai kuwa ni dawa ya Panya, lakini alipobanwa alieleza kuwa ilikuwa sumu ambayo hakuitaja jina na kwamba alipewa na Dk. Slaa ili amuwekee Zitto kwa sababu alikuwa akimsumbua sana.

Alisema, sumu ingewekwa kwenye kinywaji cha Zitto akiwa katika kikao hicho, lakini hatua yake ya kutohudhuria ndiyo iliyomuokoa. 

Shonza alisema, baada ya Saanane kukiri kuwa alitumwa na Dk. Slaa kumuwekea Zitto sumu, walimtaarifu wakati akiwa Marekani na aliporudi alikutana na kuwataka jambo hilo wasilifikishe polisi kwa sababu lingekivuruga chama na kwamba kwa sababu alikwishawajua wabaya wake atajilinda.

Alimtuhumu Zitto kwa kuficha ukweli na kumwita kiongozi mwoga, huku akimuonya kuwa iwapo ataendelea na tabia ya kukanusha ukweli atamuumbua hadharani kwa sababu anamjua vizuri.

“Ameongea hayo kwa sababu ana tabia ya kushindwa kuthibitisha kuwa ana uwezo wa kujiongoza yeye mwenyewe pamoja na wengine. Mtu wa maslahi Zitto, anatafuta huruma ya Chadema baada ya kuona amepukutika kisiasa kutokana na kukosa msimamo kiuongozi na hawezi tena kutetea wanyonge, ni mtu mwoga.

Mnapokuwa kwenye mapambano yeye yuko tayari kurudi nyuma, lakini huruma hiyo asitegemee kuipata Chadema, labda akubali kushaurika na kubadilika kama kweli anataka kutetea maslahi ya wanyonge,” alisema Shonza.

Aidha, Shonza alimshambulia pia Saanane kwa kudai anakataa ukweli anaojua, kwa sababu tukio la kukamatwa kwake akiwa na sumu lilitokea akiwa mbele ya zaidi ya mtu mmoja na kusisitiza kuwa kada huyo wa Chadema anatumika na viongozi wa juu wa chama hicho kuwashughulikia baadhi ya wanachama wasiotakiwa.

Katika hili, Shonza alidai zaidi kuwa Saanane ni mtu hatari kwa sababu ndiye aliyeanzisha kundi la PM7, ambalo lilikuwa na lengo la kumpindua Mbowe kutoka kwenye wadhfa wake wa uenyekiti, lakini baadaye aliwageuka wenzake na kusababisha kufukuzwa katika chama.

“Saanane alikuwa anatumika kutuingiza mkenge. Alianzisha kile alichokiita mapinduzi, Patriotic Movement (PM7), lengo lilikuwa Pindua Mbowe, sisi hatukujua.

Tulikuwa saba katika PM7, Saanane alifanikiwa kutuchezea akili na alikuja na 'nick names' (majina bandia) yake. Mimi akaniita Benanzir Bhuto, Mchange akaitwa Mdude, Mwampamba- Joseph Kony, Zitto- Dogo kama tulivyozoea kumuita na yeye mwenyewe akajiita Cobra, wapo na wengine sikumbuki vizuri majina yao hapa.

Sisi vijana wakati mwingine tunatumika vibaya, sisi hatukujua ana ajenda yake, tulivyoshtuka akatukana na ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea,” anazidi kueleza Shonza.
Mwampamba
Kwa upande wake Mwampamba ambaye aliandamana na Shonza katika ofisi za Mtanzania Jumatano, alidai kushangazwa na hatua ya Zitto kukanusha kauli ya Shonza iliyokuwa ikieleza namna Saanane alivyokamatwa akiwa na sumu aliyokuwa ametumwa kumuwekea Zitto.

Alisisitiza kuwa, Zitto anajua mipango inayopangwa ndani ya Chadema kwa ajili ya kummaliza na alimtaka aache tabia ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, kwa sababu inaweza kuwa na athari mbaya kwake.

