Friday, April 25, 2014

MAALIM SEIF; SIKUMMALIZA JUMBE.


NAIKUMBUKA KURA YA MAONI YA CCM YA MWAKA 1994 KUHUSU MUUNGANO

MJADALA wa Bunge Maalum la Katiba, hasa kuhusu muundo wa Muungano bado unavuta hisia za wengi kutokana na yanayozungumzwa.
Tunapoadhimisha miaka 50 ya Muungano huo, mambo mengi yanazidi kuelezwa, japo siyo mapya kwa vile yamekwishawahi kuelezwa katika Tume mbalimbali huko nyuma kama ya Jaji Robert Kisanga, Jaji Francis Nyalali na Jaji Joseph Warioba.

Mzee Warioba pia katika Tume ya Marekebisho ya Katiba aliwasilisha maoni kama yale yale, na safari hii yakiwa yametolewa mapendekezo lukuki ambayo kwayo ndiyo yaliyozaa mjadala mkubwa ndani ya Bunge Maalum.

Kubwa lililojitokeza ni kwa Wajumbe wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutamka hadharani kwamba wao wanataka muundo wa Muungano wa Serikali Mbili na siyo Tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Warioba.
Wengi wao wamekejeli hata takwimu zilizotumiwa na Tume hiyo kwamba siyo sahihi na hazibebi mawazo ya Watanzania wote ambao kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 wamefikia milioni 44.

Tuesday, April 22, 2014

BUTIJE: KIGOMA NI NYUMBANI WE HAVE TO RETURN TO


Tuesday, April 8, 2014

Siku 100 za mauaji ya Rwanda- 1994

ALLAH Ibariki Nchi Yetu 

Picha za watu waliouawa katika mauaji ya Rwanda mwaka 1994
Katika siku miamoja mnamo mwaka 1994, watu 800,000 waliuawa kinyama nchini Rwanda. Mauji hayo yalifanywa na wahutu wenye msimamo mkali.
Walikuwa wanawalenga watutsi waliokuwa wachache pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.

Kwa nini wahutu waliwaua watutsi?

Asilimia 85 ya wananchi wa Rwanda ni wa kabila la Hutu, lakini jamii ya Tutsi imekuwa ikishikilia nyadhifa kubwa tu za ngazi za juu kwa miaka mingi.
Mwaka 1959, wahutu walimuondoa mamlakani mfalme wa Tutsi huku maelfu ya watu wa kabila hilo wakikimbilia nchi jirani kama vile Uganda.
Kikundi cha watutsi waliokuwa ukimbizini kikaunda vuguvugu waliloliita RPF ambalo lilivamia Rwanda mwaka 1990 huku vita vikiendelea hadi mwaka 1993 ambapo makubaliano ya amani yalifikiwa.
Lakini usiku wa terehe 6 Aprili mwaka1994, ndege iliyokuwa imewabeba hayati Rais Juvenal Habyarmana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira ilidunguliwa.
Kila mtu aliyekuwa katika ndege hiyo alifariki. RPF kilisema kuwa ndege hiyo iliangushwa na wahutu kama kisingizio cha mauaji kufanyika.

Waume waliwaua wake zao kwa hofu ya wao kuuawa

Mauaji ya Kimbari yalifanyika vipi?

Kwa mpangilio wa hali ya juu. Orodha ya majina ya waliokuwa wanapinga serikali ilitolewa kwa wapiganaji ili waweze kuwaua pamoja na familia zao.
Majirani waliuana na hata waume wa kabila ta Hutu kuwaua wake zao wa Tutsi wakisema kuwa wangeuawa ikiwa wangetaa kufanya hivyo.
Wapiganaji walitumia vitambulisho vya watu kuwaua kwani majina yao yalionyesha ikiwa walikuwa wahutu au watutsi. Maelfu ya wanawake walifugwa kama watumwa wa ngono


Jumuiya ya kimataifa ililaumiwa pakubwa kwa kutizama tu mauaji yalipokuwa yanaendelea Rwanda

Nani alijaribu kusitisha vita?

