Thursday, February 28, 2013

MTANZANIA ATUNUKIWA UWAZIRI NCHINI RWANDA



RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.
Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera
Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.
“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.
Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.
Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.
Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.
Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.

IMAM ASHIKILIWA, ASKOFU MPEMBA ASAKWA NA JESHI LA POLISI


POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa Msikiti wa Ijumaa, huku likitangaza kuwasaka  masheikh wawili wengine   pamoja na Askofu (majina yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi wa kidini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema Imamu huyo wa msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya  kubainika kwamba wanahusika na usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa zikihamasisha vurugu pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.

Kwa upande wake Askofu  Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field  Evangelist  yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa video (DVD) yenye jina la ‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili wanasakwa kwa kuhusika na uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD) zenye majina ya ‘Unafiki katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Uadui wa Makafiri’.

Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (Bakwata) Mkoa wa Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata Taifa kufuatia hatua ya Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua madaraka Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata utaratibu.

CHANZO: MWANANCHI

DROGBA RUKSA KUKIPIGA KLABU BINGWA ULAYA


Benedikt Howedes and Didier Drogba
DIDIER Drogba ruksa kuitumikia Galatasary ya Uturuki kwenye michuano ya kombe mabingwa Ulaya baada UEFA kutupilia mbali malalamiko ya Schalke ya Ujerumani.
Nyota huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 34 alicheza mechi yake ya kwanza ya Ulaya dhidi ya Schalke Februari 20 katika mzunguko wa kwanza ulioishia kwa matokeo ya 1-1.
Schalke walilalamika kuwa mhezaji huyo hakusajiliwa katika muda muafaka kumuwezesha kucheza michuano ya Ulaya iliyofikia hatua ya mtoano.
Hata hivyo UEFA imetupilia mbali malalamiko hayo ambayo kama yangetia hatiani Galatasaray basi ingekwenda katika mechi ya marudiano ikiwa nyuma kwa bao 3-0 kwa mujibu wa kanuni za UEFA.

Tuesday, February 26, 2013

IMANI FM, KWA-NEEMA FM WAFUNGIWA MIEZI 6, CLOUDS FM WALIMWA FAINI KWA KUKIUKA MAADILI YA UTANGAZAJI

  • Ushoga waiadhibu Clouds Fm
  • Sensa ya mwaka 2012  yaiweka korokoroni Imani Fm
  • Mgogoro wa uchinjaji waiweka Lockup Kwa-Neema Fm
KATIKATI: Makam M/Kiti wa kamati ya maadili ya utangazaji nchini Bw. Wolter Bgoya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam

Kamati ya maadili ya utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadinli ya utangazaji.

Vituo vya radio vilivyofungiwa kutangaza ni IMANI FM cha mjini Morogoro na KWA-NEEMA FM cha jijini Mwanza ambavyo vyote vimefungiwa kwa muda wa miezi sita..

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam, Makam mwenyekiti wa kamati hiyo Walter Bgoya amesema kituo cha IMANI FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi ya 2012 na kituo cha KWA-NEEMA FM kinadaiwa kuchochea mgogoro wa uchinjaji kati ya waislam na wakristo mkoani Geita.

Akitangaza uamuzi huo Bwana Bgoya amesema kituo cha CLOUDS FM kimetakiwa kulipa faini ya Sh. 5 milioni na kufuta kipengele ( segment) cha jicho la ng'ombe kwani kimekuwa kikiendeshwa kwa kutofata maadili  na walihusii wa uchaguka katika kushabikia masuala ya ushoga wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa marekani.

CHANZO: Michuzi Blog na Jamii Forum






MWANAFUNZI WA CHUO CHA SAUT AJINYONGA NA KUPOTEZA MAISHA


Mwanafunzi Athanas Ernest wa chuo cha SAUT amejinyonga na kupoteza maisha leo asubuhi katika eneo la Malimbe .jijini Mwanza huku sababu za kujinyonga kwake zikiwa bado hazijafahamika.

Mganga wa Chuoni hapo  DR. Mnema amthibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo marehemu alijinyonga kwa kamba aliyoifunga kwenye kenchi ya dari chumbani kwake.
Marehem Athanas alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Sanaa na Elimu (Bachelor of Arts with Education) na alikuwa akiishi na mwanafunzi ambae alikuwepo eneo la tukio na jina lake halikuweza kutambulika mara moja kutokana na hali ya mazingira iliyokuwepo wakati huo.