“Zitto anajua mpango mzima wa kutaka kumalizwa kwa sumu na Ben Saanane, baada ya kutumwa na Dk. Slaa kwa sababu tulimwambia na alithibitisha mwenyewe pale Saanane alipomuomba msamaha, sisi ndiyo tulimbana Saanane hadi akaeleza ukweli wa mipango yao ya mauaji.

“Leo namshangaa anavyojikomba eti haamini kuwa anaweza kuuawa na hao jamaa. Lakini kwa Ben Saanane, namtaka atambue kuwa Ludovick alipokamatwa alikanwa na Dk. Slaa wakati ndiye alikuwa kijana wake mpenzi, sasa na yeye ipo siku atakimbiwa.

“Zitto anatakiwa aache tabia ya kufunika funika mambo, ajue nimemwokoa sana katika mambo mengi, mfano mauaji ya Morogoro yaliyopangwa na Chadema yalimlenga Zitto, alikuwa atolewe kafara. Yule muuza magazeti aliyepigwa risasi Morogoro akafa, siku hiyo ilikuwa afe Zitto,” alidai Mwampamba.

Alipoulizwa ni kwanini viongozi wa Chadema wanataka kumuua Zitto, alisema ni kwa sababu ya uhusiano mbaya baina yake na vigogo hao ambao chanzo chake ni hatua ya kutaka kugombea urais na kutomuunga mkono Dk. Slaa katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2010.

“Zitto hana uhusiano mzuri na viongozi wa juu wa Chadema. Nia yake ya kutaka kugombea urais hawaipendi, inawaudhi sana na amekuwa akitofautiana nao kwa mambo mengi, anajua kuwa anawindwa ndiyo maana hata oparesheni za M4C hashiriki.

“Mimi nilikuwa Chadema na nilikuwa karibu sana na Zitto, najua nini kilikuwa kinaendelea juu yake na najua baadhi ya mambo ya Chadema. Ninaijua mipango ya mauaji ya Chadema. Zitto aliwahi kuwekewa sumu Bagamoyo wakati wabunge wa chama hicho walipokuwa kwenye mkutano wao huko. 

“Alinusurika kufa. Alipona baada ya sumu hiyo kutolewa mwilini mwake. Waliiflashi.” Alidai Mwampamba. 

Alidai kuwa Zitto alipata kunusurika katika ajali ya gari wakati akitokea Bagamoyo kuelekea Iringa, baada ya gari alilokuwa akitumia kulegezwa nati zinazofunga tairi. Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya Zitto na Mbowe kutupiana maneno makali kwenye mkutano
Kauli ya Saanane
Akizungumza na Mtanzania Jumatano jana kupitia simu yake ya kiganjani, Saanane alisema madai yaliyotolewa na Shonza na Mwampamba dhidi yake siyo ya kweli, kwa sababu wanayodai kuwa walimkamata akiwa na sumu, hakuwa nao.

Alisema kwa mujibu wa kumbukumbu zake, siku ya Desemba 5, mwaka jana, alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akikutana na wanaharakati na baadaye jioni alikwenda harusini.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo alipata kukutana na Shonza na Mwampamba katika Hotel ya Lunch Time, Saanane alisema amepata kukutana nao mara kadhaa kwa ajili ya kupanga mikakati ya PM7, ambayo alishiriki kuianzisha lakini aliachana nao baada ya kubaini walikuwa wakiitumia kwa malengo mabaya.

Mtanzania Jumatano lilipombana Saanane aeleze mikakati waliyokuwa wakiipanga yeye na wenzake katika PM7, alisema ilikuwa ya siri na vikao vyao vilikuwa vya siri kutokana na hofu ya kufikiriwa vibaya na viongozi wa chama iwapo wangebainika wanajihusisha na kundi hilo.

Alipoulizwa kama anafahamiana na Zitto na wapi amekwishakutana naye, alisema anamfahamu na amekuwa akikutana mara kwa mara huku akishangaa tamko lake kwenye mitandao ya kijamii lilikokuwa likieleza kuwa, hamfahamu na hata akimuona anaweza kupishana naye.