Umoja wa Mataifa na Ubelgiji zilikuwa na wanajeshi wao nchini Rwanda. Lakini umoja wa Mataifa haukuwa na idhini ya kusitisha mauaji.
Mwaka mmoja baada ya wanajeshi wa Marekani kuuawa Somalia, Marekani ilijitahidi kadri ya uwezo wake kujizuia kuingia katika vita barani Afrika.
Wanajeshi wa Ubelgiji walilazimika kuondoka nchini humo baada ya kumi kati yao kuuawa.
Walituhumiwa kwa kutofanya juhudi za kumaliza vita. Rais Paul Kagame ametuhumu Ufaransa kwa kuhusika na mauaji hao ingawa Ufaransa imekanusha vikali madai hayo.

Vita vilimalizika vipi?

Chama cha RPF kikisaidiwa na Uganda , kilianza kudhibiti sehemu kadhaa za nchi hiyo hadi Julai tarehe 4, wanajeshi wake walipoingia mjini Kigali.
Wahutu milioni mbili wengi wakiwa raia walikimbilia nchi jirani ya DRC wakihofia kushambuliwa kama hatua ya kulipiza kisasi.


Watu milioni mbili wa kabila la Hutu walikimbilia nchi jirani kuepuka kisasi cha watutsi

Vipi hali ya Rwanda sasa?

Rais Paul Kagame na chama chake RPF amesifiwa kwa kurejesha utulivu nchini Rwanda na hata kukuza uchumi wa nchi hiyo ndogo.
Pia amejaribu kuifanya Rwanda kuwa nchi inayong'aa kiteknolojia. Lakini wakosoaji wake wanasema kuwa hapendi kukosolewa huku vifo vya wapinzani wake vikileta shaka.
Takriban watu milioni mbili walihukumiwa katika mahakama za jadi, viongozi wa mauaji wakihukumiwa katika mahakama maalum kuhusu mauaji ya Rwanda mjini Arusha Tanzania.
Kwa sasa ni hatia kwa mtu yeyote kuzungumzia ukabila nchini Rwanda, serikali inasema hii inasaidia kuzuia kutokea tena kwa mauaji kama hayo, lakini wakosoaji wa serikali wanasema hiki ni kiini macho tu kwani hisia zilizopo kuhusu ukabila huenda zikasababisha hali nyingine mbaya baadaye ikiwa watu hawatapewa uhuru wa kuzungumza.

TAMKO LA CHADEMA KUPINGA UCHAGUZI MDOGO CHALINZE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinatoa tamko la awali kwa umma kuhusu ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia uchaguzi, zilizofanyika kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chalinze, ambao umehitimishwa Aprili 6, mwaka huu, kwa wapiga kura wa jimbo hili mkubwa kupiga kura.

Ukiukwaji huo ni kama ifuatavyo;

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza wapiga kura wapya kinyume cha sheria
Kinyume kabisa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 15(5), kinachosema; 

“Kwa madhumuni ya kifungu hiki, Tume itapitia upya daftari la kudumu la taifa la wapiga kura mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na tarehe inayofuatia siku ya uteuzi,”
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekiuka kifungu hiki cha sheria kwa kufanya kile wanachoita wao ni ‘uhakiki wa mwaka 2014’ wa daftari ambao wanadai lengo lake lilikuwa ni kupunguza idadi ya wapiga kura waliokufa au kuhama au kuandikishwa mara mbili, lakini badala ya wapiga kura kupungua, uhakiki huo uliofanywa na tume bila kushirikisha wala kuwataarifu wananchi wa Jimbo la Chalinze, umeongeza idadi ya wapiga kura wapya katika jimbo hili kwenye uchaguzi huu mdogo.

Vile vile, kutokana na kitendo hicho cha NEC kuongeza idadi ya wapiga kura wapya kwenye daftari kimesababisha kuongezeka kwa vituo vya kupigia kura tofauti na ilivyokuwa mwaka 2010, ambapo Jimbo la Chalinze lilikuw ana jumla ya vituo 286 na sasa vimekuwa 288.

Kutangaza matokeo kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi >>>>