Akikzungumza na Tanganyika One DR. Mnema amesema tukio hili ni la kusikitisha kwani hakuna aliyeamini kijana huyu msomi angeweza kufanya kitendo cha kujinyonga.
Tanganyika One ilipotaka kujua ni sababu zipi zilizopelekea kujinynga kwake, DR. Mnema alibainisha kuwa ni mapema mno kuzijua kwani hakuna maandishi yaliyoachwa na marehemu bali uatafanyika uchunguzi ili kubaini sababu zilizopelekea tukio hilo.

Kufuatia tukio hilo watu wametakiwa kuwa wawazi pingi wanapokabiliwa na matatizo ili waweze kusaidiwa. " watu wawe wawazi pindi wanapokabiliwa na msongo wa mawazo na matatizo ili waweze kupata msaada na kuepukana na vitendo kama hiv" alisema DR. Mnema huku akibainisha kuwa watu huwa wanachukua uamuzi kama huu ili kuepukana na matatizo yanayowasonga wakiamini kuwa kuko waendako wanakwenda kupumzika na hakutakuwa na matatizo kama yanayowakabili hapa duniani.

" Huenda huko kuna matatizo na shida kubwa kuliko zilizoko hapa duniani hivyo si vyema watu kuchukua uamuzi wa kujipeleka huko kabla ya wakati uliopangwa na Mungu. Alisema DR. Mnema  akiwaasa watu wasichukue uamuzi kama huo wakiamini watakwenda kupumzika matatizo yaliyoko duniani.

Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi.

Marehemu Athanas alikuwa ni mkazi wa Mpanda mkoani Katavi.

Mwandishi: Butije H.

POLISI WATUMIA NGUVU KUZUIA MAITI KUSAFIRISHWA MKOANI GEITA.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa kiasi cha Sh360 milioni kiliporwa. Kati ya fedha hizo, Sh60 milioni zinadaiwa kwamba zilikuwa kwenye gari wakati Sh300 milioni. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo.
POLISI wa Mkoa wa Geita wametumia nguvu kuzuia msafara wa waombolezaji waliokuwa na mwili wa marehemu mfanyabiashara, Yemuga Fungungu (48), mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vurugu kubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikuwapo wakati askari wake walipoingilia msafara huo na kusababisha vurumai kubwa.


Waombolezaji hao walikuwa wakiuhamisha mwili wa marehemu Fungungu kutoka Hospitali ya Runzewa kuupeleka katika Hospitali ya Geita.

Sakata hilo la ndugu na polisi lililotokea saa nane mchana juzi Jumamosi katika Pori la Samina, Geita na polisi wakiwa kwenye magari matatu wakiwa wamesheheni silaha mbalimbali walifika na kuzuia mwili wa marehemu kusafirishwa.

Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwamo mkewe, wanadai kwamba Fungungu alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi wanaosemekana kwamba walimvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita kisha kupora mamilioni ya fedha. 


Wanadai kwamba alipigwa risasi tumboni na kichwani katika Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe mkoani hapa.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa kiasi cha Sh360 milioni kiliporwa. Kati ya fedha hizo, Sh60 milioni zinadaiwa kwamba zilikuwa kwenye gari wakati Sh300 milioni zilikuwa kwenye masanduku mawili yaliyokuwa ndani ya nyumba.

Pia ndugu hao walidai kwamba Sh1.2 milioni zilichukuliwa na askari wawili wa kiume baada ya kumpekua mke wa marehemu kwenye nguo za ndani.

Pia askari hao wanadaiwa kupora mali mbalimbali za marehemu zikiwamo redio mbili, video kamera moja, nguo za marehemu ikiwamo kanzu, mashine ya printer, mashine ya inventor, karatasi za picha, deki mbili za kucheza CD, pamoja na nguo za mke wa marehemu.

Mapema Kamanda Paulo alikuwa ameeleza kuwa marehemu alijiua mwenyewe baada ya kumjeruhi Polisi, Fortunatus Beatus kwa risasi lakini taarifa hizo zimepingwa vikali na ndugu na jamaa wa marehemu ambao wanadai marehemu aliuawa na polisi akiwa nyumbani kwake.

Polisi kuzuia waombolezaji.

Baada ya polisi kuyasimamisha magari manane yaliyokuwa katika msafara huo wa kupeleka mwili wa marehemu kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Geita, kulizuka mabishano makali kati ya Kamanda Paulo na ndugu wa marehemu.