Hata hivyo, baadaye Saanane aliomba anuani ya barua pepe ya Mhariri wa gazeti hili na kumtumia barua ya kumtaka amuombe radhi kwa kuandika habari ya uongo iliyokuwa ikieleza madai ya masharika wake wanaomuhusisha na tuhuma za kutumwa kumuwekea sumu Zitto, pasipo kumtafuta Zitto mwenyewe kuzungumza hata neno moja
Vituko vya Dk. Slaa
Dk. Slaa alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani na kuulizwa kuhusu madai hayo, alianza kuporomosha matusi mazito huku akilituhumu gazeti hili kutoa nafasi ya kuandika habari zinazowagusa viongozi wa Chadema badala ya kuandika habari za maendeleo.

“Sina muda wa kujibu maswali hayo… hayana msingi…tuhuma hizo hazijadiliwi kwenye magazeti……ni masuala ya kijinga…pumbavu kabisa. Acheni upumbavu bwana. Nina mambo mengi ya msingi ya kitaifa ya kushughulikia kuliko haya madai ya kipumbavu.” Aling’aka Dk. Slaa.

Hata gazeti hili lilipomsihi awe mtulivu ili aweze kutoa ushirikiano, aliendelea kufoka huku akiporomosha matusi zaidi kabla halijaagana naye na kukata simu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe simu yake iliita muda wote bila majibu na hata Zitto.
CHANZO: Gazeti la Mtanzania

Tuesday, April 2, 2013

KIJIJI CHAFUMULIWA BAADA YA KUDAIWA KUWA NA MISUKULE BAGAMOYO MKOANI PWANI


KWA WANAO AMINI MAMBO YA USHIRIKINA HALI NDIVYO ILIVYO HIVI KIJIJI CHA KIMANGE WILAYANI BAGAMOYO.Msukule.

Msukule.
Msukule.



Na Makongoro Oging'. BAGAMOYO.

INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.

Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
 
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000  hadi 250,000  kwa kila mtu.
Msukule.
Imegundulika kuwa viongozi hao wa dini  hufanya zoezi hilo kwa siri kubwa na kuna  nyumba ya mchungaji mmoja, nje kidogo ya kijiji hicho ambapo misukule hao feki  hupewa mafunzo ya nini cha kufanya kabla ya kusafirishwa kuelekea Dar es Saalam.

Imeelezwa kuwa misukule husafirishwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ‘tinted’ wakiwa wamepakwa matope mwili mzima  na kuvalishwa nguo zilizochanika.

“Wapo wachungaji waliofanya hivyo kwa kuwalaghai waumini wao kwamba wana uwezo wa kufufua watu huku wakijua kwamba lengo lao ni kuwavutia watu wajazane kwenye makanisa yao ili wapate  sadaka nyingi,” kilisema chanzo chetu.

 Uchunguzi  umebaini  kwamba  kuna makanisa  ambayo  yana wafuasi wengi wa kufanya mazingaombwe ya namna hiyo na wamekuwa wakijipatia fedha nyingi ambapo kwa Jumapili moja, hujikusanyia kati ya shilingi 7,000,000 hadi 7,500,000.

Aidha, ‘hukomba’ sadaka wakati wa maombi ya katikati ya wiki kwa kutumia mbinu mbalimbali za kuvuta waumini.

Baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao  waliwahi kurubuniwa na wachungaji baada ya kufuatwa kijijini hapo ni pamoja na Ziada Mlanga (33) na Shakila Ayubu (29).

Katika  mahojiano  na mwandishi wetu kijijini hapo, Ziada alikuwa na haya ya kusema:

“Machi 21, 2011 kaka mmoja (jina tunalihifadhi) anayeishi Kijiji cha Makore jirani na chetu, alinifuata na kunieleza kwamba anahitaji vijana wanne, wa kike  wawili na wa kiume wawili ili wajiunge katika shughuli za sanaa, yaani kuigiza.

“Hata hivyo, alifanikiwa kunipata mimi na Shakila, akatuahidi kutulipa shilingi 350,000 kila mmoja na wazazi wetu kupewa shilingi 100,000 kila mmoja.