Inadaiwa kwamba polisi walikuwa wakishinikiza mwili huo urejeshwe Runzewe, Bukombe kwa kuwa tayari ulikuwa umefanyiwa uchunguzi jambo ambalo liliwakera waombolezaji hao.

Kabla ya kamanda huyo kufika eneo hilo, msafara huo ulisimamishwa na Polisi wa Usalama Barabarani ambao walikuwa wamefuatana na wale wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita, Leonard Makona.


Baada ya kuusimamisha msafara huo, Makona aliwataka ndugu wa marehemu kumsubiri Kamanda Paulo ambaye alifika baada ya takriban dakika 10.

Mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alishuhudia ndugu wa marehemu na Kamanda Paulo wakirushiana maneno.

“Mnapeleka wapi mwili wa marehemu, ina maana hamkuridhika na uchunguzi wa daktari wa Bukombe?” alihoji kwa ukali na kujibiwa pia kwa ukali na kaka wa marehemu, Mariatabu Fungungu: “Kwa nini mnatusimamisha ?. 


Tunaomba tuite waandishi wa habari hapa ili waje washuhudie tukio hili. Kwa nini msikae ofisini ?”.

CHANZO: http://www.mwananchi.co.tz

Friday, February 22, 2013

FINANCIAL TSUNAMI -TIJA KWA AFRIKA WABADILISHE MFUMO WA KIBENKI


 

Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEBAINIKA kuwa, Mfumo wa kuwekeza fedha Benki  kwa  Riba ni anguko la viwanda vya kimataifa na kudumaa kwa uchumi wa Nchi za Afrika.
Kauli hiyo imebainishwa  na Mkurugenzi  wa  huduma ya benki isiyo na riba NBC  Yassir  Masoud  Kigoma Ujiji  jana  kwenye warsha ya wadau wa uwekezaji wa fedha katika mabenki mbalimbali  wakibainishiwa  mfumo wa riba na athari zake na chukizo kwa mungu  ikiwa na tija ya kufuata  mfumo usiokuwa na riba ( Islamic Banking) ambao  unaridhiwa na mungu  kwa wananchi wa imani zote za dini hali itakayochochea  kupanda kwa uchumi wa  mmoja mmoja sanjari na  kukua kwa huduma za  wananchi .
“Mfumo wa kuwekeza bila riba unaepusha ugomvi baina ya benki husika na mteja ,wateja wengi wanauziwa thamani zao kutokana na kushindwa kulipa riba ya fedha alikyokopeshwa,sasa itumieni huduma hii ambayo hata mataifa ya magharibi ikiwemo marekani ,malasia,Singapore wamebaini hili wanatumia  mfumo kama Islamic banking msitishike na jina ni kwa wote wahitaji” alibainisha Masoud.
Meneja  wa  NBC-Tawi la Kigoma  Mathias  Mhangilwa alisema kuwa,mfumo wa Islamic Banking ni uwekezaji wa fedha unaolenga uhalisia wa maumbile ya mwanadamu ambao unauadilifu kwa mafundisho ya vitabu vyote vinakataza riba haimanishi ni kwa ajili ya imani ya kislamu tu ni kwa kila mdau  huku akiwataka  wafanyabiashara wa kigoma wachangamkie fursa hiyo ili waboreshe tija zao.
“ World Bank inafanya mchakato wa kuhakikisha kuna sera  ya mfumo huu usiokuwa na riba ,pia mfumo huu hauna anguko la kiuchumi kwani anguko ni chachu ya fedha haramu ya riba watanzania tumechelewa  kujiunga na mfumo huu,lakini sasa utumieni ili nchi yetu isiyumbe kiuchumi ikiwa mataifa ya magharibi yataanguka cha ajabu 30% waliwekeza mfumo huu ni wakristo na 2% waislamu msihofu ” alisisitiza Mhangilwa.
Khadija Katumba  na Asha Issa walidai kuwa,kutokana na elimu waliyoipata  toka kwa NBC-Isalamic Banking ,juu ya adha ya  mikopo ya riba watakuwa mabalozi wa elimu hiyo kwa wanawake wathubutu wa kufanya biashara waachane na mfumo wa udhalilishaji ambao wengi wameuziwa majumba yao kutokana na riba ambaye ni sawa na mdudu wa kansa kwa kumaliza uchumi wa wajasiliamali wasio na elimu juu ya mikopo ya riba.
Ikumbukwe kuwa,wadau wa uwekezaji ni wahanga wa kufilisiwa thamani zao na Benki mbalimbali za hapa nchini pindi wanaposhindwa kulipa deni la mikopo, hali iliyopelekea Benki ya Taifa NBC kuanzisha huduma hiyo ambayo kwa sasa unatumiwa ulimwenguni na mataifa ya magharibi na Asia wakijaribu kufutu (Financial Tsunami) anguko la kiuchumi siku za usoni kwa mujibu wa mwanazuoni wa zamadamu  bara la Asia anayejulikana kama Ibn Qayyim Jawziyya.

Sunday, February 17, 2013

KWA NINI NI RAHISI WATU KUINGIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA NJIA YA MTANDAO?

Teknolojia ya Mtadao ... inawezesha kuwa na uhusiano wa kasi na wa moja kwa moja, 

Mawasiliano ya mtandao humpa mtu uwezo na nafasi ya kuuliza maswali ambayo pengine mtu angeshindwa kuyauliza uso kwa uso wakati huo.

Wale ambao hukutana katika chumba cha giza, kwa ujumla, huwa huru zaidi ya wawazi na wenye  ukaribu sana, kwa washiriki wenzao kuliko wale ambao hukutana uso kwa uso kwenye eneo la wazi na angavu. 

Kwa kifupi:, watu kujisikia huru zaidi kuwa wao wenyewe na kupata kujua kila mmoja. Hivyo ni rahisi watu kujikita kwenye mahusiano kupitia mtadao kuliko njia ya ana kwa ana.

 "Upendo Mtandaoni: Hisia kwenye mtandao."  Huwezesha kuendeleza kwa mazungumzo ya mapenzi  ikilinganishwa na mazungumzo ya ana kwa ana au mfumo  wa barua. 

Saturday, February 16, 2013

PINDA AKATAA MABUCHA YA WAISLAM NA WAKRISTO


 

v  Aagaiza utaratibu ulokuepo kwa muda mrefu uendelee mpaka kamati itakayoundwa ipate muafaka
v  Ataka kamati ya viongozi wa madhehebu ya dini iundwe haraka kupata muarobaini wa tatizo hili
             
                  By Butije Hamisi
Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Mizengo pinda ameagiza utaratibu uliokuwepo kwa muda mrefu wa waislam kuchinja katika machinjio ya umma uendelee mpaka hapo kamati inayoundwa ya maafikiano ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kiislam na kikristo itakapokaa na kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kikao cha viongozi wa madhehebu ya kiislam na kikristo kilichofanyika katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza Pinda amesema   serikali haiko tayari kuona mgawanyiko baina ya watanzania kwa kuruhusu mabucha ya wakristo na waislam kwani mgawanyiko hautoishia hapo utakwenda mbali zaidi katika Nyanja za kijamii. 

“ Jambo hili si la kisheria, ni jambo ambalo limeibuka kwa maridhiano ya kuheshimiana madhehebu haya makubwa mawili kwa muda mrefu. ” alisema Pinda na kuwataka viongozi wa dini kuendeleza utamaduni huu ili kujenga amani, utulivu na mshikamano baina ya watanzania.

Waziri pinda amesema yapo "makandokando" yaliyojitokeza na kutochukuliwa hatua haraka ndio yaliyoleta  kuchocheachochea fikra hizi nakufanywa kuwa ajenda mojawapo kati ya ajenda za msingi.
Pinda amemuagiza mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh Evarist Ndikilo kusimamia shughuli za kamati inayoundwa ili kufikia muafaka wa tatizo hili haraka iwezekanavyo
Habari zilizoifikia Tanganyika One zinaeleza kuwa kamati hiyo itakuwa na wajumbe ishirini, kumi wakiwa viongozi wa kiislam na wengine 10 viongozi wa kikristo.

 Pinda ametahadharisha kuwa mgawanyiko huu utaziathiri taasisi kama magereza, jeshini,bunge na taasisi zingine za umma kwa kutenga nyama ya wakristo na nyama ya waislam na hivyo kupelekea watu kujigawa kwa kila jambo kitendo ambacho kinahatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Katika kikao hicho vituo vya radio vya Kwaneema Fm na Radio Iman na DVD zilizopo mitaani za Sh. Ilunga vimelalamikiwa kuchangia kukua kwa mgogoro huu na mamlaka husika kushauriwa kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia vyombo hivyo kuendeleza chuki kwa watanzania.