“Tulikubali  kufanya hivyo, walituchukua kwa pikipiki hadi Kijiji cha Makore  nyumbani kwa mtu mmoja aliyemtaja kuwa ni mchungaji.

“Tulipofika huko walituweka katika chumba maalum katika nyumba ya huyo mchungaji  ambayo ipo porini, wakatueleza kwamba  tusubiri kuna watu wanakuja kutupa  mafunzo.

“Baada ya muda mfupi walifika watu ambao tulipoongea nao, walitueleza tuvue nguo zote tubaki na za ndani. 

Tulifanya hivyo, wakatupaka majivu, wakatuvuruga nywele  na kutuvalisha nguo chakavu na ilipofika saa moja usiku, walikuja watu wengine wakiwa kwenye gari yenye vioo vya tinted.

“Walitueleza kwamba tunaelekea jijini Dar es Salaam ambako tukifika tujifanye mazezeta. Tulifika usiku sana na kupelekwa katika kanisa moja (jina linahifadhiwa).

“Ndani ya gari lile kulikuwa na bastola, hatukujua ni ya nini, pale kanisani tulitengenezewa chai. Hata hivyo, tulikataa  kuinywa.

“Baadaye walitueleza kwamba wametufanya vile ili tuonekane kama watu  waliokuwa wamechukuliwa kimazingara na kufanywa misukule na sasa tumeokolewa na mchungaji wa kanisa hilo.

“Kesho yake ilikuwa Jumapili, tuliambiwa tutasimama mbele ya waumini kanisani na tusiseme kitu chochote ili tuje kuanza kuongea kidogo baada ya kuombewa na mchungaji.

 “Hata hivyo, tulipewa majina ya watu mashuhuri waliokufa lakini mimi nilikataa kwa kuwa aliyetajwa kuwa nijifanye ndiyo mimi alikuwa mtu maarufu.

 “Nilijiuliza ndugu zake wangenielewaje? Kitu cha pili ni kwamba nilikataa kwa kuwa fedha tulizokubaliana walikuwa hawajatupatia na tukaona kuwa huo ni udhalilishaji.

“Baada ya kuona tumekataa, walitusihi  tusitoe siri na baadaye tulipewa nguo  nyingine tukavaa na tukapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama nauli ya kurudia kijijini kwetu Kimange.

“Tulipofika tuliwaeleza wazazi wetu  mambo tuliyofanyiwa wakaona tumedhalilishwa, ikabidi tuje nao Dar es Salaam  tukaenda hadi Kituo cha Polisi  Magomeni na kufungua  kesi.

  “Tuliwaambia polisi kuwa simu na nguo zetu ziko kwa watu hao lakini hadi leo kesi tuliyofungua hatujui ilipofikia na tuliambiwa polisi wamewasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani.

“Polisi wa Pwani walikuja Dar na kutuchukua hadi Kibaha ambako tulitoa maelezo na tukaenda nao Kijiji cha Makore lakini  hatukumkuta mchungaji huyo, tukaambiwa kuwa alihama baada ya kupata habari kuwa anatafutwa na polisi,” alisema Ziada akiungwa mkono na Shakila.

BABA  WA  ZIADA
Baba wa Ziada aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Musini Mlanga, alisema kwamba kitendo walichofanyiwa watoto hao ni cha udhalilishaji na anaiomba serikali kuchukua hatua.

“Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo, huo ni utapeli na udhalilishaji mkubwa, hakuna dini  inayoweza kufanya mambo kama hayo, wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Mlanga.

MWENYEKITI  WA  KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimange, Juma Issa  Madinga amekiri kufahamu suala hilo na kukemea kitendo hicho.

“Hao wachungaji hawawezi kuachwa wakifanya mambo hayo na kusababisha kijiji kupakaziwa kuwa ni cha misukule, sasa wananchi wasilaghaiwe na matapeli hao, wakija tena watoe taarifa kwangu,” alisema  mwenyekiti huyo.

CHANZO: http://jumamtanda.blogspot.com