Meshimiwa Pinda natarajiwa Kesho kwenda mkoani geita ikiwa ni moja ya jitihada za serikali kutatua mgogoo huu.

Hivi karibuni waziri wa nchi Ofisi ya rais uratibu na mahusiano Mh Stevine Wasira aliagiza wakristo wanaruhusiwa kuchinja majumbani kwao na katika shughuli zao binafi na waislam waengdelee kuchinja kayika machinjio ya umaa.

SAKATA LA MGOGORO WA UCHINJAJI;


KIKAO KATI YA WAZIRI MKUU MH MIZENGO PINDA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA DINI KINAENDELEA KATIKA UKUMBI WA BOT JIJINI MWANZA. MH PINDA AMEKUJA KUSULUHISHA MGOGORO HUO BAADA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH EMANUEL NCHIMBI KUSHINDWA KUTATUA MGOGORO HUO KATIKA ZIARA ALIYOIFANYA MKOANI GEITA WIKI HII.
TAARIFA KAMILI ITAKUJIA PINDI TUTAKAPOFANYA MAHOJIANO NA WAZIRI MKUU.

Wednesday, February 13, 2013

JK AWATOSA CC WAWANIA URAIS 2015


MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameamua kuwatosa vinara wanaotajwa kutaka kuwania urais kupitia chama hicho kutoingia kwenye Kamati Kuu (CC).
Dalili za kuwatosa vinara wanaotajwa kuwania urais 2015, ni kutokana na hatua yake ya juzi kuamua kutowapendekeza kuwa miongoni mwa majina ambayo yangepigiwa kura ili kuweza kuingia katika CC.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa ndani na nje ya CCM wanaona hatua ya Kikwete kutopendekeza majina ya wanasiasa vigogo wanaotaka urais 2015 kupitia chama hicho katika orodha ya watu 42 ili kuwania nafasi 14 za CC kama mkakati maalumu wa kuwaweka kando.

Hata hivyo, mkakati huu wa Kikwete ulikuwa hatua muhimu kwake kama kiongozi wa chama baada ya kukwama kuzuia makundi kung’ara katika chaguzi zilizopita ambapo wafuasi wa Edward Lowassa waliibuka kidedea kuanzia katika NEC, mikoani na Jumuiya za chama hicho.
Ndiyo maana baada ya kumalizika Uchaguzi wa wajumbe wa NEC, Kikwete alisita kuunda CC kwa maelezo kwamba waliochaguliwa walikuwa wageni na alikuwa hawafamu vizuri. Hatua hii ya Kikwete ilitafsiriwa kama mkakati wa kuzima nguvu ya mojawapo ya kambi.

Hata hivyo, kuna mtazamo tofauti kwamba hatua ya Kikwete kutopendekeza majina makubwa na yenye nguvu ndani ya CCM kuwania ujumbe wa Kamati Kuu inaweza ikawa ni njia ya kuwafanya wajumbe wa CC kuwa na kazi moja tu ambayo ni kuchuja majina ya wagombea badala ya wao pia kuwa washiriki.
Bebard Membe, Samuel Sitta na Edward Lowasa

Katika hali iliyozua gumzo, majina ya wanasiasa vigogo Edward Lowassa, Benard Membe na Samuel Sitta ha yakuwamo katika orodha ya Rais Kikwete aliyowasilisha mbele ya NEC ili kupata wajumbe wa CC, ambacho ni chombo muhimu cha uamuzi ndani ya chama hicho.

Lowassa, Membe na Sitta ndiyo wanaelezewa kuwa na makundi makubwa yana yowaunga mkono kiasi cha kutishia uhai wa chama hicho katika chaguzi zijazo.
Makundi ya watu hao yamekuwa hasimu kiasi cha wakati fulani, Kikwete kulazimika kuunda kamati ya watu watatu chini ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana, ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho kwa sasa ili kusuluhisha mgogoro huo.
CHANZO: MWANANCHI

ZITO: UBADHILIFU WA SHILINGI TRILIONI 1, MKATABA WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA MTWARA CHANZO CHA KUFUTWA KAMATI YA POAC



Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), Zitto Kabwe amesema ubadhiliu wa shilingi trilioni 1 na mkataba wa ujenzi wa bomba ka mafuta Mtwara ni chanzo cha kufutwa kwa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya uma (POAC)

Akizungumza katika mikutano wa hadhara jijini Dar es Salam ikiwa ni muendelezo wa  mchakamchaka wa chama hicho ulioanzia bungeni wa kutaka hoja zake zisikilizwe baada ya kutupiliwa mbali kimizengwe bungeni.

Zitto ametaja sababu ya kufutwa kwa kamati hiyo kuwa ni utendaji wa kamati hiyo uliogundua matumizi ya zaidi ya Sh1 trilioni kutoka kwenye mifuko ya pensheni zilizotumika katika kampeni za CCM, na ujenzi wa vyuo vikuu vya Dodoma, Hombolo na Chuo Kikuu cha Arusha Nelson Mandela.

“Spika lazima ajue kwamba mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la Wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi yetu itaumia,” anasema Zitto.

Zitto aligusia pia sakata la Mtwara akisema kamati iliyofutwa ililitaka Shirika la Maendeleo ya Mafuta (TPDC) kuonyesha mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta, wakaahidi kuupeleka ifikapo Aprili mwaka huu.

“Tulipowataka TPDC watuletee mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi wakasema uko wizarani. Katibu Mkuu ambaye anapaswa kwenda kujieleza kwenye Kamati ya Nishati na Madini hakwenda kwa kuwa kamati hiyo pia imefutwa. TPDC wakasema watauleta Aprili. Ndiyo hivyo kamati yetu nayo imefutwa.”

Wabunge wa upinzani waliowasilisha hoja zao ni pamoja na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia aliyetaka mfumo wa elimu nchini ufumuliwe au kuboreshwa, kero ya maji jijini Dar es Salaam iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika

Hali hiyo ilizua vurugu na matokeo yake hoja nyingine binafsi za wabunge, ikiwamo ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari aliyetaka kujadiliwa kwa mwenendo wa Baraza la Mitihani la Taifa na jinsi linavyoathiri mfumo wa elimu nchini, ziliahirishwa kwa muda usiojulikana.

Mbali na kuzitupilia mbali hoja hizo, Bunge hilo lilimalizika likiifuta Kamati ya Bunge ya Mashirika ya umma iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Katika mkutano wa hadhara, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara), Zitto Kabwe anasema Spika wa Bunge, Anna Makinda ameshindwa kuwajibika na hivyo anapaswa kung’olewa kutokana na kutaka kuirudisha nchi kwenye kipindi cha kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (Epa).

Zitto aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, anasema imefutwa kwa mbinu za CCM kuzima sauti ya wabunge wa upinzani wanaozungumzia maslahi ya wananchi.

CHANZO: MWANANCHI

Tuesday, February 12, 2013

MAPIGANO YA KIDINI GEITA YASABABISHA MAUAJI


MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania (PAGT) Buseresere, Wilaya ya Chato, Mathayo Kachila (45) amefariki dunia na watu 15 wakijeruhiwa kwa mapanga kufuatia vurugu inayotokana na mgogoro wa bucha.
Tukio hilo lilitokea jana saa 2 asubuhi kwenye Soko la Buseresere baada ya kundi la wananchi kuvamia bucha iliyokuwa na maandishi ya ‘Bwana Yesu Asifiwe, Yesu ni Bwana’, kuwataka waliokuwa wakiuza kuifunga hali iliyozusha vurugu.

Inadaiwa kabla ya kufunguliwa kwa bucha hiyo, Wakristo walifanya mkutano wa Injili Uwanja wa CCM Katoro na kutangaza kuwa, watachinja nyama yao na kuiuza kwenye bucha maalumu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wananchi hao wanaodaiwa kuwa waumini wa Kiislamu walikuwa wamechukizwa na kufunguliwa kwa bucha hiyo, ndiyo wakachukua uamuzi wa kwenda kuamuru ifungwe.

“Tulipata taarifa za kufunguliwa kwa bucha hii na tulipofika kuwaomba waache kuuza nyama yao, waligoma na kuendelea kuuza, baada ya kuona hilo wafuasi wa Dini ya Kiislamu walikimbilia msikitini na kuunda kikosi cha kupambana nao,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Chato, Yusuf Idd.
Alisema licha ya kuwasihi hawakumsikiliza, waliamua kwenda kupambana.

Katika vurugu hizo, duka la Idd lilivunjwa na kuporwa simu na fedha, huku pikipiki mbili ambazo hazijafahamika wamiliki zilichomwa moto.
Katika vurugu hizo nyama ndani ya bucha hiyo ilimwagiwa maji, ikiwamo kuharibiwa kwa madirisha na milango yake.

Licha ya majeruhi kutajwa kuwa 15, waliotibiwa Kituo cha Afya Buseresere na kuruhusiwa ni Abdallah Shaaban (25), Abubakar Shaaban (27), Faruk Shaaban (14), Kassim Almasi (23), Yusuf Shaaban (18), Bilal Hassan na Abdallah Ibrahim.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk John Lumona alisema majeruhi wengine waliofikishwa ni Yasin Rajabu (56), Said Taompangaze (47), Masoud Idd (21), Ramadhan Pastory (36), Haruna Rashid (61) na Sadiq Yahya (40), ambaye hali yake ameieleza kuwa mbaya na alipelekwa Hospitali ya Rufani Bugando.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geira, Paul Katabago alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo aliwataka wananchi kutulia kwa vile suala hilo linashughulikiwa na serikali na litapatiwa ufumbuzi.

Monday, February 11, 2013

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI YAKE February 28 MWAKA HUU


Akitangaza maamuzi hayo Papa Benedict alisema ameamua kujiuzuru kwa sababu hana nguvu tena za kuendelea na majuku yake ya ofisi.
Papa Benedict mwenye umri wa miaka (85) alisema kwamba amekuwa na maamuzi hayo ya kujiuzuri tangu mwezi uliopita.
"Nimefikia kiwango ambacho siwezi tena kuendelea na majukumu yangu ya kutoa huduma na siwezi kutimiza majukumu yangu ipasavyo ofisini” alisema kupitia taarifa yake iliyotolea na Msemaji wa Vatican.

Papa Benedict anatarajia kukabidhi ofisi  yake rasmi february 28 mwaka huu.
Papa Benedict amekuwa wa kwanza kujiuzuri nafasi hiyo tangu Kanisa la Roma duniani kuweka utaratibu wa kuongozwa na kiongozi huyo kwani Papa hutakiwa kulitumikia Kanisa hilo mpaka atakapofariki dunia.

Hatua hiyo itatoa mwanya kwa Kanisa katoliki kufanya uteuzi wa Papa mwingine atakayechukuwa nafasi yake
CHANZO:  Reuters

VURUGU KATI YA WAISLAM NA WAKRISTO ZASABABISHA FIFO VYA WATU WAWILI


Vurugu zilizoibuka leo kati ya waislam na wakristo katika eneo la Buselesele mkoani Geita zimesababisha vifo vya watu wawili na wangine kadhaa kujeruhiwa.

Vurugu hizo zimeibuka baada ya baadhi ya  waumini wa kikristo  kuendesha zoezi la kuchinja nyama ya ngombe wakitii agizo lililotolewa na viongozi wa mwadhehebu ya kikikristo mkoani mwanza kuwaagiza wakristo kuacha kula nyama iliyochinjwa kwa imani ya kiislam na kuwataka wachinje nyama yao kwa mujibu wa imani ya kikristo.

Habari zililoifikia Tanganyika One zimedai kuwa waliopoteza maisha ni mchungaji wa kanisa moja pamoja na muumuini wa dini ya kikristo.

Kwa sasa hali ya utulivu imerejea na kikao cha kamati ya ulinzi ulinzi na usalama ya mkoa wa geita ipo kwenye kikao cha dharura kujadili kadhia hiyo

CHANZO: MAHOJIANO 

Sunday, February 10, 2013

UTALII WA NGONO WASHAMIRI NCHINI


Vijana wa kitanzania wawapagawisha wanawake wa kizungu, na kuwa vivutio vya utalii huo
 “apewe mpaka apagawe, atoe tiketi.” ni kaulimbiu inayotolewa na vijana hao kupata tiketi ya kwenda ulaya.
 Kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar.
Wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka 60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.
Uchunguzi huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta mwanamume atakayestarehe naye kingono.
Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa kustarehe nao.
 Utalii huu umeshamiri nchini, ambapo vijana wa Kitanzania wanaufahamu na kukiri kuwa umewanufaisha na baadhi yao kuwasaidia kupata tiketi za kwenda kuishi Ulaya.
Katika Visiwa vya Zanzibar utalii huo unafanyika zaidi katika fukwe za Nungwi, Kiwengwa, Paje, Kendwa, Jambiani na maeneo mengine yaliyopo pembezoni mwa bahari.
Katika fukwe hizo vijana maalumu kwa kazi hiyo, wana kauli mbiu yao inayosema:“apewe mpaka apagawe, atoe tiketi.”
Kwa kauli mbiu hiyo vijana hao wanamaanisha kuwa, kwa kila mwanamke watakayekutana naye, watatumia kila mbinu ili kumfurahisha hadi awasafirishe au kwenda naye Ulaya.
Abdulla Ali Haji (Sio jina halisi) ni miongoni wa vijana wanaojihusisha na aina hiyo ya utalii, akiishi visiwani humo ambapo anaeleza kuwa shughuli yake kubwa ni kuzunguka katika fukwe mbalimbali akiwinda wanawake wa kizungu wanaotaka kustarehe.
CHANZO: MWANANCHI

Wednesday, February 6, 2013

Wataka wanawake waruhusiwe kuchumbia


MKAZI wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Phillipo Tango (25), amependekeza Katiba Mpya itoe haki na usawa katika suala la ndoa kwa wanawake kuruhusiwa kuchumbia, kutoa mahari na kuoa wanaume wanaowapenda na kukubaliana.
Akitoa maoni yake mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya juzi, Tango ambaye ni mkazi wa Kata ya Olmotonyi, wilayani Arumeru alisema lazima Katiba hiyo mpya ikomeshe mfumo dume unaotawala suala la ndoa.
“Katiba itoe haki sawa kwa jinsi zote mbili katika suala la kuoana na haki zote za ndoa tofauti na sasa ambapo wanaume ndiyo wenye maamuzi makubwa kulinganisha na wanawake,” alisema Tango.
Kwa upande wake, Makamba Meshilieki (32), mkazi wa kijiji cha Ngaramtoni yeye alipendekeza wabunge na madiwani kuingia mikataba na wananchi wa maeneo yao kuhusu utendaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mara baada ya kushinda uchaguzi.
Alipendekeza pamoja na kuonyesha muda wa utekelezaji, mkataba baina ya wabunge, madiwani na wananchi kutaja adhabu atakayostahili kiongozi anayeshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii.
“Mbunge au diwani atakayeshindwa kutimiza yaliyoahidi katika mkataba wachapwe viboko 60 hadharani ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia ya kutoa ahadi zisizotekelezeka kipindi cha kampeni za uchaguzi,” alisema Tango.
Emanuel Mollel (44), yeye alitaka Katiba Mpya kuwazuia viongozi na watendaji Serikalini, mashirika na taasisi za Umma kufanya biashara wakiwa madarakani ili kudhibiti migongano wa kimaslahi.
Alisema viongozi kuendelea kushiriki shughuli za kibiashara wakiwa madarakani kunachochea vitendo vya ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya madaraka na ofisi za umma kwa faida na maslahi binafsi.

CHANZO: MWANANCHI

Monday, February 4, 2013

MAANDAMANO KUSHINIKIZA DHAMANA YA SHEIKH PONDA YAANDALIWA


Sheikh Ponda Issa Ponda
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetangaza kuwa zitaandamana Februari 15, mwaka huu endapo Katibu wa Jumuiya hiyo, Shekh Ponda Isa Ponda, pamoja na wenzake walioko gerezani hawatapewa dhamana Februari 14.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Amiri Mkuu wa Shura ya Wahadhiri Tanzania, Kondo Bungo, wakati wa kongamano la mwendelezo wa kuwainua Waislamu waweze kudai haki zao lililofanyika katiak viwanja vya Shule ya Sekondari ya Nuruyakin, Temeke, jijini Dar es Salaam.
 
“Kupewa dhamana ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania, haiwezekani hadi leo (jana) wenzetu wanasota jela kwa kosa la kutetea haki zao na wakati wapo watu waliotuhumiwa kuua wamepewa dhamana, lakini Waislamu wananyimwa, kwa sasa hatutakubali, lazima kieleweke,” alisema Bungo.
 
Alisema kama dhamana haitapatikana siku hiyo, wataandamana hadi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwani aliyewanyima dhamana viongozi wao ni yeye (DPP)na siyo mahakama.
 
Sheikh Bungo alisema wapo viongozi wengi wa Kiislamu kutoka bara na visiwani waliokamatwa kwa sababu ya kutetea haki za Waislamu na badala yake kubadilishiwa makosa wanapofikishwa mahakamani ili ionekane kuwa wana makosa.